Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Tanzania sio kubwa acha chai
Mzee Baba kama hujatembea ila linchi likubwa japo naona unataka fananisha na Russia. Nchi kubwa sana hii na ina mapori Mengi sana. Mara ya Kwanza natoka Nyumbani Arusha naenda Katavi pitia Tabora ndio niliona linchi lilivyo kikubwa. Kuna kipindi nilitoka Kagera kwenda Kugoma via Nyakanazi. Sio kwa Misitu ile.
 
Kinaitwaje mkuu?
 
Tangeni bila shaka[emoji16] siku ya jumapili wanashuka milimani kuja kugonga kitimoto
Mkuu Tangeni hapo jirani na Mzumbe University? Hiyo labda itakuwa Bunduki au kule Juu kabisa ya Kijiji kinaitwa Nyandira..
 
Tanzania sio kubwa acha chai
Ukubwa wa Tanzania ni 945,087 km²... Yaani ukiunganisha Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda labda ndiyo itakaribia... Kwa ukubwa wa hii nchi ili kila eneo lipate maendeleo ya haraka ilikuwa ni vema kuwa na mfumo wa majimbo, yaani mfano Kigoma, Katavi na Rukwa jimbo moja hilo ambalo linapewa mamlaka ya kutumia sehemu ya asilimia from their resources kwa maendeleo yake...
 
Nenda Morogoro shuka msamvu, chukua bodaboda akupeleke hadi shule ya msingi kikundi, nauli 1500.
Ukifika pale angalia mlimani kule watu wamejenga mlimani yaani. Sasa unajiuliza hawa watu hata mabati walipelekaje kule!
Niliwahi kwenda kijiji kinaitwa Lunenzi, huko wilayani Kilosa. Huko kila kitu kinabebwa kwa kichwa mpaka simenti, nondo, bati etc..
 
Kijij hcho Cha ngiyeke naifahamu Kuna mtu wa kijij. Hicho aliwai nitapeli Kijiji unaacha ipinda kwa nyuma Kisha unaanzaa kuikabili mlima wanyakyusa Ni wengi mno Nan Ni wale wa oh kbsa

Sent from my Infin
 
Ukifika siha na hai Barbara ya kwenda merarani hutatamani

Pia same na mwanga ni pa hovyo mno
Mwanga kwenda wapi? Maana kama ni kwenda milimani usangi au ugweno kuna lami mpaka pale Kikweni... Same napo kumekuwa sanaa
 
Pia walikimbilia huko milimani ili wasikamatwe utumwa na waarabu..
 
Tanzania kubwa sana ndugu yangu, na ina mila na desturi na maisha ya kila namna. Naomba Mungu siku moja nikipata fedha ya ziada nitafanya ziara Tanzania nzima au sehemu nyingi kadiri niwezavyo. Sehemu kama hizo ambazo wengi wamezizungumzia hapa.
Tatizo letu sisi hatupendi kutalii na kujifunza kuhusu nchi yetu na mikoa yetu. Kuna siku nimeshangaa kwenye kundi la watu 10 ni watu 4 tuu ndiyo wametembea nusu ya mikoa ya nchi hii.. Sasa how can one learn na kuona fursa bila kutembea? Babu yangu pale Kijijini alikuwa very smart na mjuzi wa mambo mengi na wengi walikuwa wabamtegemea.. Mara zote nikimuuliza mbona unajua vitu vingi sana kuliko wenzako? Jibu lake lilikuwa mjukuu wangu tembea uone na ujifunze, ukisikia elimu dunia maana yake ni kutembea na kuona na kujifunza kwa wengine.
 
Kapanga nimepita majuzi tuu mkuu pamebadilika sana. Mishamo nilifika pia [emoji23] [emoji23]
 
Mwanga kwenda wapi? Maana kama ni kwenda milimani usangi au ugweno kuna lami mpaka pale Kikweni... Same napo kumekuwa sanaa
Nahisi anazungumzia hali ya lile Jangwa pale tambarare ya Mwanga na Same

Huko juu at least hali ya hewa ni nzuri japo udongo mkavu hauna rutuba kabisa, vindizi vinatoka vigumu kama mawe

Kule napo pagumu sana aisee
 
Hapo ndio umefafanua kitaalamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…