Vijiji vya Vunta na Kidunda, Hedaru, wilaya ya Same.
Ni vijiji vilivyo milimani - ktk Safu ya milima ya Usambara.
Ukitokea Mombo, kabla ya kufika Hedaru, unakata kulia na kuanza songombingo la kupanda mlima kuelekea vijiji hivi.
Issue hapa ni barabara ya vumbi yenye slope kubwa ajabu! Dereva akifanya kosa kidogo tu, mmekwisha kwani gari litaserereka bondeni takribani mita 600 - 800 hadi litakapogonga mwamba na kusimama! Bila gari imara lenye 4-W, huwezi kwenda kule.
Wakati wa kurudi toka Vunta, nilimuuliza mwenyeji wangu kuwa kwanini hawa Wapare waliamua kwenda kuishi sehemu hatarishi kama zile? Aliniambia kuwa, Wapare walikimbilia kwenda kule kwa ajili ya maficho kutokana na vita kati yao na maadui zao pamoja na maasidi wao - Wachagga. Ilikuwa zamani sana kabla ya ujio wa Wakoloni.
Baadaye waliweka makazi mpaka leo.