Ukifika siha na hai Barbara ya kwenda merarani hutatamani
Pia same na mwanga ni pa hovyo mno
Hayo maeneo ya kawaida sana, hakuna kipya kibaya au kitu cha ajabu. Jiografia yake ndio inaweza kukutisha lakini ukipakaribia utagundua pako poa.
Mahali penye barabara inayopitika majira yote na huduma zote muhimu za kijamii, sio mahali pa ajabu.
Kwa mfano, kwa Kilimanjaro, eneo kama wilaya ya Mwanga (maeneo ya huko milimani).
-Pana barabara ya lami kutoka tambarare mpaka juu kileleni mwa milima huko kwenye vijiji vya wapare (sijui Usangi, Ugweno?), na usafiri wa umma unaelezwa kuwepo wakati wote wa siku, kuanzia alfajiri mpaka mida ya usiku. Sijui serikali iliamua kuwapendelea? Maana hakuna shughuli yoyote ya maana ya uzalishaji kama kilimo nk.
-Tanesco wanasema mtandao wa umeme ulifika huko milimani tangu miaka ya 1980, na kwa sasa zaidi ya 90% ya kaya zao zina umeme.
-Hayo maeneo mbali ya kuwa na vituo vya afya vya kutosha, inaelezwa wana zahanati karibu kila kijiji, shule kila kijiji, maji ya bomba karibu kila kaya, vituo vya polisi, mahakama nk.