Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Sehemu pekee ya kushangaa kwamba binadamu mwenye akili timamu anawezaje kuishi ni bonde la Msimbazi, Dar es Salaam na maeneo mengine ya mabondeni Dar. Nyumba za thamani zimejengwa kwenye bonde la Msimbazi na watu wanaotajwa kama wasomi na wajanja wa mjini.
 
Kijiji cha mbagala kizuiani...jaman Kuna kunguni mpaka maji ya visima ukichota unakuta kunguni walidondokeamo.
Kunguni wanatembea msafara barabarani kama siafu
JamiiForums-1531000277.jpg
 
Misitu ndio ukubwa ww nchi?
Mzee Baba kama hujatembea ila linchi likubwa japo naona unataka fananisha na Russia. Nchi kubwa sana hii na ina mapori Mengi sana. Mara ya Kwanza natoka Nyumbani Arusha naenda Katavi pitia Tabora ndio niliona linchi lilivyo kikubwa. Kuna kipindi nilitoka Kagera kwenda Kugoma via Nyakanazi. Sio kwa Misitu ile.
 
Ukifika siha na hai Barbara ya kwenda merarani hutatamani

Pia same na mwanga ni pa hovyo mno
Hayo maeneo ya kawaida sana, hakuna kipya kibaya au kitu cha ajabu. Jiografia yake ndio inaweza kukutisha lakini ukipakaribia utagundua pako poa.

Mahali penye barabara inayopitika majira yote na huduma zote muhimu za kijamii, sio mahali pa ajabu.

Kwa mfano, kwa Kilimanjaro, eneo kama wilaya ya Mwanga (maeneo ya huko milimani).
-Pana barabara ya lami kutoka tambarare mpaka juu kileleni mwa milima huko kwenye vijiji vya wapare (sijui Usangi, Ugweno?), na usafiri wa umma unaelezwa kuwepo wakati wote wa siku, kuanzia alfajiri mpaka mida ya usiku. Sijui serikali iliamua kuwapendelea? Maana hakuna shughuli yoyote ya maana ya uzalishaji kama kilimo nk.

-Tanesco wanasema mtandao wa umeme ulifika huko milimani tangu miaka ya 1980, na kwa sasa zaidi ya 90% ya kaya zao zina umeme.

-Hayo maeneo mbali ya kuwa na vituo vya afya vya kutosha, inaelezwa wana zahanati karibu kila kijiji, shule kila kijiji, maji ya bomba karibu kila kaya, vituo vya polisi, mahakama nk.
 
Mwakaleli- Tukuyu Mbeya. Aisee baridi lilinushinda pale Mwax sec.
Mwakaleli sec. Mbona pana barid la kawaida tu ,vipi ungepangwa makete si ungekufa wewe.

Me nimesoma hapo mwaka2009- 2011 niliinjoy Sana life la mwakaleli sec.

Matamba ,isange ,kandete vilikua viwanja vyangu sana.
Napamic Sana
 
Back
Top Bottom