Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Mpanda Katavi....mji wa hovyo sana ule
Historia ya mji wa Mpanda ina mizizi yake tangu mwaka 1934 kufuatia ugunduzi wa dhahabu uliofanywa na Mhandisi wa madini na Mjiolojia wa Kibelgiji aliyeitwa Jean Poussin. Awali eneo hilo lilikuwa mojawapo ya Wilaya za Mkoa wa Tabora hadi ilipofika mwaka 1975 ilipohamishiwa Mkoa wa Rukwa na baadaye Katavi mwaka 2012.

Jean Poussin alipata leseni ya uchimbaji baada ya kugundua akiba kubwa ya madini ya Zinki (Zinc) na Risasi (Lead) ambayo yalikuwa na umuhimu mkubwa sana kiuchumi katika kipindi hicho, alianzisha mgodi wa kuzama chini (underground mine). Pamoja na changamoto za Vita Kuu ya pili ya Dunia, Serikali ya wakati huo ilimuunga mkono na kumpatia ushirikiano mkubwa katika biashara yake hiyo, ikizingatiwa kwamba mgodi huo ulikuwa chanzo cha malighafi za vifaa vya kijeshi.

Mgodi wa Ururirwa (Ululilwa?) Mineral Ltd uliorodheshwa kwenye Soko la Hisa la London (London Stock Exchange Market) mwaka 1947 kama njia ya kuwezesha ufadhili wa mchango wake katika ujenzi wa miradi ya bomba la maji na reli iliyohudumia mgodi na mji kwa wakati huo. Ulazima wa kusafirisha makinikia ya madini kwenda bandari ya Dar es Salaam ulilazimu ujenzi wa reli iliyounganisha Reli ya Ujiji-Tabora.

Mbali na madini, eneo hilo lilivuta watu wengi kwa ajili ya kilimo cha mazao ya mpunga, mahindi na tumbaku yanayostawi sana eneo hilo na pia ufugaji wa mifugo hususan Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo na hata uvunaji wa mazao ya misitu zikiwemo mbao na asali.
 
Mkuu Tangeni hapo jirani na Mzumbe University? Hiyo labda itakuwa Bunduki au kule Juu kabisa ya Kijiji kinaitwa Nyandira..
Kabla ya Bunduki unapita Mlale Kisha unapanda ule Mlima mrefu kuipata Mgeta Kibaoni, Mgeta Kibaoni Kuna njia Moja inaenda Bunduki na nyingine inaenda Lolo mpaka Nyandira. Bunduki wanafunzi wa sekondari wanatoka mbali na majumbani Kuna Siku wanafunzi wanaenda robo ya Darasa.

Mgeta Kibaoni usiagize supu bila kuuliza Kuna supu ya nguruwe, Gari za Moro Town Kwenda Mgeta kulikuwa na Noah zimeandikwa Mama Mlezi na Toyota Dayna Hiace Double Diff zinaenda mpaka milimani Nyandira, seat ya karibu na dereva nauli ilikuwa inaongezeka elfu 1.
 
Bora hata mpanda, kuna mahali panaitwa MAJIMOTO aisee huko nilipoenda nilijiuliza qatu wamefuata nini, na wengi wao ni wasukuma kule...Ajabu ni kwamba they are making money ile hatari. Ni matajiri wa kutupwa kutokana na kilimo ufugaji na madini.
Majimoto iko wapi hio mkuu?
 
Kijiji Cha kenge,kata ya kiroka milima ya uluguru huko,mita 3000 kutoka chini,yaani huko unayaona mawingu tu,hakuna umeme, chakula ni ndizi tu
Watu wamekomaa vifua na mikono mpaka watoto kwa kupanda na kushusha mlima
Hatari sana nilishangaa mtu kushuka na mbao tatu begani mara kumi kwa siku bila kuchoka!
 
Karbu na chimala?
 
Niliendaga Kododo na Lukunguni tarafa ya Mgeta kata ya Mgeta. Huko sio Mchezo kwa milima ile. Ni kweli inakosa jibu watu walifuata nini huko Milimani.
Yani nilistaajabu maisha yao ya kila siku wanaendeshaje
Mana hata maduka yako huko bondeni ambako masaa 2 mnashuka
 
Mbinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…