Changalucha
JF-Expert Member
- Oct 19, 2011
- 508
- 593
Historia ya mji wa Mpanda ina mizizi yake tangu mwaka 1934 kufuatia ugunduzi wa dhahabu uliofanywa na Mhandisi wa madini na Mjiolojia wa Kibelgiji aliyeitwa Jean Poussin. Awali eneo hilo lilikuwa mojawapo ya Wilaya za Mkoa wa Tabora hadi ilipofika mwaka 1975 ilipohamishiwa Mkoa wa Rukwa na baadaye Katavi mwaka 2012.Mpanda Katavi....mji wa hovyo sana ule
Jean Poussin alipata leseni ya uchimbaji baada ya kugundua akiba kubwa ya madini ya Zinki (Zinc) na Risasi (Lead) ambayo yalikuwa na umuhimu mkubwa sana kiuchumi katika kipindi hicho, alianzisha mgodi wa kuzama chini (underground mine). Pamoja na changamoto za Vita Kuu ya pili ya Dunia, Serikali ya wakati huo ilimuunga mkono na kumpatia ushirikiano mkubwa katika biashara yake hiyo, ikizingatiwa kwamba mgodi huo ulikuwa chanzo cha malighafi za vifaa vya kijeshi.
Mgodi wa Ururirwa (Ululilwa?) Mineral Ltd uliorodheshwa kwenye Soko la Hisa la London (London Stock Exchange Market) mwaka 1947 kama njia ya kuwezesha ufadhili wa mchango wake katika ujenzi wa miradi ya bomba la maji na reli iliyohudumia mgodi na mji kwa wakati huo. Ulazima wa kusafirisha makinikia ya madini kwenda bandari ya Dar es Salaam ulilazimu ujenzi wa reli iliyounganisha Reli ya Ujiji-Tabora.
Mbali na madini, eneo hilo lilivuta watu wengi kwa ajili ya kilimo cha mazao ya mpunga, mahindi na tumbaku yanayostawi sana eneo hilo na pia ufugaji wa mifugo hususan Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo na hata uvunaji wa mazao ya misitu zikiwemo mbao na asali.