Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Singida ,Wilaya ya ikungi,kuna vijini kama mandimu,mkungua kihendo aise kule ni kukame maji ni shida ,umeme sijui utafika link huko,mitandao ya shida ,maji machafu kiukwel sijui wanaishi vipi lakini ni mazingira magumu
kuna sehemu nilipita kuna Secondary ya kiislamu sijui inaitwa IDISYA vijiji sikuvijua majina ila wilaya hio hio ya ikungi ..tulitokea singida mjini aisee palikua ni mbali kinoma mpaka watoto bado wanaogopa magari, maji ni meupe kama maziwa nayo ni kidogo mnoo
nikajiuliza ivi watu wanaishi huku kufanya nini jamani
 
Panafaa maji yanatoka mwanza umeme upo,network ipo ,hospital ipo na barabara ya kufika shy town unafika tu
ile barabara kuja kufika town unaumwa mgongo, usafiri wa shida , ukame , hamna matunda na mboga za majani ,hamna maduka ya maana
 
Kuna Kijiji nilienda mpaka unafika inabidi utumie aina zote za Usafiri kasoro Ndege na Treni.
 
ile barabara kuja kufika town unaumwa mgongo, usafiri wa shida , ukame , hamna matunda na mboga za majani ,hamna maduka ya maana
Maduka mpaka shy siku hiz wamefungua kule halmashauri πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Dodoma vijijini. huwa nafikiria sana, maji ni shida kupita kiasi, kilimo hakikubali, ufugaji sio wafugaji wa maana. wanakula nini? mbona kuna maeneo mengi tu mikoa mingine yapo wazi wangeenda wakalima wakapata chakula wakaishi vizuri tu?
 
Aisee! Ni makutupora... kijiji fulani kiko Dodoma mbele huko ndanindani kama unaelekea Singida kumzika marehemu BIBI yangu... alafu kwa vile kulivyo Wajomba zangu wakawa wananipa story wao walikuwa wanakuja likizo miaka ya "70/80" huko imagine kulikuwaje kama saiv panaonekana bado hovyo namna hii aisee! Nilichoka πŸ˜‚πŸ™ŒπŸΎ
 
Dodoma vijijini. huwa nafikiria sana, maji ni shida kupita kiasi, kilimo hakikubali, ufugaji sio wafugaji wa maana. wanakula nini? mbona kuna maeneo mengi tu mikoa mingine yapo wazi wangeenda wakalima wakapata chakula wakaishi vizuri tu?
Kuna jamii haijui kama kuna sehemu nyingine zaidi ya wanapoishi wao.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…