Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Singida ,Wilaya ya ikungi,kuna vijini kama mandimu,mkungua kihendo aise kule ni kukame maji ni shida ,umeme sijui utafika link huko,mitandao ya shida ,maji machafu kiukwel sijui wanaishi vipi lakini ni mazingira magumu
kuna sehemu nilipita kuna Secondary ya kiislamu sijui inaitwa IDISYA vijiji sikuvijua majina ila wilaya hio hio ya ikungi ..tulitokea singida mjini aisee palikua ni mbali kinoma mpaka watoto bado wanaogopa magari, maji ni meupe kama maziwa nayo ni kidogo mnoo
nikajiuliza ivi watu wanaishi huku kufanya nini jamani
 
Panafaa maji yanatoka mwanza umeme upo,network ipo ,hospital ipo na barabara ya kufika shy town unafika tu
ile barabara kuja kufika town unaumwa mgongo, usafiri wa shida , ukame , hamna matunda na mboga za majani ,hamna maduka ya maana
 
Kuna Kijiji nilienda mpaka unafika inabidi utumie aina zote za Usafiri kasoro Ndege na Treni.
 
ile barabara kuja kufika town unaumwa mgongo, usafiri wa shida , ukame , hamna matunda na mboga za majani ,hamna maduka ya maana
Maduka mpaka shy siku hiz wamefungua kule halmashauri 😂😂😂😂
 
Habari za muda huu wana JF,

Nchi yetu ni kubwa na Ina miji na vijiji vingi lakini Kuna baadhi ya maeneo unaweza ukahisi sio sehemu ya nchi yetu mpaka ukajiuliza maswali kuwa Hawa watu waishio hapa walivutiwa na Nini mpaka wakaweka makazi ya kudumu maeneo haya

Mfano, Mimi niliwahi kutembelea Kijiji cha Baranga kata ya Sirorisimba kupitia Kyagata. Nilistajabu na kujiuliza Hawa watu huku wanaishije?

Ukame ndio kwao, maji shida, Hali ya hewa mbovu, jua kali ndio kwao, vurugu Sasa ndio chimbuko lake. Siku moja tulikuwa na mechi ya kirafiki na timu ya Kijiji jirani ile tupo kwenye gari tukashangaa tunaanza kurushiwa mawe barabarani.

Kwa kuwa sisi tulikuwa wageni tuliogopa sana lakini wenyeji wakatuambia msiogope hao wote tutakutana kwenye mnada. Siku nyingine tulikuwa Mnadani Sirorisimba siku hiyo kulikuwa na mgogoro wa mpaka wa shamba kati ya ukoo na ukoo huku polisi wakiwa na mitutu ya bunduki lakini ilivyo ajabu watu wa kule nilishudia wakibebana na kuhamasishana wabebe mishale waende wakaanzishe vurugu.

Wewe ulipita wapi na ulistaajabu nini?
Dodoma vijijini. huwa nafikiria sana, maji ni shida kupita kiasi, kilimo hakikubali, ufugaji sio wafugaji wa maana. wanakula nini? mbona kuna maeneo mengi tu mikoa mingine yapo wazi wangeenda wakalima wakapata chakula wakaishi vizuri tu?
 
Aisee! Ni makutupora... kijiji fulani kiko Dodoma mbele huko ndanindani kama unaelekea Singida kumzika marehemu BIBI yangu... alafu kwa vile kulivyo Wajomba zangu wakawa wananipa story wao walikuwa wanakuja likizo miaka ya "70/80" huko imagine kulikuwaje kama saiv panaonekana bado hovyo namna hii aisee! Nilichoka 😂🙌🏾
 
Dodoma vijijini. huwa nafikiria sana, maji ni shida kupita kiasi, kilimo hakikubali, ufugaji sio wafugaji wa maana. wanakula nini? mbona kuna maeneo mengi tu mikoa mingine yapo wazi wangeenda wakalima wakapata chakula wakaishi vizuri tu?
Kuna jamii haijui kama kuna sehemu nyingine zaidi ya wanapoishi wao.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom