Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Mkoa wa Songwe..... ukiwa unamaliza kupanda mlima wa Senjele unataka kushoto kuna sehemu inaitwa Iyula.....huko kuna kijiji kinaitwa Idiwili.......yaani kule nimeshangaa watu wamefata nini kule........watu mpaka saa nne hakuna aliyeamka baridi kali....watu wanalala huku wameacha milango wazi ili kuku watoke pakikucha......mitaani kumezagaa nguruwe tu na vitoto vya nguruwe.....
 
kibondo kigoma yani, ilikua mwaka 2015 , kwanza kufika uko ni barrier za maana tulikutana nazo barabarani adi nikajiuliza ivi uku ni Tanzania au nchi nyingine.

kwanza kipindi icho uko kibondo ukienda kijiji kimoja ukitaka kwenda kingine ni hakuna njia ya shortcut ni lazima urudi barabara kuu ndio uanze moja, alafu kuna mito ina mamba, na nyumba kule ni za nyasi yaani unaambiwa ukiezeka bati tu umekwishaaaaa ni wanakuloga
 
Wewe unisurika kuchomwa moto na gari lenu. Kimsingi wanawaona kama wanyonya damu za watu
 
Ni wapi huko, hao ndio waandamanaji wanaotakiwa Tz.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Dah umenikumbusha mbali, tanganyika masagati, iduhi ndembo na utengule.
 
Kuna sehemu Mkoa wa mbeya inaitwa Lupa tingatinga then unaingia ndani ndani huko kunaitwa Nkunungu aisee nliona watoto wa shule ya msingi shati Lina rangi ya udongo hata ufulie jiq haliwezi takata! Umasikini ni mkubwa sana vijijini, Bado watu hutumia mitishamba kwa kiasi kikubwa! Nlikuwa nna project ya research kule sasa pencils nlikuwa nazo kwenye vibox ikabidi nizikatekate nigawe kwa watoto karibia darasa la pili wote walikuwa hawana mtoto anakipenseli kama ukucha! Kila nikikumbuka huwa nawaza wale watu ni lini watakuja kuondokana na Hali ile
 
Unawawaza halafu wao wanaona kawaida
 
Mimi nilifika sehemu moja panaitwa salawe shinyanga v/jijini kuna mnada mkubwa wa ng'ombe jumamos siku moja ulitokea upepo mkali kuna upepo flan huwa unakuja kama mnara mrefu huwa unazunguka kwa kujinyonga kama kamba unasepeed san huwa unatumiwa na wachawi ule upepo ulikufika ulianza kuondoka na vitu kam pesa za matajiri zilizokuwa mkononi na mifugo kupotea tu maana lazima ufumbe macho vumbi kali mno cha ajabu ulienda kupita kwenye gari la tajiri mmoja maarufu mnunuzi wa ng'ombe ukasepa na jacket lilikuwa ndani ya gari na pesa nyingi sana tuliishia kuliona juu tu linazid kupaa na hatukuona liliposhukia huku upepo unazid kusepa,, hiyo sehemu kuna uchawi balaa.
 
God must be crazy kumbe bado inaishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…