Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Mkuu tusaidie jina la kijiji hii ni adventure aisee, nimecheka sana
Ni kati ya Turiani na korogwe kuna boda pori kwa pori ukitokea turiani.
Bus liko moja tu linapita kwa wiki mara moja,so siku zingine ni baiskeli tu.
Kuna mahali unakunja kushoto unapanda milimani huko ndio unakuta watu wanaishi kabisa bila matatizo.
 
Mimi nimekulia vijijini huko dodoma wilaya ya bahi. Kuna siku nilipita ikabidi nisimame kwanza nipaangalie maana hata sielewi niliwezaje kuishi maeneo kama yale. Maji ya shida, mnachota kwenye visima, unafanya kumsogeza chura ndo uchote maji. mtandao wa simu ni mpaka uende kwenye mti mmoja hivi upo kwenye uwanja wa mpira. gari la kwenda mjini ni moja, na lenyewe linapita vijiji kama vitano, mpaka lifike kwenu limeshajaa vya kutosha.
 
Mkoa wa Songwe..... ukiwa unamaliza kupanda mlima wa Senjele unataka kushoto kuna sehemu inaitwa Iyula.....huko kuna kijiji kinaitwa Idiwili.......yaani kule nimeshangaa watu wamefata nini kule........watu mpaka saa nne hakuna aliyeamka baridi kali....watu wanalala huku wameacha milango wazi ili kuku watoke pakikucha......mitaani kumezagaa nguruwe tu na vitoto vya nguruwe.....
Duuuuuh noma sana, inamaana ustaarabu F
 
Mwanza miambani wananoishi watia huruma sana japo wao wanaona wamepata viwanja city centre.

Huwa najiuliza walishindwaje kuweka makazi Usagara, Misungwi na Magu badala ya kubanana kwenye mawe kama mijusi ambako kupanda ni shida na inaweza kuchukulia lisaa kwenda sehemu unayoiona kwa mbele tu hapo.

View attachment 2378247
Mvua zikinyesha aliye juu zaidi anafungulia choo chake ili kuondoa kinyesi. Sasa fikiria adha wanayoipata hao waliopo chini zaidi.
 
Mwanza miambani wananoishi watia huruma sana japo wao wanaona wamepata viwanja city centre.

Huwa najiuliza walishindwaje kuweka makazi Usagara, Misungwi na Magu badala ya kubanana kwenye mawe kama mijusi ambako kupanda ni shida na inaweza kuchukulia lisaa kwenda sehemu unayoiona kwa mbele tu hapo.

View attachment 2378247
Hapa igogo au Mabatini ama Nyamazobe MWANZA ji
Ilturot Lorkereyan- kijiji kipo Ngorongoro
 
Hivi tanesco inawapelekea hawa jamaa umeme? Sijaona nguzo? Wanaishije?
Nguzo zipo we pimbi mpaka maji. Nimezaliwa huko nimekulia huko. Nguzo zimepanda mpaka mlimani na mabomba ya maji pia.

Na njia za kupanda zipo nzur tu labda haujawai fika umeona kwenye Tv
 
Back
Top Bottom