Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Kijiji cha MKOO wilayani MASASI
 
Ni kama ipo mpakan na igoma...mfno ni hill front ambayo ipo njia ya kuelekea kishiri..napo watu wamejenga ila c kulinganisha na mabatin
Sawa. Ila mwanza sehemu kubwa ni milima na mapango. Ni Mungu tu anawalinda wanaMwanza walio wengi. Yale mawe ukiyaangalia yalivyokaa ndio utajua kuna nguvu kubwa inaulinnda ulimwengu na mabaya
 
Lokichogio ni kimji kidogo kilichopo kaskazini magharibi mwa Kenya. Niliwahi kukwama pale kwa siku moja, sikuamini kuwa kuna sehemu katika Dunia hii watu wanaweza kuishi kama wanyama.
Mazingira ya kimji kile Hali ya hewa ya joto na ukame wa jangwa, umbali kutoka hapo hadi Rodwar au Kakuma,... miji inayotoa huduma ya kila bidhaa inayohitajika kwa mahitaji ya binadamu, inafanywa kuwa ngumu kwa kukosa miundombinu ya barabara!.... Sijui kama waliisha fanya maboresho, kama bado kule ndio mwisho Dunia.
 
Kijiji cha Kitapi, kipo wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani. Kipindi nimehamishiwa kikazi nimekuta maji ni kuchota visima vifupi, barabara imefunikwa na manyasi, hakuna mtandao wa simu hadi upande kwenye miti, nyumba zipo mbalimbali na zipo msitu, huduma ya soko ni kuanzia saa kumi Jioni hadi saa kumi na mbili jioni mchana watu wapo shamba, giza linaanza saa kumi na moja jioni kwa sababu ya msitu mnene, hakuna bodaboda zaidi ya zinazokuja na kutoka, mvua ikinyesha hakuna safari tena sababu ya utelezi na matope, husikii muungurumo wa gari kwa sababu gari pekee ni wakati wa mitihani ya darasa la saba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…