Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Habari za muda huu wanajf.

Nchi yetu ni kubwa na Ina miji na vijiji vingi lakini Kuna baadhi ya maeneo unaweza ukahisi sio sehemu ya nchi yetu mpaka ukajiuliza maswali kuwa Hawa watu waishio hapa walivutiwa na Nini mpaka wakaweka makazi ya kudumu maeneo haya

Mfano, Mimi niliwahi kutembelea Kijiji Cha Baranga kata ya sirorisimba kupitia Kyagata. Nilistajabu na kujiuliza Hawa watu huku wanaishije?

Ukame ndo kwao, maji shida, Hali ya hewa mbovu , jua kali ndo kwao, vurugu Sasa ndo chimbuko lake. Siku moja tulikuwa na mechi ya kirafikina timu ya Kijiji jirani ile tupo kwenye gari tukashangaa tunaanza kurushiwa mawe barabarani.

Kwa kuwa sisi tulikuwa wageni tuliogopa Sana lakini wenyeji wakatuambia msiogope hao wote tutakutana kwenye mnada. Siku nyingine tulikuwa Mnadani Sirorisimba siku hiyo kulikuwa namgogoro wa mpaka wa shamba Kati ya ukoo na uko huku polisi wakiwa na mitutu ya bunduki lakini ilivyo ajabu watu wa kule nilishudia wakibebana na kuhamasishana wabebe mishale waende wakaanzishe vurugu.

Wewe ulipita wapi na ulistaajabu Nini?
Kijiji cha MKOO wilayani MASASI
 
Ni kama ipo mpakan na igoma...mfno ni hill front ambayo ipo njia ya kuelekea kishiri..napo watu wamejenga ila c kulinganisha na mabatin
Sawa. Ila mwanza sehemu kubwa ni milima na mapango. Ni Mungu tu anawalinda wanaMwanza walio wengi. Yale mawe ukiyaangalia yalivyokaa ndio utajua kuna nguvu kubwa inaulinnda ulimwengu na mabaya
 
Lokichogio ni kimji kidogo kilichopo kaskazini magharibi mwa Kenya. Niliwahi kukwama pale kwa siku moja, sikuamini kuwa kuna sehemu katika Dunia hii watu wanaweza kuishi kama wanyama.
Mazingira ya kimji kile Hali ya hewa ya joto na ukame wa jangwa, umbali kutoka hapo hadi Rodwar au Kakuma,... miji inayotoa huduma ya kila bidhaa inayohitajika kwa mahitaji ya binadamu, inafanywa kuwa ngumu kwa kukosa miundombinu ya barabara!.... Sijui kama waliisha fanya maboresho, kama bado kule ndio mwisho Dunia.
 
Kijiji cha Kitapi, kipo wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani. Kipindi nimehamishiwa kikazi nimekuta maji ni kuchota visima vifupi, barabara imefunikwa na manyasi, hakuna mtandao wa simu hadi upande kwenye miti, nyumba zipo mbalimbali na zipo msitu, huduma ya soko ni kuanzia saa kumi Jioni hadi saa kumi na mbili jioni mchana watu wapo shamba, giza linaanza saa kumi na moja jioni kwa sababu ya msitu mnene, hakuna bodaboda zaidi ya zinazokuja na kutoka, mvua ikinyesha hakuna safari tena sababu ya utelezi na matope, husikii muungurumo wa gari kwa sababu gari pekee ni wakati wa mitihani ya darasa la saba.
 
Back
Top Bottom