Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Kwa kifupi uko ni jangwa sahii
Kumbe kijijini nilipokulia pakishua hapatajwa, Arusha..Miaka nakua kilikua poa ila tabia nchi, kwa sasa jua na mvua nadra, vumbi sana.

Vijiji kuzunguka mirerani, Makiba, Valeska,Lositeti, Mbuguni,Migungani,Shambarai...ma hommies.
 
Kwa kifupi uko ni jangwa sahii
Kuna sehemu inaitwa sukro, ipo mkoa wa manyara kutoka arusha unafata bara bara ya kuelekea kiteto, ukifika kijiji cha terrat unakunjia maporini huko, wacha kabisa, kuna kijiji kinaitwa narakauo, ukifika utajiuliza binadamu alifata nini huku, ila kuna mchaga amekita biashara ya maana, Ana duka la maana, yeye ndiye bank ya wamasai, yaani huduma zote muhimu wamasai wanapaita hapo, nilikutana na nyoka aina ya kifutu akiingia kwenye kanyumba flani kadogo, nika ita ili kama kuna mtu ndani nimweleze akae macho ila Hakuna aliyeitika, nilipo enda mbele kama mita 50 nikakutana na mmasai akielea uelekeo kilipo kile kibanda, nikamwuliza kama yeye ndiye anayeishi kwenye kile kibanda akasema ndiyo, nikamtaarifu kuwa nimeona joka kubwa likiingia humo kibandani hivyo awe makini, akacheka na kuniuliza "sasa nyoka ina shida gani? Nikamwambia ni kifutu mkubwa kabisa mzee, akasema tena huyo ndio hana shida kabisa! Nika achana nae ila kule hapana. Sehemu nyingine ilinishangaza ni same, gonja mahore kuna kijiji kioo kwenye kilele cha mlima, kinaitwa Mtii, ukifika chini ya mlima ili uanze kupanda kuelekea Huko kijijini kwa piki Piki ni tsh 30000 kupanda na 20 000 kusuka, picha hii hapo chini
IMG_00001221.jpg
IMG_00001224.jpg
IMG_00001231.jpg
IMG_00001222.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Experience nzuri mkuu

Hiyo alfu thelathini wanapata wateja?
Kuna sehemu inaitwa sukro, ipo mkoa wa manyara kutoka arusha unafata bara bara ya kuelekea kiteto, ukifika kijiji cha terrat unakunjia maporini huko, wacha kabisa, kuna kijiji kinaitwa narakauo, ukifika utajiuliza binadamu alifata nini huku, ila kuna mchaga amekita biashara ya maana, Ana duka la maana, yeye ndiye bank ya wamasai, yaani huduma zote muhimu wamasai wanapaita hapo, nilikutana na nyoka aina ya kifutu akiingia kwenye kanyumba flani kadogo, nika ita ili kama kuna mtu ndani nimweleze akae macho ila Hakuna aliyeitika, nilipo enda mbele kama mita 50 nikakutana na mmasai akielea uelekeo kilipo kile kibanda, nikamwuliza kama yeye ndiye anayeishi kwenye kile kibanda akasema ndiyo, nikamtaarifu kuwa nimeona joka kubwa likiingia humo kibandani hivyo awe makini, akacheka na kuniuliza "sasa nyoka ina shida gani? Nikamwambia ni kifutu mkubwa kabisa mzee, akasema tena huyo ndio hana shida kabisa! Nika achana nae ila kule hapana. Sehemu nyingine ilinishangaza ni same, gonja mahore kuna kijiji kioo kwenye kilele cha mlima, kinaitwa Mtii, ukifika chini ya mlima ili uanze kupanda kuelekea Huko kijijini kwa piki Piki ni tsh 30000 kupanda na 20 000 kusuka, picha hii hapo chiniView attachment 2382645View attachment 2382646View attachment 2382647View attachment 2382648

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mkoa wa Mara wilaya ya Butiama
Si afadhali hapo. Mimi miaka hiyo hiyo sehemu ikiwa inaitwa Musoma vijijini, wakati huo yapo mabasi yaitwa yo Ngoreme bus aka Mwanamara yakiendeshwa na akina Masyane. Wakati wa masika mwisho wa basi ilikuwa hapo Sirorisimba, tulikuwa tunakanyaga kwa miguu kuelekea huko Kenyana, Masinki na Kemugongo kwa muda ya masaa 12. Tulikuwa tuna lala njiani tunalazimika kuomba pa kulala njiani. Watu wa kule miaka hiyo walikuwa wakalimu sana. Maji ya kunywa toka mto Somoche na Nyaruherere yalikuwa machafu sana na tope hasa kiangazi mnago mbania na wanyama poli. Watu wengi walikuwa wana uwawa na nyati. Acha kabisa life la Ngoreme enzi hizo. Hakuna hospital, hakuna Sekondari hata moja shule za msingi hazikuzidi 5 na umbali kati ya shule na shule kwenye km 30 na kuendelea.
 
Kwa hiyo miaka ni agemate wangu, advance nimemaliza 2011 pia,Minaki Sec, pale ilikua joto tu na maji yenye fangasi sijui, pumbu zinawasha mpaka unataka uzitoe.hahah
Hiyo kitu Mkuu niilikuta Galanos tulikuwa tunaita erosion, tulikuwa tunatumia kidawa flani cha chupa ya kijani,kende utatamani uzinyofoe.
 
Nilicho furahi ni kwamba wasukuma humu tumetajwa tuko sehem mbali mbali tunapambana ila kila siku watu wanatutania sisi ni wajinga washamba lakini hao hao ndo wamesambaa kutafuta fulsa tanzania nzima [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuna Kijiji jina Dotina, manyara huko, aisee kile Kijiji wiki niliyokaa niliona kama miaka 5!! Dotina, Endamasaki, wenyeji wa kule heshima kwenu!!
 
Sawa. Ila mwanza sehemu kubwa ni milima na mapango. Ni Mungu tu anawalinda wanaMwanza walio wengi. Yale mawe ukiyaangalia yalivyokaa ndio utajua kuna nguvu kubwa inaulinnda ulimwengu na mabaya
Tetemeko la Ritcher Scale ya 7 likipita pale lazima tuzike zaidi ya 10000
 
Back
Top Bottom