Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ilunde Wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi. Kijiji kipo Porini, Kilomita 70 toka makao makuu ya Wilaya ya Mlele. Hakuna network wala nini na ni Porini hasa. Sijui walifuata nini kule.
Wengi ni Wasukuma wahamiaji na Wakonongo.
 
Kuna Wavidunda wanaishi juu ya milima pembeni ya Bwawa la Kidatu. Tulikwenda study tour unapita chuo cha Maafisa wa Polisi. Wao wanaahuka toka milimani ni hatari. Naambiwa Wana Mila Yao ya kubudu Moto lazima wawashe Pori mara moja Kila mwaka. Wale watu mpaka Serikali imeingia nao mkataba wa kuwasafirisha kwenda Kilombero kufuata mahitaji. Magari ya TANESCO yanawapeleka na kuwarudisha bure Kila alhamisi.
 
Kuna kijiji kipo Iringa ndanindani[emoji16][emoji16]

Asubuh nikaletewa maji ya kuoga nikaoga fresh sasa ilivyofika jioni nikasema ngoja niende na huyo dada nikachote mwenyew [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hicho kisima unachota maji pamoja na chura, unafanya kuwatoa chura kwenye ndoo ili upate maji aiseeh

Ikifika mida ya saa 12 jioni wanakijiji wote wanaenda kilabuni inshort kijiji kizima wanamwagilia moyo[emoji23]

Wanamwagilia moyo [emoji28]
 
Watu wanaokaa tukuyu,mwakaleli,katumba kule mbeya, asee wana moyo sana, ni kama watu wanaoishi Dar alafu kipato ni dollar moja.
Huko unakotaja ni mjini wewe! Kuna mashule,zahanati na huduma zote za kijamii maji umeme etc!! Cha ajabu ni nn hasa?
 
Oyster Bay mkoa wa Dar es salaam huwa najiuliza hv Hawa wanoishi huku vijora, baikoko, chura, mihogo vitumbua nk. Wanaviona saa ngapi?
 
Hao Jamaa noma!

Way back walitumia NGUVU ZA GIZA kuzuia Project ya KIDATU HEP!

SERIKALI (TANeSCO) ikanyoosha Mikono Juu kwa kuingia nao huo Mkataba wa kuwapeleka MNADANI kila Alhamis na kuwarudisha!

Kuna Wavidunda wanaishi juu ya milima pembeni ya Bwawa la Kidatu. Tulikwenda study tour unapita chuo cha Maafisa wa Polisi. Wao wanaahuka toka milimani ni hatari. Naambiwa Wana Mila Yao ya kubudu Moto lazima wawashe Pori mara moja Kila mwaka. Wale watu mpaka Serikali imeingia nao mkataba wa kuwasafirisha kwenda Kilombero kufuata mahitaji. Magari ya TANESCO yanawapeleka na kuwarudisha bure Kila alhamisi.
 
Nilipanda mlima uluguru nikakuta waluguru huko juu Tena wanavijiji vyao Hali ya hewa ilikuwa nzuri ila huduma za kijamii Hadi uteremke mlima, binafsi nilishuka miguu inatetemeka na maumivu makali mno. Mpaka Leo nawashangaa watu Kule wanavyoishi
Ilonga je?
 
Mwanza miambani wananoishi watia huruma sana japo wao wanaona wamepata viwanja city centre.

Huwa najiuliza walishindwaje kuweka makazi Usagara, Misungwi na Magu badala ya kubanana kwenye mawe kama mijusi ambako kupanda ni shida na inaweza kuchukulia lisaa kwenda sehemu unayoiona kwa mbele tu hapo.

View attachment 2378247
Huku kila mtu yupo fiti. 😂
 
Back
Top Bottom