Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Masagati

MASAGATI


MASAGATI.


AISEEEH NIKIRUDI KULE MNIITE MBWA NIMEKAA PALEEEEEEEEE

Unaweza hisi upo kuzimu...

Hakuna huduma muhimu kwa binadamu,watu wanakula nyama yoyote ilimradi inatoka damu,nyani,kima,ngedere, twende.....

Ngono inafanyika kama mazoezi ya viungo tu,inauzwa kama njugu,mpaka najiuliza kweli kuna UKIMWI duniani!
Hakuna barabara wala umeme wala maji salama...

Mvua ikinyesha hakuna kutoka wala kuingia
Sasa unasema masagati .....mbona hujafika kule Tanganyika mkuu?
Hii nchi waigawanye tu aisee tuna linchi likubwa mnoo.
Hyo Masagati iskieni hivyo hivyo hakuna kanisa wala msikiti😂😂😂
 
Sasa unasema masagati .....mbona hujafika kule Tanganyika mkuu?
Hii nchi waigawanye tu aisee tuna linchi likubwa mnoo.
Hyo Masagati iskieni hivyo hivyo hakuna kanisa wala msikiti😂😂😂
Mkoa gani inapopatikana hiyo masagati na Tanganyika?
 
Mtwara hakuna vijiji vibaya sana, ni moja ya mikoa ambayo vijiji vyake unakutana na NYUMBA nyingi kabisa, wanakuwa na Soko, maduka yanakuwepo. Kule 90% ya vijiji magari yanafika, nyumba nyingi ni zile za udongo lkn zenye bati na kubwa sio kama vijiji vya kule DODOMA Jmn hadi unajiuliza wanalalaje mule?? Sijui ilikuwaje lkn Mtwara kwenye vijiji wako far better than 80% ya mikoa ya TZ.

Kwangu mimi mikoa ambayo ni ya kijinga zaidi ni DODOMA, KIGOMA, MANYARA, KATAVI, SHINYANGA, MARA na SINGIDA bila kusahau MOROGORO, hiyo mikoa ina vijiji vya ajabu sana sana sana sana.

Hivi unajua 80% ya vijiji vya mkoa wa Mara vina umeme? Nimepita pita vijiji vya huko sio vya hovyo kivile! Aisee kuna mikoa ina vijiji vya ajabu acha kabisa
 
Sitasahau 2018 nimepelekwa Longido masaini huko Kijiji kinaitwa Lorienito kikazi, siku 45 nilizokaa huko niliona kama ni Miaka 10

Hamna Barbara na hawataki barabara Kwa maelezo kwamba vijana wao watakimbilia mjini, ni wao na mifugo mifuga na wao, nyumba za tofali zilizoko huko ni 2 tu shule ya msingi na zahanati

Kutoka huko mpaka sehemu ya kuipata usafiri wa kukufikisha Longido mjini ni nauli ya sh 30,000 bodaboda

Hakuna network hakuna hata radio station inayoshika huko yaani kule hata Kwa mtutu siendi tena
 
Niliwahi kufika kule mwaka 2002 mpaka mimea inaungua kutokana na baridi nilifika Kandete, Kyejo mpaka Isange kupitia kiwanda cha majani ya chai Katumba au Tandale Tukuyu Mjini.
Ha ha haaa.....

Mkuu umenikumbusha mbali Sana. Nilikuwa Kule Mwaka huu 2022.

Usafiri ni Noah au Bodaboda au Malori yanayopeleka Mizigo.

Kuna siku nataka kuja Town halafu usafiri ni shida kinoma. Ilinidi nipande Canter iliyobeba Makreti tupu ya Bia.

Ile nafika pale Njia panda ya kwenda Tukuyu na Kushuka suruali yote inanuka Bia maana nilikalia zile Kreti tupu za Bia.
 
Habari za muda huu wana JF,

Nchi yetu ni kubwa na Ina miji na vijiji vingi lakini Kuna baadhi ya maeneo unaweza ukahisi sio sehemu ya nchi yetu mpaka ukajiuliza maswali kuwa Hawa watu waishio hapa walivutiwa na Nini mpaka wakaweka makazi ya kudumu maeneo haya

Mfano, Mimi niliwahi kutembelea Kijiji cha Baranga kata ya Sirorisimba kupitia Kyagata. Nilistajabu na kujiuliza Hawa watu huku wanaishije?

Ukame ndio kwao, maji shida, Hali ya hewa mbovu, jua kali ndio kwao, vurugu Sasa ndio chimbuko lake. Siku moja tulikuwa na mechi ya kirafiki na timu ya Kijiji jirani ile tupo kwenye gari tukashangaa tunaanza kurushiwa mawe barabarani.

Kwa kuwa sisi tulikuwa wageni tuliogopa sana lakini wenyeji wakatuambia msiogope hao wote tutakutana kwenye mnada. Siku nyingine tulikuwa Mnadani Sirorisimba siku hiyo kulikuwa na mgogoro wa mpaka wa shamba kati ya ukoo na ukoo huku polisi wakiwa na mitutu ya bunduki lakini ilivyo ajabu watu wa kule nilishudia wakibebana na kuhamasishana wabebe mishale waende wakaanzishe vurugu.

Wewe ulipita wapi na ulistaajabu nini?
Ukwama makete
 
Singida ,Wilaya ya ikungi,kuna vijini kama mandimu,mkungua kihendo aise kule ni kukame maji ni shida ,umeme sijui utafika link huko,mitandao ya shida ,maji machafu kiukwel sijui wanaishi vipi lakini ni mazingira magumu
 
Shekilango kuna kisoko cha ajabu ajabu kinatoa harufu mbaya utafikiri upo mochuari umeme umekatika week 3 halafu ndugu wa kuchukua miili wamegoma.

Hivi nyie watu Dar mnaishi vipi !.Ukipita mabibo kuelekea Kigogo mazingira machafu harufu mbaya halafu unamkuta mtu ana kunywa chai mazingira yale yuko pouwa kabisa.
 
Nandete, Kipatimu,Kilwa. Lindi.
Kuiyona lami Ni saa 4. Milima na mabonde. Maji huduma za kijamii maduka tu shida mwendo wa Sola ... Cha ajabu nauli 13000/=Mwendo was saa 6 kufika DAR-ES-SALAAM...
 
Baranga kata ya Sirorisimba hiki kijiji kiko wilaya ipi na mkoa upi?
 
Back
Top Bottom