Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Mimi huwa nikipita na gari barabarani maeneo ya kondoa yalivyo makavu na pia nikiwangalia wakazi wa maeneo yale wanavyoishi maisha ya mateso huwa najisikia vibaya sana....
Mbona naona wako bien tuu...ushawahi pita pita maeneno ya kuanzia babati kama unaenda Arusha wale watu ndo wa kuwaonea huruma..ndo maana wakabuni nguo ndefu za mashuka maana ule upepo na vigauni vyetu tungejikuta tupo wazi...au shati linaweza jaa upepo ukapaa..yale mashuka ni wind proof...
 
Kuna kijiji nilifika kutafuta ndizi biashara miaka hiyo.
Aisee ni mbali katikati ya turiani na korogwe njia ya pori kwa pori.hamna magari ni kwenda kwa baskeli tu alafu unachepuka kwenda mlimani huko nikakuta kakijiji aisee vijumba kichekesho,alafu wana mfalme wao yaani chakula wanakula woote familia zoote pale kwa mfalme.
Kila kaya inaleta ilichopika pale.
Nilikula mboga mboga mpk nilikoma.
Siku nikalogwa nikanunua kuku 2 wameniuzia wao wenyewe kaya 1 niliokuwa nakaa nikawapa wapike nikajua ntakula japo nusu aaah wakapeleka kwa mfalme kule tunakokula nikaambulia kibawa,yaani mkulu ana nyofoa kinyama anampa mtu kushoto au kulia kwake kinatumwa mpk kikufikie kila mtu kakishika
Nilikasirika sana.
Dah qqmkk
 
Habari za muda huu wana JF,

Nchi yetu ni kubwa na Ina miji na vijiji vingi lakini Kuna baadhi ya maeneo unaweza ukahisi sio sehemu ya nchi yetu mpaka ukajiuliza maswali kuwa Hawa watu waishio hapa walivutiwa na Nini mpaka wakaweka makazi ya kudumu maeneo haya.

Mfano, Mimi niliwahi kutembelea Kijiji cha Baranga kata ya Sirorisimba kupitia Kyagata. Nilistajabu na kujiuliza Hawa watu huku wanaishije?

Ukame ndio kwao, maji shida, Hali ya hewa mbovu, jua kali ndio kwao, vurugu Sasa ndio chimbuko lake. Siku moja tulikuwa na mechi ya kirafiki na timu ya Kijiji jirani ile tupo kwenye gari tukashangaa tunaanza kurushiwa mawe barabarani.

Kwa kuwa sisi tulikuwa wageni tuliogopa sana lakini wenyeji wakatuambia msiogope hao wote tutakutana kwenye mnada. Siku nyingine tulikuwa Mnadani Sirorisimba siku hiyo kulikuwa na mgogoro wa mpaka wa shamba kati ya ukoo na ukoo huku polisi wakiwa na mitutu ya bunduki lakini ilivyo ajabu watu wa kule nilishudia wakibebana na kuhamasishana wabebe mishale waende wakaanzishe vurugu.

Wewe ulipita wapi na ulistaajabu nini?
Sio Kijiji Ungesema Hii Nchi Ya Tanzania Watu Wanakalia Nini haileweki.
 
Jamani mkoa wa simiyu hukoooo ndanindani nyumba zilivyojipanga, mchawi mchawi mchawi mganga mganga mganga mganga mfuga misukule mfuga misukule mwenye roho mtu mwema roho mbaya roho mbaya Hadi nikasema hivi shetani hakai kule kweli? Hapa ukienda upande wa kaskazini magharibi inaungia bariadi ndo unakutana na Kijiji funga kazi kinaitwa Gamboshi hiyo ndo mitaa ya JOKA LA MAKENGEZA ndo maana Kuna mtu akauliza mbona hii njemba Kila kashfa ya upigaji lazima alambe Kuna mtu akasema ooh yule ni mwanasheria nguli from havard! Hiyo siyo sababu kwani wakubwa wanajua ukipigwa juju unamfata JOKA anakupeleka huko Gamboga unabinuliwa kichuguu unachanjwa Kisha sangoma anakuweka dole lile kubwa bila kujali cheo wa protoko maana vyote unaviacha dsm kama siyo dom sasa mtu kama huyu Kuna wa kumgusa kweli?
Natamani uandike kitabu Cha simuli mkuu
 
Hatari Sana jamii
Nimezunguka sehemu kibao watu wanaishi sehemu ambazo ukifika
Unajiuliza walifikaje huko na kuanza maisha milimani
Wengine ukiongea nao wanakuambia enzi za nguvu kazi
Watu ndiyo walipoanza kukimbiaa

Ova
Jamii imetoka mbali
 
Back
Top Bottom