Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uko sahihiVijiji vya Vunta na Kidunda, Hedaru, wilaya ya Same.
Ni vijiji vilivyo milimani - ktk Safu ya milima ya Usambara.
Ukitokea Mombo, kabla ya kufika Hedaru, unakata kulia na kuanza songombingo la kupanda mlima kuelekea vijiji hivi.
Issue hapa ni barabara ya vumbi yenye slope kubwa ajabu! Dereva akifanya kosa kidogo tu, mmekwisha kwani gari litaserereka bondeni takribani mita 600 - 800 hadi litakapogonga mwamba na kusimama! Bila gari imara lenye 4-W, huwezi kwenda kule.
Wakati wa kurudi toka Vunta, nilimuuliza mwenyeji wangu kuwa kwanini hawa Wapare waliamua kwenda kuishi sehemu hatarishi kama zile? Aliniambia kuwa, Wapare walikimbilia kwenda kule kwa ajili ya maficho kutokana na vita kati yao na maadui zao pamoja na maasidi wao - Wachagga. Ilikuwa zamani sana kabla ya ujio wa Wakoloni.
Baadaye waliweka makazi mpaka leo.
Aiseeee hatarrrMilo ipo Chalinze hapo karbu na ruvu unaingia kulia km20, kulikuwa na kambi ya wapigania uhuru wa South Africa miaka ya 80 adi 90 kwa sasa imegeuzwa kuwa zahanati ya kijiji.
Sio mbali sana ila barabara ni mbovu sana na mvua ikinyesha hakupitiki, kilichonishangaza kipind nafany mradi flani wa afya ni maisha ya kule kuna kiwango kikubwa cha maambukizi ya HIV, unaweza pima watu 10 ukakuta 6 wanao teyari au familia nzima wameathirika.
Toka Iringa mjini kituo cha mafuta unakikuta Migoli mbele ya Nyang'oroHadi Nyang'oro, kote hakuna vituo. Nimepazungumzia huko kwa sababu nililazimika kukaa hapo kwa wiki tatu kikazi, nami si shabiki wa videbe.
Kuna ukame balaa ila Watu wake wanakomaa kufuga kuliko kulima, wakiuhemea ule mto ambao kiangazi hali ni tete. Ila watu ni washkaji sana.
Ova
Bukundi, sina hakika kama nitakuwa nimepatia, makao, kwingine nishasahau mkuu.Kijiji Gani mkuu?
Bukundi na Makao kwa Sasa Kuna uafadhaliBukundi, sina hakika kama nitakuwa nimepatia, makao, kwingine nishasahau mkuu.
Nilienda mwaka juzi huko Bukundi aisee hakuna rangi sijaona. Kuna vumbi hata kama una v8 lazima likufikie. Maisha magumu sana kuna sehemu nyingine huko sijui karibu na ziwa magadi daaah.!!!Bukundi na Makao kwa Sasa Kuna uafadhali
Nina route ya huko mwaka huu pia, Busega, Bariadi, Meatu na Maswa.Bukundi na Makao kwa Sasa Kuna uafadhali
Karibu mkuuNina route ya huko mwaka huu pia, Busega, Bariadi, Meatu na Maswa.
Haina shida mkuu.Karibu mkuu
Ukifika meatu nshitue
Hayo maeneo yalivyokaa ni kiana aina tu.Kuna kijiji kinaitwa Ngapa katikati ya Mikumi na Iyovi, pale sijawahi kupaelewa kabisa
Soda ilikuwa inaagizwa masasi kwa Oda maalum.mkitaka nyama ya mbuzi mnamnunua angali mzima ndipo achinjwe.Yaani ajitokeze Kila mtu kununua kiungo kimoja.ukiwa na mfuko wa dementia wa deal unauuza kwa wiki mbili.Kukoje huko mkuu
Pale wenyewe huwatoi mtandao shida, watoto wanasoma mbali hatari.Kuna kijiji kinaitwa Ngapa katikati ya Mikumi na Iyovi, pale sijawahi kupaelewa kabisa
Duh haya mambo yako kweli ndugu?imenishtua sana hiiJamani mkoa wa simiyu hukoooo ndanindani nyumba zilivyojipanga, mchawi mchawi mchawi mganga mganga mganga mganga mfuga misukule mfuga misukule mwenye roho mtu mwema roho mbaya roho mbaya Hadi nikasema hivi shetani hakai kule kweli? Hapa ukienda upande wa kaskazini magharibi inaungia bariadi ndo unakutana na Kijiji funga kazi kinaitwa Gamboshi hiyo ndo mitaa ya JOKA LA MAKENGEZA ndo maana Kuna mtu akauliza mbona hii njemba Kila kashfa ya upigaji lazima alambe Kuna mtu akasema ooh yule ni mwanasheria nguli from havard! Hiyo siyo sababu kwani wakubwa wanajua ukipigwa juju unamfata JOKA anakupeleka huko Gamboga unabinuliwa kichuguu unachanjwa Kisha sangoma anakuweka dole lile kubwa bila kujali cheo wa protoko maana vyote unaviacha dsm kama siyo dom sasa mtu kama huyu Kuna wa kumgusa kweli?
Mimi kusema ukweli kuna yale maeneo ya vingunguti yaani nikikatiza mara moja tu huwa najisikia hovyo sasa najiuluza wale wakazi wa pale wanawezaje kukaa masaa 24 miaka na miakaPugu Dampo, Harufu ni kali pia Moshi wa takataka ni shida!
Ni kweli kabisa. Mimi kwetu ni Usangi Kirongwe. Toka nazaliwa kuna maji na umeme kitambo sana. Barabara ya lami. Usafiri upo muda wote. Coaster, mabasi makubwa, coaster etc.Nenda Upareni sehemu inaitwa Usangi barabara ilikuwepo toka enzi ya Mjerumani na shule za seminari.Maji yapo toka miaka ya uhuru kule juu ni kijani kitupu watu wengi wanawachulia Wapare ni watu wa njaa sana wanaishi sehemu ya ukame wanasema hivyo wakichukulia kule tambarare Mwanga,Same,Kisangara na Hedaru ila ukweli ni kwamba ni kama mji wa Moshi ulivyo wapare wanakaa kule milimani kwenye maendeleo ya kutisha.
Kule huwezi kuta nyumba za majani hata siku moja kuna shule nyingi mno watu wa kule ni wasomi mno walimkubali mkoloni mapema mno na kupeleka watoto wao shule.
Nenda Suji nenda Mamba nenda Kihurio ndio utajua wapare ni kabila dogo lakini wana maendeleo makubwa mno Mshana Jr ni shahidi.
Aise karibu tena aisee mimi nimeoa huko nasifia ukweni
Duh nauli ni kama unarudi Dar tenaKilolo Iringa huko kuna kijiji kinaitwa Kisakulo...ni balaa yani. Nauli tu ya boda kutoka Kidabaga unaambiwa 35,000