Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Vijiji vya Vunta na Kidunda, Hedaru, wilaya ya Same.

Ni vijiji vilivyo milimani - ktk Safu ya milima ya Usambara.
Ukitokea Mombo, kabla ya kufika Hedaru, unakata kulia na kuanza songombingo la kupanda mlima kuelekea vijiji hivi.
Issue hapa ni barabara ya vumbi yenye slope kubwa ajabu! Dereva akifanya kosa kidogo tu, mmekwisha kwani gari litaserereka bondeni takribani mita 600 - 800 hadi litakapogonga mwamba na kusimama! Bila gari imara lenye 4-W, huwezi kwenda kule.
Wakati wa kurudi toka Vunta, nilimuuliza mwenyeji wangu kuwa kwanini hawa Wapare waliamua kwenda kuishi sehemu hatarishi kama zile? Aliniambia kuwa, Wapare walikimbilia kwenda kule kwa ajili ya maficho kutokana na vita kati yao na maadui zao pamoja na maasidi wao - Wachagga. Ilikuwa zamani sana kabla ya ujio wa Wakoloni.
Baadaye waliweka makazi mpaka leo.
Uko sahihi
 
Bukiriro wilaya ya Ngara.....uchawi wa kutisha.....ukipangiwa kazi huko huwez kurud nyumban wanakjj wanakufungia huko
 
A
Milo ipo Chalinze hapo karbu na ruvu unaingia kulia km20, kulikuwa na kambi ya wapigania uhuru wa South Africa miaka ya 80 adi 90 kwa sasa imegeuzwa kuwa zahanati ya kijiji.

Sio mbali sana ila barabara ni mbovu sana na mvua ikinyesha hakupitiki, kilichonishangaza kipind nafany mradi flani wa afya ni maisha ya kule kuna kiwango kikubwa cha maambukizi ya HIV, unaweza pima watu 10 ukakuta 6 wanao teyari au familia nzima wameathirika.
Aiseeee hatarrr
 
Hadi Nyang'oro, kote hakuna vituo. Nimepazungumzia huko kwa sababu nililazimika kukaa hapo kwa wiki tatu kikazi, nami si shabiki wa videbe.

Kuna ukame balaa ila Watu wake wanakomaa kufuga kuliko kulima, wakiuhemea ule mto ambao kiangazi hali ni tete. Ila watu ni washkaji sana.

Ova
Toka Iringa mjini kituo cha mafuta unakikuta Migoli mbele ya Nyang'oro
 
  • Nzuri
Reactions: EEX
Niliwahi enda sehemu moja pwani chalinze inaaitwa Kilemela nilidhani ni pagumu kumbe kuna sehemu ngumu zaidi
 
Bukundi na Makao kwa Sasa Kuna uafadhali
Nilienda mwaka juzi huko Bukundi aisee hakuna rangi sijaona. Kuna vumbi hata kama una v8 lazima likufikie. Maisha magumu sana kuna sehemu nyingine huko sijui karibu na ziwa magadi daaah.!!!
 
Jamani mkoa wa simiyu hukoooo ndanindani nyumba zilivyojipanga, mchawi mchawi mchawi mganga mganga mganga mganga mfuga misukule mfuga misukule mwenye roho mtu mwema roho mbaya roho mbaya Hadi nikasema hivi shetani hakai kule kweli? Hapa ukienda upande wa kaskazini magharibi inaungia bariadi ndo unakutana na Kijiji funga kazi kinaitwa Gamboshi hiyo ndo mitaa ya JOKA LA MAKENGEZA ndo maana Kuna mtu akauliza mbona hii njemba Kila kashfa ya upigaji lazima alambe Kuna mtu akasema ooh yule ni mwanasheria nguli from havard! Hiyo siyo sababu kwani wakubwa wanajua ukipigwa juju unamfata JOKA anakupeleka huko Gamboga unabinuliwa kichuguu unachanjwa Kisha sangoma anakuweka dole lile kubwa bila kujali cheo wa protoko maana vyote unaviacha dsm kama siyo dom sasa mtu kama huyu Kuna wa kumgusa kweli?
Duh haya mambo yako kweli ndugu?imenishtua sana hii
 
Nenda Upareni sehemu inaitwa Usangi barabara ilikuwepo toka enzi ya Mjerumani na shule za seminari.Maji yapo toka miaka ya uhuru kule juu ni kijani kitupu watu wengi wanawachulia Wapare ni watu wa njaa sana wanaishi sehemu ya ukame wanasema hivyo wakichukulia kule tambarare Mwanga,Same,Kisangara na Hedaru ila ukweli ni kwamba ni kama mji wa Moshi ulivyo wapare wanakaa kule milimani kwenye maendeleo ya kutisha.
Kule huwezi kuta nyumba za majani hata siku moja kuna shule nyingi mno watu wa kule ni wasomi mno walimkubali mkoloni mapema mno na kupeleka watoto wao shule.

Nenda Suji nenda Mamba nenda Kihurio ndio utajua wapare ni kabila dogo lakini wana maendeleo makubwa mno Mshana Jr ni shahidi.

Aise karibu tena aisee mimi nimeoa huko nasifia ukweni
Ni kweli kabisa. Mimi kwetu ni Usangi Kirongwe. Toka nazaliwa kuna maji na umeme kitambo sana. Barabara ya lami. Usafiri upo muda wote. Coaster, mabasi makubwa, coaster etc.
Shule ni nyingi hadi zinakosa wanafunzi. Nyumba za kisasa. Karibu Usangi , Greenland.
 

Attachments

  • Screenshot_20250308_115621_Gallery.jpg
    Screenshot_20250308_115621_Gallery.jpg
    2 MB · Views: 1
Back
Top Bottom