Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

hadi leo huwa najiuliza hivi hawa watu vyoo vyao wanachimbaje, au wanaweka uchafu wao kwenye rambo?
Mimi kuna maswali huwa najiuliza sipati majibu.
1.Wakiwa na shughuli wanatandika vipi majamvi,watu wanakusanyika vipi kule juu?
2.Haya tufanye kuna mgonjwa anatakiwa kuwahishwa hospitali ambulance inafikaje kule juu?
3.Zimamoto inaendaje kule juu ikitokea ajali ya moto?
 
Bukiriro wilaya ya Ngara.....uchawi wa kutisha.....ukipangiwa kazi huko huwez kurud nyumban wanakjj wanakufungia huko
Serikali inatakiwa inapeleke Walimu na Polisi na ma Daktar
 
mara nyingi wanaoishi katika vijiji hivyo ni watu waliofukuzwa vijiji au mikoa mingine kwa makosa mbalimbali kama wizi,mauaji na uchawi hivyo wanakutana huko wenye tabia zinazofanana
 
Mwanza miambani wananoishi watia huruma sana japo wao wanaona wamepata viwanja city centre.

Huwa najiuliza walishindwaje kuweka makazi Usagara, Misungwi na Magu badala ya kubanana kwenye mawe kama mijusi ambako kupanda ni shida na inaweza kuchukulia lisaa kwenda sehemu unayoiona kwa mbele tu hapo.

View attachment 2378247
Dah kuna muwekezaji alikuwa anaitaka sehemu kama hiyo ngoja nimuoneshe hapa.
 
Kuna kijiji kipo singida sijui ni wilaya ile inaitwa Ikungi...kijiji chenyewe kinaitwa ighuka kimezungukwa na machimbo yan duh sio mchezo huduma za jamii zipo kwa asilimia 1%
 
Tanzania ni kubwa jameni kuna mgodi wa warusi sijui waarmenia upo kilomita 20 kutoka bunda unapita njia karibu na hospitali ya manyama njia ni ya vumbi nilienda huko kwa kazi maalumu nilienjoy maziwa fresh na supu ya samaki wa siku hiyo hiyo
 
Kijiji cha Kitapi, kipo wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani. Kipindi nimehamishiwa kikazi nimekuta maji ni kuchota visima vifupi, barabara imefunikwa na manyasi, hakuna mtandao wa simu hadi upande kwenye miti, nyumba zipo mbalimbali na zipo msitu, huduma ya soko ni kuanzia saa kumi Jioni hadi saa kumi na mbili jioni mchana watu wapo shamba, giza linaanza saa kumi na moja jioni kwa sababu ya msitu mnene, hakuna bodaboda zaidi ya zinazokuja na kutoka, mvua ikinyesha hakuna safari tena sababu ya utelezi na matope, husikii muungurumo wa gari kwa sababu gari pekee ni wakati wa mitihani ya darasa la saba.
aisee
 
Back
Top Bottom