Ni siku 21 leo, endelea kulala salama kipenzi chetu Rais John Pombe Joseph Magufuli

Ni siku 21 leo, endelea kulala salama kipenzi chetu Rais John Pombe Joseph Magufuli

Nikiondoka Mimi hizi ndege zitanunuliwa?

Je,nikiondoka Mimi hizi flyover zitajengwa?

Nikiondoka Mimi,hizi barabara zitajengwa?Mbona hapo kabla mambo haya yalikuwa hayafanyiki??

Leo,hayupo Tena lakin mbona Tanzania ipo na itazid kuwepo?

Dunia tunapita,nothing is permanent even the world itself...

Mungu,kaingilia Kati.
Too early to judge! Miradi aliyokuwa ameanzisha inaweza kukamilika kwa sababu za kisheria, lakini je kutakuwa na miradi mipya ya viwango hivyo tena?
 
Nikiondoka Mimi hizi ndege zitanunuliwa?

Je,nikiondoka Mimi hizi flyover zitajengwa?

Nikiondoka Mimi,hizi barabara zitajengwa?Mbona hapo kabla mambo haya yalikuwa hayafanyiki??

Leo,hayupo Tena lakin mbona Tanzania ipo na itazid kuwepo?

Dunia tunapita,nothing is permanent even the world itself...

Mungu,kaingilia Kati.

Hayupo tena baada ya kufanya na kuanzisha kile alichoamini na alichotamani kwa nchi yake

John Pombe Joseph Magufuli aliipenda nchi yake

Makao makuu imehamia Dodoma kama ilivyopangwa
Ikulu imejengwa na watanzania
Ndege zimenunuliwa
Reli zimejengwa
Barabara na madaraja vimejengwa
Shule na mahospitali vimejengwa na kuboreshwa
Makanisa na misikiti vimejengwa na kuboreshwa
Ametengeneza viongozi imara na wazalendo
Kawajengea watanzania walio wengi imani kwa serikali yao na upendo kwa nchi yao
Na mengine mengiiiiiii

Tuseme nini kwa Mungu zaidi ya kushukuru kwa zawadi ya uhai wake John Pombe Joseph Magufuli

Rest well our hero 💔🕊
 
Kosa walilolifanya kwangu ni kumleta Magufuli,

KWA sababu ya yeye,ndiyo chanzo Cha kuleta umaskin kwetu wamakonde kwa kutudhulumu korosho zetu na kusababisha mateso yasiyo na kifani,

Tulimkosea nin sisi hadi aje kuharibu kilimo chetu Cha korosho.
Aisee.. Pole sana Kiongozi.

Nakumbuka hili sakata. Ilibaki kidogo PM aliwe kichwa.
 
Natafuta Mbuzi aliyenona ili nimchinje kusudi niendelee Kulia Kimoyomoyo japo najua tu kwa Utamu wa Nyama utakuwa unanifanya niwe natabasamu nyakati zingine.

Tutachinja ng'ombe kabisa 40
 
Jembe lenu na nani? alale alipojiandalia mwenyewe. Nawaombea kulala salama Ben Saaa Nane, Azory Lwanda na wengineo waliodhulumiwa haki ya kuishi na shetani JIWE.
Tufafanulie sisi tusiojua linkage ya Jiwe na hao waliopotea, kwa nini huhusishwa na jiwe. Walifanya nini hao majamaa?
 
mama D am waiting for you! I want to take you out today! Umeteseka sana ndani hizi siku 21 ukiomboleza kwa kulia, kugalagala, kujivika nguo za magunia na kushindia malimao na ndimu siku nzima!😇

Kabisa mkuu, kufarijiana kwenye nyakati ngumu ndio upendo na utanzania wetu
Msiba unauma nyie acheni
Nimeteseka sana Tate Mkuu
 
Ishu ni Je! Miradi hiyo tunaihitaajii!? Ina tija!?over.
Hiyo ni short sighted view kwani wewe kutoihitaji siyo kuwa taifa lote haliihataji. Miaka minne iliyopita nilikuwa natoka Mwanza kwenda Atlanta, nilitakiwa kutoka mwanza na ndege ya Fastjet, halafu ndege hiyo ya kunitoa Mwanza kwenda Dar ikafuta safari yake ghafla na kunifanya nikose connection yangu ya KLM na kulazimika kulipia $250 zaidi kwenye nauli yangu kutapa flight iliyokuwa inafuata. Mtu kama wewe unaweza huhitaji usafiri wa anga kwa hiyo miradi ya ndege hutaki kuisikia. Vile vile unaweza kuwa unaishi mitaa ambayo hutaweza kupita kwenye daraja na Tanzanite hivyo unadhani huihitaji, lakini inawezekana watu wanaokupatia kipato wanalihitaji daraja hilo. Angalia maslahi ya taifa kwa mapana ndipo ujue maslahi yako binafsi.
 
Nikiondoka Mimi hizi ndege zitanunuliwa?

Je,nikiondoka Mimi hizi flyover zitajengwa?

Nikiondoka Mimi,hizi barabara zitajengwa?Mbona hapo kabla mambo haya yalikuwa hayafanyiki??

Leo,hayupo Tena lakin mbona Tanzania ipo na itazid kuwepo?

Dunia tunapita,nothing is permanent even the world itself...

Mungu,kaingilia Kati.
Mkuu THE BIG SHOW ...Mwamba KUSINI Karibuni sana......
 
Mmmhhh leo sio siku ya 20? Au Siku 21 kuanzia Tar 17? Haraka ya nini? Si tulikubaliana mitano tena?

18,19,20,21,22,23,24 - Week 01
25,26,27,28,29,30,31 - Week 02
01,02,03,04,05,06,07 - Week 03
Inaanzia siku iliotangazwa msiba wa Mtupoli 17 sio 18. Usitucheleweshe mkuu, samahani sana.
Imeisha hiyooo.. 🤸🏾‍♂️🤸🏽‍♀️🤸🏾‍♂️🤸🏽‍♀️🤸🏾‍♂️🤸🏽‍♀️🤸🏾‍♂️
 
Hiyo ni short sighted view kwani wewe kutoihitaji siyo kuwa taifa lote haliihataji. Miaka minne iliyopita nilikuwa natoka Mwanza kwenda Atlanta, nilitakiwa kutoka mwanza na ndege ya Fastjet, halafu ndege hiyo ya kunitoa Mwanza kwenda Dar ikafuta safari yake ghafla na kunifanya nikose connection yangu ya KLM na kulipia $250 zaidi kwenye nauli yangu kutapa flight iliyokuwa inafuata. Mtu kama wewe unaweza huhitaji usafiri wa anga kwa hiyo miradi ya ndege hutaki kuisikia. Vile vile unaweza kuwa unaishi mitaa ambayo hutaweza kupita kwenye daraja na Tanzanine hivyo unadhani huihitaji, lakini inawezekana watu wanaokupatia kipato wanalihitaji daraja hilo. Angalia maslahi ya taifa kwa mapana ndipo ujue maslahi yako binafsi.
Ungeondoka siku moja kabla ukaja kulala Dar hasara isingekuwa kubwa hivyo. Waswahili wanasema " Msafiri ali pwani" unapokuwa na safari muhimu kama sio ya ghafla ni muhimu kuzingatia vitu kama hivyo
 
Hiyo ni short sighted view kwani wewe kutoihitaji siyo kuwa taifa lote haliihataji. Miaka minne iliyopita nilikuwa natoka Mwanza kwenda Atlanta, nilitakiwa kutoka mwanza na ndege ya Fastjet, halafu ndege hiyo ya kunitoa Mwanza kwenda Dar ikafuta safari yake ghafla na kunifanya nikose connection yangu ya KLM na kulipia $250 zaidi kwenye nauli yangu kutapa flight iliyokuwa inafuata. Mtu kama wewe unaweza huhitaji usafiri wa anga kwa hiyo miradi ya ndege hutaki kuisikia. Vile vile unaweza kuwa unaishi mitaa ambayo hutaweza kupita kwenye daraja na Tanzanine hivyo unadhani huihitaji, lakini inawezekana watu wanaokupatia kipato wanalihitaji daraja hilo. Angalia maslahi ya taifa kwa mapana ndipo ujue maslahi yako binafsi.
Ubinafsi na choyo ndio vinavyotutesa wabongo
Kama kitu sio cha muhimu kwako chaweza kuwa muhimu sana kwa wengine
Kila alichofanya JPM ni kwaajili ya Watanzania
 
Kipaombele chetu sisi wanyonge ni maisha yetu,

Hayo yote uliyoyasema hayana maana kwangu Kama Mimi nimelima korosho zangu then wewe from nowhere unakuja kuingiza siasa na ujinga wako kisha unaua soko la zao hilo kisha utegemee sisi tuje tushangilie ndege,sijui flyovers na kadhalika,zina maana gani kwangu kama hazinipi matumain yeyote...

Airport chato inanipa faid gan,mbuga hiyo ya burigi Ina faida gan kwetu,

Miaka zaid ya sita hajafanya ongezeko lolote la mishahara kwa watumishi wa umma,Hakuna ajira mpya vijana wanamalizia vyuo kila mwaka wanateseka ukiuliza anasema anajenga barabara,sijui ananunua ndege,

Ameua democracy,freedom of speech na uhuru wa vyombo vya habari,

Haitoshi kalishika bunge mpaka kufikia hatua wabunge na speaker kupayuka kutaka wamuongezee muda atawale nchii hii,na eti kama hataki Alazimishwe,nan angependa haya mauza uza yaendelee
 
Wanyonge wanamshukuru na kumuombea dua kila siku kwa

Serikali imara iliyozuia mgambo wahuni kuwamwagia mitaji yao
Reli zinatumika na wanyonge zaidi
Barabara na madaraja vimejengwa
Shule na mahospitali vimejengwa na kuboreshwa
Elimu bure
Makanisa na misikiti vimejengwa na kuboreshwa
Ametengeneza viongozi imara na wazalendo
 
Wanyonge wanamshukuru na kumuombea dua kila siku kwa

Serikali imara iliyozuia mgambo wahuni kuwamwagia mitaji yao
Reli zinatumika na wanyonge zaidi
Barabara na madaraja vimejengwa
Shule na mahospitali vimejengwa na kuboreshwa
Elimu bure
Makanisa na misikiti vimejengwa na kuboreshwa
Ametengeneza viongozi imara na wazalendo
Kimara wavunjieni nyumba ila watu wa Mwanza msiwavunjie hao ni wapiga kura wangu.

Wanyongeeeeeeeeeee.
 
Kwahio wale wa kusherekea, Telenovela, Bongo Fleva na Shamrashamra nyingine ruksa kuanzia kesho ?
 
Tunamshukuru Mungu kwa Maisha ya JPM.
 
Back
Top Bottom