Ni smart TV gani 4K kwa sasa ipo vizuri sana?

Sio kwa sasa tu kwa kila wakati ni Lg Na Samsung tu
Hii TV niliyonayo ni Samsung HD inch 32, nilinunua laki saba wakati ndio zinatoka, imeshawahi kupigwa chini kwenye domestic violence lakini iko vilevile na Ina miaka zaidi ya 10, je Samsung bado watakuwa na bidhaa imara kiasi hiki kwa miaka hii?
 
Samsung, LG Hisense
 
Unaweza kujazia nyama kidogo kwa faida ya wengi?
Hapa Bongo kwa Tsh 650,000/= unapata Hisense yenye inchi 43, smart kabisa na ni 4K resolution, umeshamaliza kazi. Sasa wewe huoni hiyo Samsung umenunua kwa laki saba halafu ni 32 inches tu. Ukikutana na muuzaji mwenye tamaa sana hiyo Hisense unapata kwa laki saba. Kupata Samsung au LG yenye ubora sawa na Hisense hii inakupasa uwe na milioni moja kupanda.
 
Lg Tv with magic remote control,
 
Kufananisha Hisense na Samsung Ni Sawa na kufananisha tecno na iPhone

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Hii magic remote INA maajabu gani?
Inafanya kazi kama remote ya kawaida na wakati huo huo kama mouse na ina mic, ukii program badala ya kuandika unaongea tu ina command.

Mfano unataka kuangalia youtube, unabonyeza mic unaongea open youtube tom and jerry, TV itafungua youtube na content za tom&jerry
 
Kufananisha Hisense na Samsung Ni Sawa na kufananisha tecno na iPhone

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
Si sawa, kwenye TV cha muhimu ni ubora wa kioo. Sio sawa kabisa na simu. Simu ina mambo mengi maCPU, maGPU huko na makolokolo kibao.

Turudi kwenye TV sio simu hizo Samsung ni nzuri lakini ni overpriced. Ukinunua Samsung ya milioni 1 unachomzidi mwenye Hisense ya laki sita ni jina la brand tu yaani laki nne yote unakuwa umelipia brand na laki sita ndio actual value ya product
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…