Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
CCM walilazimika kumpa madaraka Magufuli kutokana na mazingira ya wakati ule ila walidhani wangeweza kumdhibiti. Magufuli akawashangaza na kuwafumba midomo hata wale ambao walidhani wangekuwa na sauti juu yake. Mmoja wa watu pekee ambaye NADHANI bado alibaki na kauwezo fulani ka kumkemea alikuwa ni Benjamin Mkapa.
Lakini kwa wengine Magufuli alikuwa too much. Si vigogo si nani, wote waliishi kwa hofu wasijue mzee anaweza akaamka na maamuzi gani juu ya maisha yao.
Sasa hivi CCM wako comfortable, Mama ameweza kuwadhibiti watu wa Magufuli. Polepole kamalizwa kisiasa kwa kupewa ubalozi na wengine kama kina Mwigulu ndiyo wanachafuliwa CV zao za kuwamaliza kabisa kisiasa.
Ila ninachoona CCM ni chama kinachotapatapa. Toka 1995 ni chama ambacho ni nusu mfu. Chochote wanachoweza kujishikizia ili waendelee tu kubaki madarakani, wanafanya hivyo. Siyo tena habari za itikadi au principles. Kwa maneno ya Kolimba, ni chama kilichopoteza dira na muelekeo.
Kesho wanaweza kumtengeneza 'Magufuli' mwingine ambaye watajiaminisha wataweza kumdhibiti tofauti ya yule wa nyuma au mazingira yatawalazimisha kumuunga mkono, na watatulazimisha tumkubali. Na kama kawaida yetu, tutakuwa tunarudia makosa ya nyuma bila kujifunza chochote kwa yaliyopita.