Ni hatari sana unapokuwa na chama kinachofanya chochote kuendelea kukaa madarakani. Kwa sasa CCM wako tayari kufanya lolote ili kubaki madarakani, na sio kwamba wako kwa ridhaa ya umma, bali wanaunyamazisha umma, na sauti zinazotakiwa kutoka ni zile za propaganda kuwa CCM inakubalika sana.
Wakiona hiyo porojo yao haikai vizuri, wanasema ni kweli CCM haipaswi kuendelea kukaa madarakani, lakini ni chama gani kipewe nchi. Ukiwauliza mbona hapo Kenya vyama ni vipya kila uchaguzi, na Kenya bado wako mbele yetu kwenye uchumi, afya, elimu, siasa nk wanapotezea.