Ni suala la muda tu kabla CCM hawajatuletea 'Magufuli' mwingine

Majirani gani hao wanaotushangaa? Nitajie nchi yeyote yenye political stability kutuzidi Watanzania kwenye eneo la East & Central Africa?

Basically wote wakikorofishana sisi ndiyo huwa kimbilio lao kwa kujificha kama wakimbizi au kuwapatanisha. Acheni uwongo vijana
Kenya tu hapo unafikiri viongozi wao wanaongoza maiti kama huku Tanzania?
 
Hao ndiyo usiwaseme kabisa. Kwanza mpaka sasa hivi Urais umehusisha familia moja to ya Gatundu tokea Mzee Kenyatta, shemeji yake Moi, Binamu yake Mwai Kibabi na mwnaye Uhuru.

Unatamani maisha na siasa za Wakenya waliouana mwaka 2008 baada ya matokeo ya uchaguzi? Wewe ni kiazi mbatata
 
CCM walilazimika kumpa madaraka Magufuli kutokana na mazingira ya wakati ule ila walidhani wangeweza kumdhibiti. Magufuli akawashangaza na kuwafumba midomo hata wale ambao walidhani wangekuwa na sauti juu yake. Mmoja wa watu pekee ambaye NADHANI bado alibaki na kauwezo fulani ka kumkemea alikuwa ni Benjamin Mkapa.

Lakini kwa wengine Magufuli alikuwa too much. Si vigogo si nani, wote waliishi kwa hofu wasijue mzee anaweza akaamka na maamuzi gani juu ya maisha yao.

Sasa hivi CCM wako comfortable, Mama ameweza kuwadhibiti watu wa Magufuli. Polepole kamalizwa kisiasa kwa kupewa ubalozi na wengine kama kina Mwigulu ndiyo wanachafuliwa CV zao za kuwamaliza kabisa kisiasa.

Ila ninachoona CCM ni chama kinachotapatapa. Toka 1995 ni chama ambacho ni nusu mfu. Chochote wanachoweza kujishikizia ili waendelee tu kubaki madarakani, wanafanya hivyo. Siyo tena habari za itikadi au principles. Kwa maneno ya Kolimba, ni chama kilichopoteza dira na muelekeo.

Kesho wanaweza kumtengeneza 'Magufuli' mwingine ambaye watajiaminisha wataweza kumdhibiti tofauti ya yule wa nyuma au mazingira yatawalazimisha kumuunga mkono, na watatulazimisha tumkubali. Na kama kawaida yetu, tutakuwa tunarudia makosa ya nyuma bila kujifunza chochote kwa yaliyopita.
Suluhisho kwa uongozi mzuri wa nchi yetu mbeleni ni kupatikana kwa Katiba Mpya.
 
Hao ndiyo usiwaseme kabisa. Kwanza mpaka sasa hivi Urais umehusisha familia moja to ya Gatundu tokea Mzee Kenyatta, shemeji yake Moi, Binamu yake Mwai Kibabi na mwnaye Uhuru.

Unatamani maisha na siasa za Wakenya waliouana mwaka 2008 baada ya matokeo ya uchaguzi? Wewe ni kiazi mbatata
Hatutafuti ukamilifu kila sehemu kuna mapungu yake na hapo Kenya tatizo lao kubwa ukabila na ndio ulichokizungumzia hapo, je sisi tatizo letu ni nini ikiwa unakataa ujinga kuwa sio tatizo letu? Sie tupo vile vile hadi leo bado ccm wanatuburuza tu anaibuka waziri mmoja bila hofu anatuambia kama hutaki hama nchi ni kwa sababu anajua anadeal na wajinga hawana la kumfanya. Halafu unakuja na story za kwamba et Magufuli mshamba hakufaa kutuongoza sisi, kwa ujanja upi tulionao?
 
CCM walilazimika kumpa madaraka Magufuli kutokana na mazingira ya wakati ule ila walidhani wangeweza kumdhibiti. Magufuli akawashangaza na kuwafumba midomo hata wale ambao walidhani wangekuwa na sauti juu yake. Mmoja wa watu pekee ambaye NADHANI bado alibaki na kauwezo fulani ka kumkemea alikuwa ni Benjamin Mkapa.

Lakini kwa wengine Magufuli alikuwa too much. Si vigogo si nani, wote waliishi kwa hofu wasijue mzee anaweza akaamka na maamuzi gani juu ya maisha yao.

Sasa hivi CCM wako comfortable, Mama ameweza kuwadhibiti watu wa Magufuli. Polepole kamalizwa kisiasa kwa kupewa ubalozi na wengine kama kina Mwigulu ndiyo wanachafuliwa CV zao za kuwamaliza kabisa kisiasa.

Ila ninachoona CCM ni chama kinachotapatapa. Toka 1995 ni chama ambacho ni nusu mfu. Chochote wanachoweza kujishikizia ili waendelee tu kubaki madarakani, wanafanya hivyo. Siyo tena habari za itikadi au principles. Kwa maneno ya Kolimba, ni chama kilichopoteza dira na muelekeo.

Kesho wanaweza kumtengeneza 'Magufuli' mwingine ambaye watajiaminisha wataweza kumdhibiti tofauti ya yule wa nyuma au mazingira yatawalazimisha kumuunga mkono, na watatulazimisha tumkubali. Na kama kawaida yetu, tutakuwa tunarudia makosa ya nyuma bila kujifunza chochote kwa yaliyopita.
Kwa utitili wa tozo hizi kwa mlala hoi ni SUALA LA MUDA CCM kuendelea kuongoza nchi. Labda tuone zinafanya nini kwetu (wapiga kura) sio kwao tu (viongozi)
 
Wahuni gani? Na Magufuli alimfunga muhuni gani hata mmoja? Afadhali JK aliwafunga Mramba na Daniel Yona, na kuwashtaki vigogo wengine kama akina Zombe, Mzuzuri n.k

JPM aliwahi kumfunga kigogo gani wa CCM?
Hili nalo kweli. Alipoteza muda kukimbizana na akina Lissu na Mbowe akiwaacha akina Change waliotupiga pesa za Rada mchana kweupe. Kwenye hili alikuwa na unafiki wa wazi wazi.
 
Ila mtu wa aina ya magufuli hatakiwi kurudi tena Tz, kilikuwa kipindi cha kishetani na unyama wa kikatili kabisa!
 
serikali ya Tanzania haipaswi kuitwa ya mtu, bali iitwe serekali ya ccm au ya Tanzania.
Ila ukifuatilia mada na issues mbalimbali nchini unagundya unafiki ulivyo mkubwa, leo eti mnasena hadharani serikali ya Rais Samia 'imetoa ... ' na hakuna mtu anasimama kuongelea hilo.

HUo ni unafiki ule wa kuchafuana kisa jamaa alikuwa mbabe, ahahahaaa...
 
Back
Top Bottom