Ni suala la muda tu kabla CCM hawajatuletea 'Magufuli' mwingine

BM si kwamba alikuwa anammudu,hapana alikuwa kama mshauri wake.

hawa wengine walijichanganya pale walipotaka kujifanya ni remote,
Mshauri wake ambaye kila mara kwenye hotuba zake alikuwa akimnanga kuhusu alivyo binafsisha viwanda

Na majibu mengine ya kimajungu kama alivyosema wastaafu wanawashwawashwa baada ya Mkapa kusema mfumo wetu wa elimu uangaliwe upya
 
Kipindi cha Jakaya machawa walikuwa hawapo, Uchawa umeanzia kwa JPM.
Kazi ya machawa Ni kusifia/kutetea pasipostahili sifa/utetezi.

Sasa kwa hizi tozo, mfumuko wa bei, maisha magumu bila machawa labda Raisi ajiuzuru.
Labda ulikuwa mdogo, kipindi cha JK machawa waliokuwepo sema hawakuwa wengi kama kipindi cha Magufuli
 
Magufuli hater at his best!!
 
Swala la kusifia mi nililisia ata kwa Kikwete, suala Mh Jakaya katoe hela tujenge hikihiki na kile zilikuwepo sema tu 2014 huko ni mbali hukumbuki
Ndio zilikuwepo,ila kipindi cha Magufuli ilikuwa mara dufu.. nyimbo na kwaya za kumsifu Magufuli zikatamalaki TBC masaa 24
 
Wanajf tukybaliane kwa pamoja kuwa Magufuli hakuwa na akili sawa sawa maana kuna vitu vingi tu alivyovifanya hata wenyeviti wa vitongoji wa kule nyakato,chato hawawezi kuvifanya


Kiufupi hakutakiwa kuwa hata mkuu wa shule ya msingi Katerero
Labda nchi nyengine ndio hakufaa kuwa hata mkuu wa shule ila sio Tz ambayo ndio wajinga hadi majirani zetu wanajua hilo. Yani mnataka mtoe viongozi miongoni mwenu wasiofanana na ninyi wenyewe.
Angalia leo majibu ya mawaziri kama Nape,Mwigulu na January kwa sisi wananchi ndio utajua kama Jiwe hakupaswa kuwa kiongozi hapa je ni wapi angetakiwa kuwa kiongozi?
 
Alikuwa na mapungufu ila alikuwa na nia ya dhati ya kuona nchi inasonga mbele tofauti Sana na wale wahuni walioigeuza ikulu kuwa sehemu ya kuufanyia biashara na kulindana kwa msemo wa ''ccm ina wenyewe''
Wahuni gani? Na Magufuli alimfunga muhuni gani hata mmoja? Afadhali JK aliwafunga Mramba na Daniel Yona, na kuwashtaki vigogo wengine kama akina Zombe, Mzuzuri n.k

JPM aliwahi kumfunga kigogo gani wa CCM?
 
Magufuli si ndio alisababisha hata Kenya, Burundi, Rwanda kutufungia mipaka wakulima tukapata hasara kwa kukosa soko? Au kimataifa kwako ni wazungu pekee?
 
Aliwadhibiti walilokuwa wakifanya nchi ni ya kwao wakati yeye ndio alijimilikisha nchi na kikundi chake cha waovu kama akina Makonda, Sabaya, Dotto James?
 
Mwingine naamini atakuja tu !! There is no other way!!
 
Duh !!
 
Labda alikuwa ana lengo lingine lakini je kwani hakujua kuwa anaishi na kibetri kifuani ?? Je watu wa hivyo huwa wanaishi miaka mingi na vibetri vyao ?? Jibu ni kwamba huwa hawaishi sana !!
 
Labda alikuwa ana lengo lingine lakini je kwani hakujua kuwa anaishi na kibetri kifuani ?? Je watu wa hivyo huwa wanaishi miaka mingi na vibetri vyao ?? Jibu ni kwamba huwa hawaishi sana !!

..mwaka 1995 kuna jamaa aliniambia kuwa mmoja wa vigogo serikalini anatumia pacemaker.

..huyo kigogo yuko mpaka leo na ana umri mkubwa kuliko Magufuli.

..kilichomuua Magufuli ni covid-19 ambayo ikishambulia inapelekea mgonjwa kushindwa kuyakabili magonjwa ambayo ameyadhibiti kwa muda mrefu.

..kwa mfano, mhusika anaweza kuwa ameishi na kisukari muda mrefu na ameweza kuuthibiti ugonjwa huo. Sasa Covid-19 ikipiga hodi hupelekea mlipuko wa kisukari ambacho hakidhibitiki na mwisho wake ni kifo.

..Magufuli alijiamini mno na kuzembea dhidi ya Covid-19. Kosa lililogharimu maisha yake ni kutoka Chato alikokuwa amefichama kuja mjini kwenye maambukizi.
 
Hata mimi nilikuwa najiuliza huyu mheshimiwa anajiamini nini na kujiexpose wakati covid 19 imepamba moto ? !!
 
.
Watanzania majirani zetu wote wanatushangaa kwa ujinga tulionao, sasa iweje wewe uone Jiwe ndio mshamba? Kwa ujanja upi mlionao watanzania hadi uone Jiwe hakufaa kuwaongoza nyie?
Majirani gani hao wanaotushangaa? Nitajie nchi yeyote yenye political stability kutuzidi Watanzania kwenye eneo la East & Central Africa?

Basically wote wakikorofishana sisi ndiyo huwa kimbilio lao kwa kujificha kama wakimbizi au kuwapatanisha. Acheni uwongo vijana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…