Ni Taarifa gani nzuri au kitu kizuri ulishawahi kuipata/kupata ukamshukuru Mungu/Mwenyezi Mungu?

Ni Taarifa gani nzuri au kitu kizuri ulishawahi kuipata/kupata ukamshukuru Mungu/Mwenyezi Mungu?

Hello wakuu,
Habari ya weekend, hivi ni taarifa gani nzuri ulishawahi kupata ukaishia kumshukuru Muumba, Mimi nakumbuka kwenye matokeo ya std 7 st Kayumba, nilichaguliwa kidato cha kwanza kwenda boarding school, na mtaani kwetu ilikua ukifaulia mbali kidogo au boarding unaonekana noma,sasa nakumbuka darasani kwetu niliwawakilisha kwenda hako kaboarding school, sijui hata ilikuaje maana sikua kipanga hivo ukilinganisha na wengine[emoji120] nauli from home to hiyo shule ilikua TZS 500 tu kwa daladala au unaweza kutembea kwa miguu tu[emoji23][emoji23] ila furaha yake si mchezo.

Baada ya kumaliza chuo, msoto kidogo mtaani(broke), huku nikipambana na interviews na kusambaza CVs, interviews zingine nyingi tu nilikua nafeli[emoji2960] nakumbuka siku niliyopigiwa simu kwamba, umepata kazi uje kucheki mkataba, Aisee nilijiskia vizuri mno.

Ni mengi mazuri Muumba ametutendea, ila karibu ushare na sisi lolote utakalojisikia.
Happy week ending wote.
Nlivyofaulu 4m four, nlivyofaulu form six, nlivyograduate nlilia machozi kabisa, siku ya engagement nlilia chozi la furaha, nlivyosikia mwanangu analia kwa mara ya kwanza sekunde chache baada ya kujifingua nlitokwa machozi, hizi ni moments muhimu sana ambazo furaha yangu ilipotiliza had machozi yakatoka. Mungu ni mwema

Sent from my SM-G930V using JamiiForums mobile app
 
Kuna taarifa nyingi ziliniacha na furaha kubwa kwani mengi sikuwahi hata kumuomba Mungu wala kuwazia kuwa nastahili.
Moja nilipofaulu form 6, nikiwa private candidate baada ya kushindwa kwenda shule kwa kukosa ada na nauli tu. Nikajiunga UDSM, nikapata shida kubwa(sitaki hata kukumbuka), hata sijui ilikuwaje nikamaliza Chuo, ukiniuliza siwezi hata kukumbuka ilikuwaje nikamaliza Chuo.
Ajabu la pili hata niliite ajabu, kabla ya wiki 1 kwa UE mwaka wa mwisho nikampoteza Mama yangu kipenzi, huyu ndio tumaini langu pekee lililokuwa limebaki ukiachia Mungu. Ilikuwa ngumu kurudi kufanya UE, ila nikarudi Chuo nikaingia kwenye paper nikijua nakamilisha idadi tu ya wanaotarajia kumaliza Chuo ila sitoboi.
Baada ya paper, nikarejea kijijin kwetu ili nikajipange kwenda kuripoti Ukerewe ambako nilipangiwa kwenda kama Mwalimu...Kwa wale wa 2009 wanajua tulikuwa tukipangiwa vituo hata kabla ya matokeo ya mwisho kama sikosei. Kabla sijaondoka nikapigiwa simu na rafiki yangu akaniambia kuna shirika wanatafuta Walimu, nikataka kumpotezea kwani nilijua hata GPA yangu haitakuwa kivutio. Ila jamaa alinisihi mno, kwani anajua uwezo wangu pamoja na muda mwingi kutoutumia darasani ila kwenye presentation aliona kitu kwangu.
Baada ya kufika Dar tu nikaulizwa nina passport ya kusafiria? Nikashangaa, nikapewa mtu pale uhamiaji akanifanyia utaratibu nikapata passport kesho yake nikaikabidhi kwa mhusika. Bila kuambiwa kitu, nikapelekwa Mikocheni nikawakuta wenzangu 7 tukawa 8.
Taarifa ikawa tunasafiri week ijayo kwenda nje kwa wiki 2 kujifunza mambo(nchi nitaihifadhi). Hapo niliamini Mungu ni mwenye huruma sana.
Nilirudi nikapewa ajira kwakweli sikuwahi kuamini kama nilistahili, ila ninachokiamini nilikuwa na uwezo mkubwa mazingira tu ndio yalikuwa magumu. Niliitendea haki kazi niliyopewa.
Nilizunguka Duniani mpaka mwaka 2016 hapo ndio nilipata jaribu la maisha tena, nikiwa safarini nilipata ajali mbaya iliyopelekea mauti ya Mama wawili niliowapa lifti tu(RIP Wamama ), Nikapoteza matumaini tena, sikiweza kwenda kazini tena, pamoja na kupewa muda ila nilikuwa kama mtu aliyerukwa na akili.
Mwaka 2017 nikajaribu kuomba program fulani US, siku nilipopata Email na simu ya kuwa shortlisted nikakumbuka Mungu ananipenda mno kwani niliamini labda sina sifa na watu niliokutana nao kwenye interview niliamini wananizidi kuanzia matokeo ya darasani, Nikafanikiwa na kuwa finalist, ila ikawa nifanye TOEFL then tusubirie zaid ya miezi 5 mbele kujua nani na nani wataenda.
Nikaanza kula msoto, nikapoteza hata marafiki na ndugu mbona ukisikia kufulia ndio huko. Hili jambo sikumuambia mtu yoyote yule zaidi, kwahiyo aliyekuwa anajua ni wale finalist wenzangu tu ambao tumejuana tulipofikia hatua hiyo. So hakuna mtu anajua nasubiria bahat ya kutimkia US.
Ilipofika mwezi wa 9, natoka zangu kuswali, ile kuwasha simu nakutana na Email ilibidi niswali Sunna kwanza labda sijaona vizur, hatimae mimi ni miongoni mwa wanaoenda US...
Nini nataka kusema?? Kila gumu lina suluhisho mbele ya Mungu, katika taarifa nzuri nilizowahi kupokea, 90%sijawahi kutegemea wala kumuomba Mungu.
 
Kitendo cha yule kiumbe kunipenda kwa dhati, hapo kulitokea tatizo fulani hivi sio zuri, lakini yule kiumbe alibaki na mie.

Hiyo siku nashangaa kanipigia cm, "hello coca najua ni situation iliyopo mbele yetu, ila usijari mie nipo nawee na siwezi kukuacha peke ako, nimejipanga kwa lolote sitajari watu watanichukuliaje au kunionaje ila nipo nawee" akamaliziaa "NAKUPENDAA SANA na kiss juu..

Sitasahau, EEH Jah aendelee kumuweka huyu kiumbe huko aliko na wengine wafurahie uwepo wake kwao.

Mapenzi ya kweli yapo!!!
 
Nlivyofaulu 4m four, nlivyofaulu form six, nlivyograduate nlilia machozi kabisa, siku ya engagement nlilia chozi la furaha, nlivyosikia mwanangu analia kwa mara ya kwanza sekunde chache baada ya kujifingua nlitokwa machozi, hizi ni moments muhimu sana ambazo furaha yangu ilipotiliza had machozi yakatoka. Mungu ni mwema

Sent from my SM-G930V using JamiiForums mobile app
Amen hongera sana kwa moments nzuri hivo👏
 
Kupata faraja ya kweli katikati ya dhiki na tabu,, .......hakika sitasahau tukio lile lilifanya niuone wema wa Mungu maishani mwangu, acha niishie hapa
Wow Mungu ni mwema, japo kama hutojali ukipata muda share na sisi tujifunze kitu dear😘
 
Kitendo cha yule kiumbe kunipenda kwa dhati, hapo kulitokea tatizo fulani hivi sio zuri, lakini yule kiumbe alibaki na mie.

Hiyo siku nashangaa kanipigia cm, "hello coca najua ni situation iliyopo mbele yetu, ila usijari mie nipo nawee na siwezi kukuacha peke ako, nimejipanga kwa lolote sitajari watu watanichukuliaje au kunionaje ila nipo nawee" akamaliziaa "NAKUPENDAA SANA na kiss juu..

Sitasahau, EEH Jah aendelee kumuweka huyu kiumbe huko aliko na wengine wafurahie uwepo wake kwao.

Mapenzi ya kweli yapo!!!
Jamani baby sis, usituambie hamko pamoja na huo wema wake kwako, mkaachana?😒
 
Back
Top Bottom