KERO Ni takribani siku tano sasa Mji wa Kahama hakuna huduma ya maji

KERO Ni takribani siku tano sasa Mji wa Kahama hakuna huduma ya maji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Shadow569

New Member
Joined
May 5, 2026
Posts
1
Reaction score
1
Mimi ni mkazi wa Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga. Ni takribani siku tano sasa hakuna huduma ya maji, hasa katika Mtaa wa Majengo, Kahama, ambako kuna idadi kubwa ya wakazi.

Licha ya kuwepo kwa baadhi ya visima vya watu binafsi, maji yake si salama kwa matumizi. Hata baada ya kuoga, baadhi ya wakazi hupata muwasho mwilini, hali inayotia wasiwasi kuhusu usalama wa maji hayo kwa ajili ya kupikia na kunywa. Hivyo, afya za wananchi zipo hatarini.

Ombi: Mamlaka ya Maji Safi na Salama Kahama (KUWASA) itoe taarifa kwa wananchi endapo huduma ya maji itakatika kwa muda fulani, ili wananchi waweze kujipanga. Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ina redio zisizopungua mbili ambazo zinaweza kutumika kutoa taarifa hizo.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom