Ni Tanzania pekee kukuta watu wanasikiliza nyimbo ya lugha wasiyoijua

Muite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
2,971
Reaction score
6,607
Nimefanikiwa kufika nchi kadhaa na sikuwahi kuona watu wa nchi hizo wakisikiliza au kufurahia nyimbo zilizoimbwa kwa lugha za nchi zingine wasizozijua.

Lakini hapa kwetu miaka nenda rudi tangu nakua miaka ya 70 nimekuwa nikishuhudia watu wengi wakisikiliza nyimbo za Kizungu na ukiwafuatilia hata neno moja hawajui maana yake, tena nakumbuka hii ni hadi vijijini ambapo hata salamu ya kiingereza haijui, nakumbuka wengine waliweza kukariri nyimbo yote ya Bob marley au Celine Diana.

Naona kwa nyimbo za Kongo ndio usiseme yaani ndizo zinazobamba kwenye baa na kwenye maharusi. Hata hapa ninapoandika hii mada nipo baa moja kali sana lakini mwanzo mwisho ni nyimbo za Kongo.

Kwa usomi wangu mdogo ninafikiri huenda kuna hujuma tulifanyiwa na wakoloni wetu wakatupatia dawa za kulevya ndio maana wengi tupo kama wajingawajinga sana , na wengine wapo kama mateja hivi NA NDIO MAANA NCHI HII NI RAHISI SANA KWA WATAWALA
 
Acha fix

Usidanganye vitu usivyovijua.

Niko Ouagadougou hapa wanasikilizia nyimbo za Diamond na za Tanzania sana tu na hadi kwenye redio station zinapigwa na hawajui kiswahili hata robo!

Nilikuwa Cote d'avoire pia wanasikilizia sana tu Acha uongo
 
Kuna songi la ki Ethiopia linaitwa Serk Addis linanibamba balaa nalisikiliza sana....ila sijui hata wanaimba nini usikute songi la mazishi 🙄

View attachment 2744147
Pigo kama za Meddy mnyarwanda,bila shaka alicopy huko
download.jpg
 
Nimefanikiwa kufika nchi kadhaa na sikuwahi kuona watu wa nchi hizo wakisikiliza au kufurahia nyimbo zilizoimbwa kwa lugha za nchi zingine wasizozijua. Lakini hapa kwetu miaka nenda rudi tangu nakua miaka ya 70 nimekuwa nikishuhudia watu wengi wakisikiliza nyimbo za Kizungu na ukiwafuatilia hata neno moja hawajui maana yake, tena nakumbuka hii ni hadi vijijini ambapo hata salamu ya kiingereza haijui, nakumbuka wengine waliweza kukariri nyimbo yote ya Bob marley au Celine Diana. Naona kwa nyimbo za Kongo ndio usiseme yaani ndizo zinazobamba kwenye baa na kwenye maharusi. Hata hapa ninapoandika hii mada nipo baa moja kali sana lakini mwanzo mwisho ni nyimbo za Kongo.

Kwa usomi wangu mdogo ninafikiri huenda kuna hujuma tulifanyiwa na wakoloni wetu wakatupatia dawa za kulevya ndio maana wengi tupo kama wajingawajinga sana , na wengine wapo kama mateja hivi NA NDIO MAANA NCHI HII NI RAHISI SANA KWA WATAWALA
kikubwa beat tu mashairi ni ya muandishi.... kuna ngoma moja naikubali beat yake tu ya ghana huko inaitwa "kyenkey bi adi mawu" ya Alhaji Frimpong

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nimefanikiwa kufika nchi kadhaa na sikuwahi kuona watu wa nchi hizo wakisikiliza au kufurahia nyimbo zilizoimbwa kwa lugha za nchi zingine wasizozijua.

Lakini hapa kwetu miaka nenda rudi tangu nakua miaka ya 70 nimekuwa nikishuhudia watu wengi wakisikiliza nyimbo za Kizungu na ukiwafuatilia hata neno moja hawajui maana yake, tena nakumbuka hii ni hadi vijijini ambapo hata salamu ya kiingereza haijui, nakumbuka wengine waliweza kukariri nyimbo yote ya Bob marley au Celine Diana.

Naona kwa nyimbo za Kongo ndio usiseme yaani ndizo zinazobamba kwenye baa na kwenye maharusi. Hata hapa ninapoandika hii mada nipo baa moja kali sana lakini mwanzo mwisho ni nyimbo za Kongo.

Kwa usomi wangu mdogo ninafikiri huenda kuna hujuma tulifanyiwa na wakoloni wetu wakatupatia dawa za kulevya ndio maana wengi tupo kama wajingawajinga sana , na wengine wapo kama mateja hivi NA NDIO MAANA NCHI HII NI RAHISI SANA KWA WATAWALA
Nasikiliza Ngoma yoyote hata ikiwa VALHALLA ilimradi melody ipo poa...

Ila tuache UONGO jumatano bar ya kitaa Kuna boa sana Kuna wana wanaimba karaoke si elewagi wale jamaa tumewakosea Nini sisi walevi.
 
Back
Top Bottom