Ni Tanzania pekee kukuta watu wanasikiliza nyimbo ya lugha wasiyoijua

Me nasikiliza sana ngoma za kikorea, yaani nikicheki series zao zile soundtrack zikinibamba tu nazipakua nakuzisikiliza hata kama sielewi kinachoimbwa. Me napenda melody, sauti ya mwimbaji na beat
 
Nimefanikiwa kufika nchi kadhaa na sikuwahi kuona watu wa nchi hizo wakisikiliza au kufurahia nyimbo zilizoimbwa kwa lugha za nchi zingine wasizozijua.

Lakini hapa kwetu miaka nenda rudi tangu nakua miaka ya 70 nimekuwa nikishuhudia watu wengi wakisikiliza nyimbo za Kizungu na ukiwafuatilia hata neno moja hawajui maana yake, tena nakumbuka hii ni hadi vijijini ambapo hata salamu ya kiingereza haijui, nakumbuka wengine waliweza kukariri nyimbo yote ya Bob marley au Celine Diana.

Naona kwa nyimbo za Kongo ndio usiseme yaani ndizo zinazobamba kwenye baa na kwenye maharusi. Hata hapa ninapoandika hii mada nipo baa moja kali sana lakini mwanzo mwisho ni nyimbo za Kongo.

Kwa usomi wangu mdogo ninafikiri huenda kuna hujuma tulifanyiwa na wakoloni wetu wakatupatia dawa za kulevya ndio maana wengi tupo kama wajingawajinga sana , na wengine wapo kama mateja hivi NA NDIO MAANA NCHI HII NI RAHISI SANA KWA WATAWALA
Sasa si Bora Hilo la nyimbo ni burudani tu.. Vipi kuhusu kutugawa walivyotugawa.. Mpaka leo hii watu weusi hatuna ushirikiano na tunachukiana kupita maelezo.. Mtu anafikia kusema Bora afanikiwe mtu Baki Kuliko mtu wake wa karibu.. Mwingine mwenye kanafasi atasema ni Bora kuajiri mtu Baki Kuliko kuajiri ndugu au mtu wa karibu..

Wakati roho hizo zimetujaa Sisi ngozi nyeusi wenzetu wanaungana na kutengeneza business empires za kutisha.. Tazama waarabu wanavyobebana.. Tazama wazungu.. Tazama wachina.. Ila Sisi tunachopandikizwa ni chuki na umimi..
 
Na wanaomuomba mungu kwa ligha wasiyoijua?
 
Music ni Km lugha yake Yenyewe Yaani you feel the vibe tu and u go. Naongea Swahili na English tu lakini nyimbo za Congo zinazoimbwa na Lingala au French Nipo, Nyinbo za Spanish, Portuguese, Hindi, Korean, Italian, German, Igbo, Yoruba, Zulu, Xhosa etc nyimbo tu ikikukaa unaruka tu na sio kweli TZ peke yake nchi kibao wanasikiliza nyimbo wasizozielewa iwe India, Ulaya, Marekani. Kwani ule mwimbo wa Jerusalema uvovuma wazungu ulaya walikuwa wanajua Zulu au Xhosa? Kuna nyimbo kibao zinavuma duniani na most hawaelewi and they still love it. Angalia ile Bella Ciao from Money Heist. That's the genius of Music.
 
Sidhani kama kuna ukweli.

Muziki ni zaidi ya lugha, wengine tunavutiwa na beats,vionjo etc.

Les Mangelepa waliimba lingala tupu ila ni band pendwa tena Kenya kwa wazungu pori.
 
Ukiona mtu anasikiliza au kucheza asichokijua basi ni dalili za kuwa HAMNAZO KICHWANI
 
Nimefanikiwa kufika nchi kadhaa na sikuwahi kuona watu wa nchi hizo wakisikiliza au kufurahia nyimbo zilizoimbwa kwa lugha za nchi zingine wasizozijua.

Lakini hapa kwetu miaka nenda rudi tangu nakua miaka ya 70 nimekuwa nikishuhudia watu wengi wakisikiliza nyimbo za Kizungu na ukiwafuatilia hata neno moja hawajui maana yake, tena nakumbuka hii ni hadi vijijini ambapo hata salamu ya kiingereza haijui, nakumbuka wengine waliweza kukariri nyimbo yote ya Bob marley au Celine Diana.

Naona kwa nyimbo za Kongo ndio usiseme yaani ndizo zinazobamba kwenye baa na kwenye maharusi. Hata hapa ninapoandika hii mada nipo baa moja kali sana lakini mwanzo mwisho ni nyimbo za Kongo.

Kwa usomi wangu mdogo ninafikiri huenda kuna hujuma tulifanyiwa na wakoloni wetu wakatupatia dawa za kulevya ndio maana wengi tupo kama wajingawajinga sana , na wengine wapo kama mateja hivi NA NDIO MAANA NCHI HII NI RAHISI SANA KWA WATAWALA
Celine Diana ndo nani mkuu
 
Nasikiliza Ngoma yoyote hata ikiwa VALHALLA ilimradi melody ipo poa...

Ila tuache UONGO jumatano bar ya kitaa Kuna boa sana Kuna wana wanaimba karaoke si elewagi wale jamaa tumewakosea Nini sisi walevi.
Sipendagi huo ujinga i see
 
mjinga mjinga ni wewe koma usituchukulie poa watz unadhani kukariri ngeli kazi ndogo!?
Wewe kubali tu kuwa tunaongoza katika ujinga. Yaani ukitaka kuelewa vizuri basi mchukuwe nyani umuwekee mziki utaona anavyosikiliza na kurukaruka japo hajui kinachoimbwa. Lakini kwa Binadamu aliyekamilika hawezi kufanya hivyo, narudia kusema BINADAMU ALIYEKAMILIKA.

Na hii tabia ipo sana Tanzania. Watu wake husikiliza sana nyimbo wasizojua zinaongelea nini.
Na ndio maana wanazijua sana nyimbo za kongo ila muulize kinachoimbwa ni kipi hajui.

Nchi hii ni rahisi sana kwa watawala
 
Nimefanikiwa kufika nchi kadhaa na sikuwahi kuona watu wa nchi hizo wakisikiliza au kufurahia nyimbo zilizoimbwa kwa lugha za nchi zingine wasizozijua.

Lakini hapa kwetu miaka nenda rudi tangu nakua miaka ya 70 nimekuwa nikishuhudia watu wengi wakisikiliza nyimbo za Kizungu na ukiwafuatilia hata neno moja hawajui maana yake, tena nakumbuka hii ni hadi vijijini ambapo hata salamu ya kiingereza haijui, nakumbuka wengine waliweza kukariri nyimbo yote ya Bob marley au Celine Diana.

Naona kwa nyimbo za Kongo ndio usiseme yaani ndizo zinazobamba kwenye baa na kwenye maharusi. Hata hapa ninapoandika hii mada nipo baa moja kali sana lakini mwanzo mwisho ni nyimbo za Kongo.

Kwa usomi wangu mdogo ninafikiri huenda kuna hujuma tulifanyiwa na wakoloni wetu wakatupatia dawa za kulevya ndio maana wengi tupo kama wajingawajinga sana , na wengine wapo kama mateja hivi NA NDIO MAANA NCHI HII NI RAHISI SANA KWA WATAWALA
Nikiona show ya mondi Ethiopia,na wanamfuatisha kuimba,Zambia huko nyimbo injili za kiswahili zinapigwa club,usher Raymond alishakopi style ya kucheza ya mondi
 
Ukiona mtu anapenda wimbo ila haelewi basi beat ndo inamvutia ama kipaumbele chake.

Abaabaaa prakatatumba...huu wimbo umechezwa sana miaka michache nyuma ila hatujui hata kinaimbwa nini

Aldji aladji hatuelewi
nyimbo za koffi olomide hatuelewi na nyingine nyingi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe kubali tu kuwa tunaongoza katika ujinga. Yaani ukitaka kuelewa vizuri basi mchukuwe nyani umuwekee mziki utaona anavyosikiliza na kurukaruka japo hajui kinachoimbwa. Lakini kwa Binadamu aliyekamilika hawezi kufanya hivyo, narudia kusema BINADAMU ALIYEKAMILIKA.

Na hii tabia ipo sana Tanzania. Watu wake husikiliza sana nyimbo wasizojua zinaongelea nini.
Na ndio maana wanazijua sana nyimbo za kongo ila muulize kinachoimbwa ni kipi hajui.

Nchi hii ni rahisi sana kwa watawala
Kote ambako mondi anapiga show wanajua kiswahili!?..
 
Kwa mfano Bob Marlay ule wimbo unaitwa natural mistake inasemekana kamtukana Mungu
 
Na wanaomuomba mungu kwa ligha wasiyoijua?
Achana nao hao, wazushi tu hao. Utasikia wanaongea " kuriabarishinda, tototototo, tetetetetete, ruguria, ruguriashinda". Ukiwauliza wanasema eti wamejawa roho mtakatifu hivyo wananena lugha mpya.

Mzungu mwenyewe aliyetuletea Biblia huwa hafanyi usaniini huu.
 
Ukiona mtu anapenda wimbo ila haelewi basi beat ndo inamvutia ama kipaumbele chake.

Abaabaaa prakatatumba...huu wimbo umechezwa sana miaka michache nyuma ila hatujui hata kinaimbwa nini

Aldji aladji hatuelewi
nyimbo za koffi olomide hatuelewi na nyingine nyingi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Pia Makirikiri hatuelewi walikua wanaimba nini ila tulivutiwa jinsi walivyokua wanadance
 
Back
Top Bottom