- Thread starter
- #61
🤣🤣🤣🤣Una hoja...kina tatizo! Hivi mnakumbuka kikundincha Ngombcha Makhirikri kilivyokuja kupiga Hela Tanzania!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤣🤣🤣🤣Una hoja...kina tatizo! Hivi mnakumbuka kikundincha Ngombcha Makhirikri kilivyokuja kupiga Hela Tanzania!
Elewa tu kuwa mimi sikutaka kuukana uraia wangu. Namshukuru sana Mungu kwani nimeijua Dunia nikiwa mdogo sana bado. Hebu nenda tu Uingereza uingie restaurant yoyote uniambie utasikia nyimbo mwanzo mwisho za Kijerumani au Kifaransa au Kihindi au Kichina au Kiswahili. Ila Tanzania nenda sehemu yoyote ya Starehe utasikia mwanzo mwisho nyimbo za Kongo na Kiingereza. Ndio maana hata Brenda Fasi nyimbo zake alizoimba Kizulu zilipata umaarufu sana Tanzania kuliko nchi zingine.Mbongo akifanikiwa kwenda tunchi tuwili tena akakaa jimbo moja muda wote alokuwa huko akifanya tuvibarua twake basi anajikuta anajua kila kitu cha ulimwengu.
Kajifunze Mziki ninini kabla hujatafuta aibu ndogo ndogo kama hizi zinazoweza kuepukika.
Huyu mtoa mada mluga luga haelewi kwamba muziki ni lugha ya Dunia.
Mfano mimi naipenda hii ngoma za kizulu ila sijui maana yake.
View: https://youtu.be/YT8HMcAqLMs?si=iyDkRY1TA5wAyGfk
Usipoelewa maneno utaelewa mdundo.
Nimefanikiwa kufika nchi kadhaa na sikuwahi kuona watu wa nchi hizo wakisikiliza au kufurahia nyimbo zilizoimbwa kwa lugha za nchi zingine wasizozijua.
Lakini hapa kwetu miaka nenda rudi tangu nakua miaka ya 70 nimekuwa nikishuhudia watu wengi wakisikiliza nyimbo za Kizungu na ukiwafuatilia hata neno moja hawajui maana yake, tena nakumbuka hii ni hadi vijijini ambapo hata salamu ya kiingereza haijui, nakumbuka wengine waliweza kukariri nyimbo yote ya Bob marley au Celine Diana.
Naona kwa nyimbo za Kongo ndio usiseme yaani ndizo zinazobamba kwenye baa na kwenye maharusi. Hata hapa ninapoandika hii mada nipo baa moja kali sana lakini mwanzo mwisho ni nyimbo za Kongo.
Kwa usomi wangu mdogo ninafikiri huenda kuna hujuma tulifanyiwa na wakoloni wetu wakatupatia dawa za kulevya ndio maana wengi tupo kama wajingawajinga sana , na wengine wapo kama mateja hivi NA NDIO MAANA NCHI HII NI RAHISI SANA KWA WATAWALA
Itakua linafanana na lile la Jamaniii Dodomaaa....Kuna songi la ki Ethiopia linaitwa Serk Addis linanibamba balaa nalisikiliza sana....ila sijui hata wanaimba nini usikute songi la mazishi 🙄
View attachment 2744147
Mkuu hapa hakuna ubishi wimbo huu alipiga Marehemu Miriam Makeba wa Afrika ya Kusini na baadaye Bendi toka Jamaika ya Boney M walikuja uimba tena.Sasa kwa mleta mada atusaidie au kama alikuwa hajazaliwa basi afahamu hii pia. Kuna wimbo wa marehemu Michael Jackson unaitwa Liberian Girl kuna maneno ya kiswahili alitumia nanukuu " nakupenda pia nakuta pia mpenzi wee". Hizi ni baadhi ya nyimbo chacheUmesahau wimbo "Malaika" ulisikilizwa na kuimbwa maeneo mbali mbali duniani hata wasikojua Kiswahili