Ni Tanzania pekee kuna mgao wa Umeme kwa sasa Afrika nzima

Ni Tanzania pekee kuna mgao wa Umeme kwa sasa Afrika nzima

Hakuweza kabisa, tusidanganyane.

Mwendazake alikuta mitambo mipya kabisa ya Kikwete ya Kinyerezi I, II, III na IV na ikaanza kufa mmoja mmoja katika wakati wake. Ilikuwa inakufa inapomaliza warranty yake tu ya miaka miwili.

Mwisho ikafa yote na hakuna poesa za kuifufuwa, alifanya ujinga sana kukataa kusaini "extended warranty" na kampuni zilizofunga hiyo mitambo. "kwani Watanzania watashindwa kuisimamia" - ka sauti yake. Ndilo kosa hilo linaloitu cost mpaka leo.

Wazungu nao wamaechukuwa advantage, wanasema kuitengeneza sasa gharama zake ni kubwa sana, uamuzi ni wetu.
Mbona wakati wake hakukuwa na mgawo wa umeme...najuwa huwezi kukubali ila kimoyoni unamkubali

Ova
 
Adui wa tanesco anajulikana, ni ujinga wa Mtanzania.

Wote wanafanya makosa ya kutatuwa tatizo kwa njia zilezile zilizoshindikana kutatuwa tatizo.

Mbona utatuzi wa Tanesco ni mdogo sana, shirika likatwe vipande vipande tu, kila mkoa uwe na shirika lake la umeme.

Hapo ndipo itajulikana, mkoa unaoshindwa wanapewa watu binafsi waendeshe.

Ndani ya miezi mitatu hutosikia tena mgao wa umeme.
Hivi Kigoma kuna mgao, manake umeme wao si wa gridi ya Taifa
 
Huko kwengine duniani baada ya wenye biashara kutaka kuona ufanisi wa mashirika, kutokua na imani ya asilimia 100% na senior management kama watalinda maslahi yao.

Kwenye kulinda maslahi wakaona waunde ‘corporate code of governance’ na kuwe na ‘non executive directors’ (NED) hili kuwe na watu neutral itakayokuwa insharikishwa kwenye maamuzi ya taasisi.

NED itaongozwa na mwenyekiti (ambae atakuwa anafanya kazi kwa karibu na mkurugenzi) sifa zake lazima awe na uelewa mpana wa industry husika na ameshawahi shika senior management (hata kama ni mwajiri wa zamani kwenye hilo shirika ilimradi miaka 5 ishapita).

Idadi ya NED lazima iwe sawa na executives wa ndani ya shirika.

Majukumu ya NED yatakuwa
Kuongoza kamati ya internal control kudhibiti maamuzi yenye risks kwa operation ya shirika na kutoa risk report ya shirika mara kwa mara. Kuongoza kamati ya renumeration ya mishahara ya senior management kutokana na mapato ya shirika na kuongoza kamati ya ‘internal audit’ kuhakikisha hela inatumika vizuri na other aspects za ufanisi wa shirika na kutoa report periodically.

Kwa muktadha kutokana na majukumu ya body lazima kuwe na mtu aliebobea kwenye finance (with accepted professional accounting qualifications), unataka watu wenye track record ya risk management; wengine utajazia mwenyewe. Lakini hao watatu (mwenyekiti with industry knowledge, financier and risk management expert) vinginevyo hakuna point ya body kwa majukumu yao ya kuongoza commitee au kusimamia management.

Sasa lini umeona report ya body ya TANESCO au shirika lolote Tanzania kuhusu operation risk, internal control, internal audit report ya shirika.

This is what happens unapoteua mwenyekiti wa body ambae yeye mwenyewe clueless kwenye maswala ya umeme na NED wengine wasio na sifa za kusimamia committees muhimu za shirika.

Matokeo yake serikali haujui nini kinaendelea TANESCO wala wananchi zaidi ya kupigwa porojo tu kila siku shida ni nini.

Uwezi panda michongoma, uvune mikorosho.

Duniani watu wanafanya mambo kisayansi; tuna namna yetu ya kufikiria watanzania na kudhani duniani kote watu wanafanya mambo kama.

Halafu utasikia miaka ya 60 tulikuwa sawa na Singapore angalia walivyotuacha leo, utadhani Singapore inaendeshwa kimzaha kama Tanzania.
 
Kwamba Kenya ipo nje ya Afrika?!
Nimekuwepo Nairobi wiki nzima, mwezi huu, sijakutana na mgao, labda Kenya nyingine,Kunatokeaga Hitilafu hilo ni jambo la kawaida, Bongo kuna mgao sio hitilafu
 
Siku hizi kuna kitu kinaitwa semented grid, ni mambo madogo sana hayo.

Kila mkoa unajitegemea na grid inabaki kama ilivyo. Ni switching tu hapo zinafanya kazi, hakuna zaidi.

Tena kwa siku hizi zinaweza kuwa automated na grid ikawepo na unaelewa kabisa nani anatumia umeme kiasi gani wa kwenye grid.

Kwa kukujuza, mimi ni REngineer mstaafu niliyefanya kazi nje ya Tnzania.
“Kila mkoa unajitegemea na grid inabaki kama ilivyo”
Sasa fox ukisema unajitegemea unamaanisha nini?
Kumbuka ikiwa main grid haina kitu wewe hata ujitegemee unajitegemea kwa kipi?

Selikali ipambane kutengeneza vyanzo vya umeme
Ili grid yetu iwe na umeme mwingi kiasi kua inaweza kugawa kwa wote BILA UPUNGUFU!

Ukisema mkoa ujitegemee unajitegemea kwa umeme upi unaozalishwa kwa mkoa husika?
 
Ukitafuta taarifa za mitandaoni utabaini Tanzania ni nchi pekee yenye mgawo wa umeme kwa sasa.
Mataifa yenye upungufu wa umeme yapo mengi ila hakuna mgawo wa umeme.

Kwanini mgawo uwe Tanzania pekee na wakati huo huo viongozi wote wa kisiasa wapo wanachapa kazi na hakuna aliyetoa hotuba ya kitaifa kueleza tatizo linachangiwa na nini? Enzi za Nyuma viongozi walikuwa wanatoka adharani wanaeleza tatizo bila kurushiana mpira.leo hii ile collective accountability haipo tena kila waziri anapambana na sekta yake.

Lakini pia kwanini kila wakati umeme ukiwa na shida lazima waziri Mkuu awekwe kwenye mtego. Alikuwepo waziri wa nishati akatolewa then Zigo akapewa Naibu WAZIRI Mkuu......je ni ili wasema waziri Mkuu ndiye kafanya haya? Do they need him to grant a wish?Wanataka kufanya nini na jina la waziri Mkuu?

Chama kinalia na serikali inalia.....nani anajua kwanini tunaongoza Duniani kwa mgawo hata kipindi cha masika? Wananchi
 
Siku hizi kuna kitu kinaitwa segmented synchronous grid, ni mambo madogo sana hayo.

Kila mkoa unajitegemea na grid inabaki kama ilivyo. Ni switching tu hapo zinafanya kazi, hakuna zaidi.

Tena kwa siku hizi zinaweza kuwa automated na grid ikawepo na unaelewa kabisa nani anatumia umeme kiasi gani wa kwenye grid.

Kwa kukujuza, mimi ni Engineer mstaafu niliyefanya kazi nje ya Tanzania.
Sasa hapa,

Mimi kila nikikusoma nakuwa sielewi kabisa unamaanisha nini ulisema kila mkoa ujitemee na haya mambo ya switch.!!

Kwa tatizo ni nini, mimi nafahamu tatizo tulilonalo ni upungufu wa umeme ( hautoshi),

Hilo ndiyo la kuangalia kwanza,
Sasa tukigawa kimikoa kipindi kuna hilo tatizo ambalo hatujalitatua itasaidia.
 
Kwenye hili, kwa mara ya kwanza nakubakiana na mawazo yako.

Shirika likatwe vipabde vipabde, kwa lengo siku moja lifutwe kabisa. Umeme uzalishwe na kusambazwa na sejta binafsi tu.

Tunafahamu kabisa, kwa aina ya watu wanaokuwepo Serikalini, hasa hii serikali ya CCM hakuna chema ambacho huwa kinafanikiwa, wanachoweza ni uovu tu: ufisadi, rushwa, kudhulumu haki za watu, na wakati wote kufikiria wanavyoweza kubakia madarakani iwe kwa haki au dhuluma.
Yaani kabisa unasema twende tena kwenye sekta binafsi!!!!

Kwamba muda huu umeshasahau nini sekta binafsi ilitufanyia,!

Au kuna sekta binafsi nyingine zaidi ya akina Richmond.

Tunasahau mapema sana Watanzania
 
Sasa hapa,

Mimi kila nikikusoma nakuwa sielewi kabisa unamaanisha nini ulisema kila mkoa ujitemee na haya mambo ya switch.!!

Kwa tatizo ni nini, mimi nafahamu tatizo tulilonalo ni upungufu wa umeme ( hautoshi),

Hilo ndiyo la kuangalia kwanza,
Sasa tukigawa kimikoa kipindi kuna hilo tatizo ambalo hatujalitatua itasaidia.
Nisome tena" Kila mkoa uwe na shirika lake la umeme" hakuna mahala nimesema kila mkoa "ujitegemee".

Huna haja ya kutafsiri maneno yangu, nimeandika Kiswahili. Au Kiswahili kinakupiga chenga? Lugha mama kwako ni ipi?
 
Back
Top Bottom