Ni Tanzania pekee kuna mgao wa Umeme kwa sasa Afrika nzima

Ni Tanzania pekee kuna mgao wa Umeme kwa sasa Afrika nzima

Kukosekana kwa huduma ya umeme kunaumiza sana wananchi [emoji24]

Kunatesa sana.

Kunachosa sana.

Kunarudisha nyuma maendeleo ya uchumi.
 
Tatizo ni uongozi mbovu siyo ukubwa wa shirika
Ndiyo maana yake, uongozi hauna uwezo wa kuendesha shirika kubwa. Sasa sielewqi unachokataa nini?

Suluhisho ni shirika likatwe ili viongozi waweze kuendesha mashirika madogo madogo yaliyo ndani ya uwezo wao.
 
Adui wa tanesco anajulikana, ni ujinga wa Mtanzania.

Wote wanafanya makosa ya kutatuwa tatizo kwa njia zilezile zilizoshindikana kutatuwa tatizo.

Mbona utatuzi wa Tanesco ni mdogo sana, shirika likatwe vipande vipande tu, kila mkoa uwe na shirika lake la umeme.

Hapo ndipo itajulikana, mkoa unaoshindwa wanapewa watu binafsi waendeshe.

Ndani ya miezi mitatu hutosikia tena mgao wa umeme.
100% uko right. hii itasaidia kujua panapovuja.
 
Kwenye hili, kwa mara ya kwanza nakubakiana na mawazo yako.

Shirika likatwe vipabde vipabde, kwa lengo siku moja lifutwe kabisa. Umeme uzalishwe na kusambazwa na sejta binafsi tu.

Tunafahamu kabisa, kwa aina ya watu wanaokuwepo Serikalini, hasa hii serikali ya CCM hakuna chema ambacho huwa kinafanikiwa, wanachoweza ni uovu tu: ufisadi, rushwa, kudhulumu haki za watu, na wakati wote kufikiria wanavyoweza kubakia madarakani iwe kwa haki au dhuluma.
Wanaofanya kazi tanesco wote ni CCM?
 
Kukosekana kwa huduma ya umeme kunaumiza sana wananchi [emoji24]

Kunatesa sana.

Kunachosa sana.

Kunarudisha nyuma maendeleo ya uchumi.
Tulia bajeti ya MKUTANO WA CHIPUKIZI CCM imebana sanaa...!!hela ikipatikana tutanunua mashine
 
Kamtengua Mwenyekiti wa Bodi TANESCO kampeleka ubalozi Uganda. Umefeli hapa unapelekwa pale, tena wazee walishastaafu, wanaumwa hiki na kile, they have nothing to lose in terms of kujenga career zao kwa hiyo wanajifanyia kazi ovyo ovyo. Misrule and mismanagement of the third world.
 
Hakuweza kabisa, tusidanganyane.

Mwendazake alikuta mitambo mipya kabisa ya Kikwete ya Kinyerezi I, II, III na IV na ikaanza kufa mmoja mmoja katika wakati wake. Ilikuwa inakufa inapomaliza warranty yake tu ya miaka miwili.

Mwisho ikafa yote na hakuna poesa za kuifufuwa, alifanya ujinga sana kukataa kusaini "extended warranty" na kampuni zilizofunga hiyo mitambo. "kwani Watanzania watashindwa kuisimamia" - ka sauti yake. Ndilo kosa hilo linaloitu cost mpaka leo.

Wazungu nao wamaechukuwa advantage, wanasema kuitengeneza sasa gharama zake ni kubwa sana, uamuzi ni wetu.
Wewe Fox kumbe na wewe akili yako kama mchwa! Kikwewete ndio aliharibu kabisa hii nchi,kila sekta ilikua imeoza hadi akaja Magufuli kurekebisha. Mama nae badala ya kukabidhi hio wizara mwanzoni tu kwa wachapa kazi akaipa kiparandezi na mabeans wizara nyeti hadi hapa ilipofikia ndio kaona maji yamezidi unga kampa Dotto. Tatizo kubwa la Tanesco haliko kwenye mitambo wewe injinia wa makaratasi, tatizo lipo kwenye uongozi tu.
 
Watenganishe. Shirika la uzalishaji umeme na mashirika ya usambazaji umeme kwa kila mkoa. Vyanzo vya uzalishaji vya sasa vibaki serikalini na viyauzie mashirika ya usambazaji ya kila mkoa. Pia mashirika hayo ya mikoa yawe huru kununua umeme kutoka kwa vyanzo binafsi.

Hapo utaona watu wanavyowekeza kwenye solar farms, windfarms, geothermal na microhydro power plants. Ndani ya muda mfupi hatutasikia tena tatizo la umeme.
 
Uuuwiiii! Kuna Nchi nyingi hazina mgawo kwa vile hazina umeme. Nusu ya Kenya hains mgawo kwa sababu hains umeme. 90% ya South Africa haina mgawo kwa sababu haina umeme. Jiji la Pretoria na Durban na Johaneesburg yana mgawo wa masaa 7 kila SIKU. Where do you live?
Na Tanzania ni % ngapi maeneo hayana umeme tusitake kujifichia huko swaka la umeme TZ limekua shida yani hii kitu imeshindikana tunaharibu vitu vyetu kisa umeme kukatika hovyo,kweli nacho maskini na watu wake hawana Akili.
Nacho ilijojaa kila rasilimali lkn Hakuna maendeleo umeme Hakuna aibu tupu

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom