"Ni Tanzania tu utasikia biashara inakufa kwa sababu ina wateja wengi" Yerico Nyerere

"Ni Tanzania tu utasikia biashara inakufa kwa sababu ina wateja wengi" Yerico Nyerere

Au mahali ambapo nchi inagawa bure rasilimali zake kisha inaenda kuomba mkopo wa kununulia rasilimali hizo.

Mahali ambapo wananchi wanafurahia mikopo na misaada kuliko uwajibikaji na kujitegemea.

Mahali ambapo unazipitishia nchi zingine shehena zao kwenye bandari yako, kisha unaenda kununua bidhaa hizohizo nchini mwao. (Courtesy of Mb. Msukuma)

Mahali ambapo harakati za maendeleo zinaonekana tu sekunde chache kabla ya ngwe za uchaguzi.

Mahali ambapo serikali inakopa ili kujenga miradi ya maendeleo, kisha inaigawa kwenye mashirika binafsi yasimamie.

Mahali ambapo kura ya rais ni muhimu kuliko kula ya raia.
Inasikitisha sana.ni Tanzaa pekee unaweza kupata mambo yakusikitisha na kukera kwa wakati mmoja kama hivi.
 
Tanzania kuna kitu inaweza kuendesha basi
 
Maneno meeeeengi ishu za msingi hujazigusa
2016 nauli ya mwendokasi ilikua 650 Lita moja ya dizeli ilikua 1699,
Leo hii 2024 nauli ya mwendokasi ni 750 na Lita moja ya dizeli ni 3000+ ,

Hapa hata uwe mtaalamu wa uchumi kutoka kuzimu, lazima kampuni ife tu
Kuzimu tena?
 
Usije ukawa una digrii yako ya Tumaini University ukadhani unajua, umetembea humu duniani ukajifunza wengine wanafanyaje na kwasababu gani? Si kila kitu ni kwa ajili ya faida, vingine ni huduma, designed for public good na kupunguziq watu ukali wa maisha. Ninyi na serikali yenu ya mchongo mnashindwa kulielewa hilo ndiyo maana kila kukicha ni mauza uza.
Mambo ya huduma au kupata faida ni swala la maamuzi na mipango.Tatizo kubwa la hapa kwetu wala sio huo utaratibu unaousemea bali shida iko kwenye usimamizi.Hakuna ambacho akiwezekani kama shirika linaingiza pesa.Tatizo ni usimamizi duni,urasimu na ubadhirifu.
 
Mnapo bugi ni hapo kwenye akili za kutaka kila huduma kwa wananchi iwe biashara. Narudia tena, huko ustaarabuni tunakoiga kila kitu, makampuni pigo za mwendokasi, yanaendeshwa kwa kodi na ruzuku. Si biashara ya kuingiza faida kubwa

Mnapo bugi ni hapo kwenye akili za kutaka kila huduma kwa wananchi iwe biashara. Narudia tena, huko ustaarabuni tunakoiga kila kitu, makampuni pigo za mwendokasi, yanaendeshwa kwa kodi na ruzuku. Si biashara ya kuingiza faida kubwa.
Mkuu mazingira ya huko unakosema na hapa bongo land ni tofauti,
Sawa, usafiri wa umma ni huduma lakini Ili iwe sustainable someone has to pay for it, there is no free lunch,
Unapotaka serikali itoe subsidies maana yake unahamisha burden kutoka kwa wananchi unapeleka serikalini, ila kumbuka pia serikali zetu hizi zina ufinyu wa budget matokeo yake watalazimika kwenda kukopa Ili kuendesha nchi , sasa jiulize kipi Bora?
Nchi zilizoendelea zinaweza ku sustain kutoa subsidies kwenye mashirika Yao kwa sababu ni tayari zinajitosheleza kifedha.
Utofauti huo wa mazingira unalazimisha mashirika yetu yajitahidi yajiendeshe yenyewe Ili yasife
 
Hapo ndipo mnapokosea, kununua ma SUV ya milioni 400/piece ni sawa, lakini kununua mabasi ni free lunch? Halafu una shangaa kwanini nchi haina maendeleo!
Chief mbona sasa unahamisha goli haha
 
Nimehamisha goli vipi, umesema serikali haina pesa blah blah blah, miye bila kutumia maneno mengi, nimekujibu kwa kuonyesha pesa ipo tatizo ni priorities. Ni wazi kuwa uwezo wako wa kuelewa, ile critical thinking haipo vizuri 😃. Ulitaka niandike gazeti kama wewe?
Sina tena neno kwako mwenyekiti wa "critical thinking"
 
"Unaweza usiamini kwamba ni Tanzania tu inatokea kwa mara ya kwanza duniani, kwamba biashara inakufa kwa sababu ina wateja wengi. Yes amini Mwendokasi inakufa huku ongezeko la wateja ni kubwa sana na haina mpinzani ni wao tu Dar nzima. Hivi sisi ni akina nani? sisi ni MANYANI" Anasema Yerico Nyerere.

Sio tu wana wateja wengi, wametengenezewa barabara zao, wamepewa sehemu bure za garage na maghala na parkings, wameongezewa roots nyingine kama sita tena root zenye wateja wengi balaa mpaka za mbaghala, wamepewa vituo vyao vya kukatia ticketi , kupakia na kushusha abilia.

😒Tena unaweza kuambiwa walipewa au wanapewa excemption kwenye baadhi ya kodi na kuingiza mabasi na vipuri. Kibaya wanawateja mpaka inakinaisha, wateja ni wengi kuliko mabasi yao yote.Sasa hawa watu biashara yao imewezaje kufa, katumia neno labda sisi ni MANYANI, akimaanisha ni kama wanyama wa msituni,hilo ni swali la kujiuliza tufanye nini turudi kuwa binadamu na si Tumbili, nyani sokwe???

Mimi nilikuwa najiuliza swali kama hilohilo lakini kwenye sekta ya Afya hasa kuhusu Bima ya afya ya Taifa (NHIF). Hivi NHIF inawezaje kupata hasara wakati inaoperate kama COMPREHENSIVE group insurance ila yenyewe ikiwa na advantage ya kuwa na group la wafanyakazi wa serikali wa nchi nzima. Kibaya wao ndio wanadetermine type of services to offer, amount to pay for providers of services and when to pay them na hawana hofu ya competetion kwani wako peke yao tu kwa wafanyakazi wa serikali. Nakwambia ni kituko cha dunia kwa wale wanaoelewa mambo ya individual na global health insurance system.

Kwa normal private health insurance, wao ni kinyume, wanatafuta wateja, wanatakiwa na kulazimika kuoffer better hospitals and services na kulipa watoa huduma vizuri na timely kwani wanaweza kukosa wateja na kampuni ikafa.

Conversely, group health insurance nyingi za kawaida kama za wafanyakazi wa masupermarkets, labda mashirika ya umma, wafanyakazi wa masoko fulani mara nyingi hata premium zao (michango) ni za chini kwa sababu wanaserve groups, kwa hiyo wako 100% sure kila mwezi wataingiza malipo ya wateja wao wa kwenye group na kiasi gani na ni wengi kidogo.

Sasa cha kushangaza na kusikitisha NHIF ya Tanzania ni tofauti na other normal group health insurance, hawa si group health insurance ya kawaida bali ni National Group Health Insurance, wana kundi kubwa la mamilioni ya wafanyakazi nchi nzima ambao kila mwezi wanakatwa divident toka kwenye mishahara yao na hela inaingia moja kwa moja NHIF;utafiti umeonyesha zaidi ya asilimia 80% ya wafanyakazi wanaweza kukaa miezi zaidi ya sita bila kutumia any of the NHIF insurance, tena wengine wanatumia cash kuliko card za NHIF kwa sababu ya kadhia zake, mimi nilikaa miaka 6 nikaitumia mara 2 tu. Thus, the estimated expected marginal profit of NHIF kwa mwezi ni kama mara 300% ya other normal group health insurance na more than 500% ya normal health insurance companies/firms

Halafu leo unaambiwa NHIF wako ICU kifedha kwa hiyo wanaondoa Baadhi ya huduma na dawa. Pathetic. Nakubaliana na Yerico sisi hatutofautiani na Manyani na tumbili, wanyama wa msituni. Swali tufanye nini tutoke huku msituni kwenye giza turudi kwenye mwanga ,tuishi kama binadamu wengine na si kama wanyama?
Tatizo letu sisi ni kwamba Wanasiasa ndiyo wenye Mamlaka ya kufanya maamuzi yaliyopaswa kufanywa na Wataalam wa Sekta husika..
 
Sina tena neno kwako mwenyekiti wa "critical thinking"
Ahaaaa nimependa discussion hii na jinsi watu wanavyopangua hoja, kuhamisha hoja na kumake a case kiutaalamu na kiustaharabu. Na hii ndio dhana nzima ya "critical thinking". Jamani tulikubaliana hii ni free discussion hakuna hoja mbovu, hakuna hoja iliyokosewa bali zote ni hoja.
 
Back
Top Bottom