Kabisa hilo naamini maana tulikuwa karibu sana. Natamani ningepata hata dk 5 tu naye za maongezi. Na nilipoambiwa kapata ajali sikudhani inaweza kuwa serious ya kuchukua uhai maana ilikua ni safari ndani ya jiji tu. Tulikuwa tumeachana nae si zaidi ya masaa mawili na ilikuwa tuonane nae tena baadae jioni.nilivopigiwa kapata ajali Zaidi nilijua ni kwenda kumsaidia ishu za polisi na nini. Ila baada ya kufika hospital na kumkuta anafanyiwa CPR hapo kwa kweli magoti yaliishiwa nguvu. Wote waliokuwa mahututi kwenye ajali yake walipona isipokuwa yeye tu ambaye mashuhuda wanasema ndio ana fadhali kwa kuwa alionekana hajaumia kwa nje.