Elections 2015 Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)

Ndo maana jk alivyoenda kwenye kampeni 2010 kijiji kwa Tundu Lissu alisema ni bora yeye anyimwe kura kuliko kumpa kura TL ila wampe mgombea wa CCM
sasa nimejua dhana yake.
Nakushukuru mleta mada kwa uchambuzi murua.
 
Naunga mkono mia ya mia juu ya sifa ulizoziainisha hapo juu, lakini napata tatizo kidogo huyu jamaa kakaa kiuanarakati zaidi sasa apatapo hiyo nafasi diplomasia ya nchi yetu yaweza shuka mno.

Napenda nitoe wazo, kama UKAWA/CHADEMA wakipata nafasi ya kuchukua dola wampatie nafasi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali, kulingana na elimu yake aliyonayo. huku ataweza kung'oa visiki vyote vilivyopata kujijenga miaka 50 baada ya uhuru.

Natoa wazo tuuu.....!
 
Alafu lissu atashindwa kuulinda Muungano, ni bora ya Kikwete. Mtazamo wa Lissu juu ya Muungano wetu ni hasi sana.

Mkuu...huu MUUNGANO tulionao sasa umeleta tija gani? au nihiyo CCM wanasema tumeoleana....!! Cdhani km kuna mtu timamu hataki muungano kinachotakiwa kuufomati huu muungano tulionao....
 

Hapa watu wanaongea vitu halis wee unaleta zakufikirika....Kwahiyo hao jamaa wa maGAMBA watahama chama chao...halafu huyo magufuri unamjua vzr? au unaona porojo anazomwaga hadharani tu....!!
 



Ikishafikia hatua hiyo ndo nguvu ya UMA inatakiwa ionekane...Piga KURA linda KURA....! Lazima mshindi halali atangazwe
 
....mkuu hakika mtu huyu ni wa kumsimamia na kumpigania kwa nguvu zote ili siku moja atuongoze.....Inasikitisha sana kiwango cha kuptoka kwa maadili ya viongozi katika TZ ya leo....Inasikitisha zaidi pale tunapoona hata wale wanaoaminiwa na jamii (kama viongozi wa dini)wanashiriki katika kulitafuna taifa..hakika taifa hili linahitaji mkombozi atakaeonyesha njia kwa tabaka zote za kijamii...Mimi siku hizi hata viongozi wa dini ninapima kauli zao...maana hawaaminiki wengine....

...Ndio maana nasema tunahitaji mtu kiongozi msafi asiye na doa katika taifa hili ili awe kioo cha jamii nzima....Kwa kuanzia hapo ndipo mabadiliko ya kweli yataanza kwa nchi hii.....Na mtu huyu namwona ni Lissu katika TZ ya leo....maana amejidhihirisha pasi na shaka kwa matendo na kauli zake.....ndio maana wanamwogopa na kumchukia wale walio wachafu....

...Labda kwa reference tu kwa wasomaji humu...someni makala hii chini toka kwa mtu makini(msomi)...ili mjue tunayosema yanasemwa pia na wasomi..

...Raia Mwema - Kujitoa ndani ya virusi vya kimfumo, anahitajika mtu
 
Mkuu JokaKuu thread hii haimaanishi slaa ni mbaya.Hapa najaribu kuionesha jamii kwamba kuna alternative dhidi ya ccm.
Hata Dr Slaa atakubaliana na mimi katika hili.
Hii ni thread maalum kwa UKAWA kujipanga na kuweza kuchukua dola.

...wazi kabisa....Labda zaidi angalizo muhimu kwa UKAWA..haswa viongozi wao wa juu ni kutokua wabinafsi....na pia kuwa flexible kwenye kuchagua wagombea wao wa urais bara na visiwani....

...Kwa ushauri tu...ningependa sana kuona wazee makini kama kina Dr.Slaa na Prof.Lipumba wanagombea ubunge katika majimbo hata ya hapa dar ili waingie bungeni(mfano wagombee kupitia K'ndoni ama Ilala/temeke)...na nina hakika wakifanya hivyo watapita...na wakiwa bungeni wataongeza viti upinzani na pia watapata nafasi za juu za uongozi wa taifa hili pale UKAWA watakapopata dola....Tukumbuke pia kuna nafasi nyeti kama ya waziri mkuu..ama waziri wa fedha ambazo zimetumika vibaya na zimechangia sana kuliangamiza taifa hili na hivyo zinahitaji watu makini kama wazee hawa....

...Pia viongozi wa UKAWA watambue kuwa sasa hivi wapiga kura wengi wa taifa hili ni vijana na wataangalia sana ni vijana gani watapitishwa kugombea nafasi hizi za juu...Na kwa maana hiyo uteuzi wa mtu kama Lissu ni muafaka sana kwa wakati huu tete....

....Tunapojadili teuzi hii ya urais tusisahau pia kule Zenj....maana nako ni sehemu ya taifa hili..hivyo suala la mgombea mwenza kwa mtu kama Lissu nalo ni muhimu kulijadili....Na kwa muono wangu mtu makini naeona angegombea kwa mafanikio makubwa na Lissu(kama ikitokea hivyo)ni yule kijana makini Ismail Jussa...vijana hawa walionyesha umahiri mkubwa katika bunge la katiba katika kupigania hoja zao....hawa jamaa ni vichwa na hadhina kubwa ya TZ....

...Kwa urais wa zenj....Mkuu Maalim Seif anawaweza kabisa ccm..maana hata urais wa 2010 alishinda yeye na akapokwa urais na ccm kwa hila.....


...Mwisho....NI vema sana UKAWA wakawa makini na kupokea mafisadi/wagombea urais watakaotoswa huko ccm....Hawa hawafai UKAWA kama kweli wanataka kujenga imani kwa watanzania....Wasiwakubali kabisa kabisa mafisadi watakaotemwa ccm....maana hata sasa UKAWA wamefika hapa bila hao mafisadi...Ila ni vema pia UKAWA wakawa open kuwapokea watu makini watakaotemwa kwa hila huko ccm....maana wapo watu makini(wachache)ccm ambao huko ccm hawapendwi kwa misimamo yao na wanaweza kutemwa kwa hila....mfano kama ilivyokua kwa kina Mansour Himidi...
 
Kiukweli mleta maada umelenga mtu ambaye anafit kotekote. Ujana, upambanaji, na uzalendo pia. Naiona kanani ileee tukiongozwa Tundu Lisu. Hatuto sikia tena mirindimo ya ujana toka upande wa pili maana tutakuwa tumewapiga bao la tobo.
 
Naunga mkono hoja lakini tundu sio president material tumuweke kwenye utendaji
 
Naunga mkono hoja lakini tundu sio president material tumuweke kwenye utendaji
..zipi qualities za president material kwa mtazamo wako??..Unamaanisha nini unaposema kumweka kwenye utendaji??..na kwanini unafikiri iwe hivi??...Naomba unitofautishie urais na utendaji wa mtu....
 
..zipi qualities za president material kwa mtazamo wako??..Unamaanisha nini unaposema kumweka kwenye utendaji??..na kwanini unafikiri iwe hivi??...Naomba unitofautishie urais na utendaji wa mtu....

Anaweza kabisa kuwa kiongozi wa taifa hili tena akaliongoza kwa ufanisi mkubwa kabisa, Lakini kwa nature ya kiongozi anayetakiwa kwa miaka ya 2015 to 2020 ni kiongozi who can make very hard decision in very high wisdom, kiongozi wa kufanya maamuzi katika hekima ya juu sana

Tundu lisu ni mtendaji na kiongozi mzuri sana na anaweza kabisa kusimama kwa hiyo position na kufanya mabdiliko but nikiangalia nafasi kama ya mwansheria mkuu he can perform zaidi na zaidi
 
 

Mkuu nimesoma na kuridhika na uchambuzi wa mwandishi huyu ingawa hakumchukuli TL kwa uzito.
 
Naunga mkono hoja lakini tundu sio president material tumuweke kwenye utendaji

Kinachohitajika kwa sasa ni utendaji na sio upresidential material.thats where n when TL comes in.
 
Mkuu nimesoma na kuridhika na uchambuzi wa mwandishi huyu ingawa hakumchukuli TL kwa uzito.
..ni kweli hajamtaja mtu..ila anamzungumzia mtu anayetakiwa na taifa hili....sifa ambazo ukianisha anazo mh.Lissu....Dhana ya uchambuzi wake si kumtaja mtu bali kuainisha aina ya mtu anaetakiwa kwa taifa hili kutuvusha kwenye mkwamo huu wa kimaadili na kimfumo...
 
...kuna dhana potofu sana iliojengeka kwa watanzania pale wanapohusisha hekima na umri/uzee wa viongozi wetu...hii mi naona ni dhana potofu sana..na mara nyingine ni upungufu unaotumiwa sana na wale wanaogombea wakiwa wazee kama hoja ya kushinda....

...dhana ya uzee kama hoja/kigezo cha kuchagua rais ni potofu sana..na haina uhusiano wowote na maamuzi ya hekima ya rais mzee....Ingekua hivi ndivyo basi TZ ya leo isingekuwa hapa ilipo leo......

...Lazima tunaposema hili tuwe na mifano pia....wenzetu majirani Kenya wamefanya maamuzi magumu na sahihi pale walipomchagua rais kijana (Uhuru) na matunda yake wameanza kuyaona....Uhuru alimshinda Raila aliyekuwa na umri mkubwa kumzidi....Hata Rwanda walimpa urais Kagame akiwa kijana tu...lakini angalia alichoifanyia Rwanda....


..Tz ya leo inahitaji rais mwenye nguvu na maono na maamuzi magumu...ili kuonyesha njia...maana bila kufanya hivyo hatutoki hapa tulipo....Tz haiitaji rais ambaye baada ya kuchaguliwa ataanza kushinda akienda ulaya na marekani kwa matibabu na kuacha kushughulikia changamoto zinazoua taifa hili....hatuitaji mtu wa namna hii TZ....maana kuna wanaowania urais sasa ambao naskia hata kufunga kamba za viatu vyao hawawezi...eti nao wanataka waje watutawale....ili wazidi kundelea kutafuna kodi zetu kwa safari za matibabu nje kila kukicha...hatuwataki watu wa namna hii wagonjwa....
 
CHADEMA msije mkafanya kosa la kumsimamisha mgombea mwingine zaidi ya Lissu kwasababu,Kwa mfano Dr Slaa anaweza kiongozi mzuri sana wa nchi hii lakini tatizo linakuja je anachagulika?Tayari inajulikana kabisa Dr Slaa anaweza kuzikosa kura za Watanzania wa imani nyingine.Ni dhahiri hakuna atakaueweza kushinda urais kwa kutegemea kura za watu wa imani moja tu.Hapo ndipo Tundu Lissu anapotokea kuwa mgombea salama kidogo kwani misimamo yake ya kisiasa imetokea kuwakuna Watanzania wa imani nyingine pia hivyo ana uhakika wa kupata kura kutoka upande huo pia.Lissu ni kijana na ni msomi anaweza kuwavutia vijana wengi kwenda kupiga kura kwa wingi.Lissu ana mwonekano hii inaweza kumsaidia kupata kura za wanawake pia.Fikiria CCM wakimsimamisha Pinda kama mgombea wao wa urais na UKAWA wakamsimamisha Lissu nini kitatokea.
 

Well said, tundu lisu ni mtendaji, hupaswi kugombea uraisi. Uraisi bado slaa anafaa kwasasa

Tundu lissu akitumika kama mtendaji katika serikali kutakuwa na ufanisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…