Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alafu lissu atashindwa kuulinda Muungano, ni bora ya Kikwete. Mtazamo wa Lissu juu ya Muungano wetu ni hasi sana.
Tundu Lissu anafaa sana kuwa AG au waziri wa sheria, atatufaa sana akiwa chini ya Rais Mhe. Dr. John Magufuli. hapo nchi itakaa sawa, ni mchakamchaka. wezi wote jela na fedha zote kurudishwa. Mhe, Mwigulu Apandishwe kuwa waziri kamili wa fedha, Prof, Lipumba awe Gavana BOT, na Dr. Slaa awe PM,
Mkuu meningitis kushinda sio kazi kwa Lisu kazi ni kutangazwa kashinda ndio haitatokea mbele ya masisi em.na hakuna kitakachotokea tena nasema ukawa hawana haja ya kupiga kampeni za nguvu sana naamini Watanzania watawachagua ila ila kutangazwa washindi ndicho hakitatokea chakufanya mapema mikakati ya kulinda kura iandaliwe na mbinu zingine.
....mkuu hakika mtu huyu ni wa kumsimamia na kumpigania kwa nguvu zote ili siku moja atuongoze.....Inasikitisha sana kiwango cha kuptoka kwa maadili ya viongozi katika TZ ya leo....Inasikitisha zaidi pale tunapoona hata wale wanaoaminiwa na jamii (kama viongozi wa dini)wanashiriki katika kulitafuna taifa..hakika taifa hili linahitaji mkombozi atakaeonyesha njia kwa tabaka zote za kijamii...Mimi siku hizi hata viongozi wa dini ninapima kauli zao...maana hawaaminiki wengine....Umuhimu wa kumchambua TL katika kipindi hiki ni kutokana na wimbi la wasaka tonge waliolipwa kuwapigia debe wagombea wale wale wenye sera zile zile na haiba zile zile za tabaka lile lile lililotufikisha hapa.
Rushwa na ufisadi ndio imekuwa tiketi wya kutuchagulia viongozi.
wananchi,wanachama wa vyama vya kisiasa,waandishi na viongozi wa kidini au jadi wanahongwa kuwapigia debe viongozi wabovu na matokeo yake Taifa linaangamia!
Wazalendo wa kweli wa Taifa hili tusimame na kulitetea kwa kuwa madhara ya viongozi wabovu yatatukumba.
say yes to TL and say ney to mafisadi.
Kwako nderingosha
Mkuu JokaKuu thread hii haimaanishi slaa ni mbaya.Hapa najaribu kuionesha jamii kwamba kuna alternative dhidi ya ccm.
Hata Dr Slaa atakubaliana na mimi katika hili.
Hii ni thread maalum kwa UKAWA kujipanga na kuweza kuchukua dola.
..zipi qualities za president material kwa mtazamo wako??..Unamaanisha nini unaposema kumweka kwenye utendaji??..na kwanini unafikiri iwe hivi??...Naomba unitofautishie urais na utendaji wa mtu....Naunga mkono hoja lakini tundu sio president material tumuweke kwenye utendaji
..zipi qualities za president material kwa mtazamo wako??..Unamaanisha nini unaposema kumweka kwenye utendaji??..na kwanini unafikiri iwe hivi??...Naomba unitofautishie urais na utendaji wa mtu....
Wanajamvi habarini!
Niliweka post hivi majuzi na kuahidi kurudi tena na kuelezea kwa nini nimeamua kushawishi umma wa Tanzania ya kwamba TANZANIA ya leo inamuhitaji Tundu Lissu kama mwajiriwa mkuu wa wananchi.
wakati umefika na wakati ndio huu!
Utangulizi:
Nikijikita katika mada moja kwa moja napenda kusema kuwa Tanzania ya leo sio Tanzania ya Nyerere,hapa namaanisha sio Tanzania yenye maadui watatu yaani Ujinga,Umasikini na Maradhi...maadui hawa walishadhibitiwa usiniulize lini au na nani bali tulie tuelezane.
Watanzania wa leo wana elimu bwana...watu wanatumia simu,TV na teknolojia za kigeni bila shida.elimu ya msingi kwa sasa ni kidato cha nne,maelfu kwa maelfu ya vijana wako vyuo vikuu.hivyo sitarajii kumsikia mtu akilalamika juu ya watanzania kupata elimu iwe bora au hiyo hiyo ya kuungaunga...Adui alikuwa ni upatikanaji wa elimu na sio ubora wake!!!
Swali la kujiuliza jee elimu hii wanayopata vijana wetu hasa ile asilimia 75 ya wakulima na labda kwa kuongezea asilimia 10 ya wafugaji inafanana na ile wanayopata asilimia chini ya kumi ya tabaka la viongozi/masingasinga na washirika wao?
Hivi hii elimu waliyopewa watoto wa mbwa imelenga kuajiriwa au kujiajiri?
Watanzania wa leo sio maskini bwana.mabarabara ya lami kila kona,umeme vijijini wa kuwasha taa tu(wanakijiji wataanza kuchelewa kulala).Watu wanamiliki simu,toyo na mafundi cherehani wa sikuhizi hawajui kuweka viraka.Ukiongelea msosi hii sio issue tena kwani siku hizi hakuna kupanga foleni ya mkate huku kuna skonzi za Azam.
Umasikini hakuna tena...naam
Watanzania wa leo hawaumwi kipindupindu,Ukoma,vikope n.k watanzania wa leo wanaumwa dengue,B.P na rare cases kansa ya Tezi....
Isitoshe kuna zahanati au kituo cha kutoa huduma za afya kila kijiji.Adui alikuwa ni upatikanaji wa huduma za afya sasa zipo.
Jiulize sasa huduma hizi za hospitali hata ile zahanati kuu ya Muhimbili zinakujia kwa hisani ya nani?Jibu lako kaa nalo.
Wakuu msichoke naendelea na utangulizi.
ADUI WA TAIFA HILI NI YUPI HASWA KWA SASA??
Kabla sijamtaja ningependa kusema kuwa inawezekana miaka yote tuliyofanya uchaguzi hatukuwahi kuwa na ajenda kama taifa bali tuliendelea kuimbishwa kama kasuku kuhusu maadui hawa watatu.Sasa
ni wakati muafaka tukaingia kwenye uchaguzi huu tukiwa na ajenda ya pamoja.
Adui pekee aliyebaki Tanzania ni UFISADI...yaani huyu ndiye kubwa la maadui .Hata hayati JKN hakustuka au aliunderestimate uwezo wa Adui hili na ndio maana leo hii limekuwa kubwa la maadui.
Tanzania ya leo inakwamishwa na Ufisadi ama mfumo na mtandao wa kifisadi unaokuwa kwa kasi.....
Vijana wanakosa mikopo ya kusoma vyuo vikuu mpaka wanasingizia wazazi wao ni vilema au wafu ili tu wapate mkopo ilihali kuna mafisadi wamehifadhi vijisenti uswisi.
Madawa yanakosekana katika zile zahanati za kila kijiji ikiwemo ile zahanati kuu kisa ni madeni au labda watu wanataka kujipigia 10%
Kwa ufupi ufisadi ni janga janga janga la kitaifa kwani hata umeanza kujidhihirisha makanisani.
Tunahitaji kuwawajibisha,kuwachukia na ikiwezekana kuwapoteza.
Kazi hii hahitaji mtu legelege bali mwenye dhamira na tabia isiyokoma ya kuwa na misimamo isiyoyumba....Hii ndio SABABU MOJA YA KUMPA LISSU KIJITI KWA TIKETI YA UKAWA.
Tunapomkabidhi Mama Tanzania tumwambie kazi yako ni moja tu ya kutuondolea ufisadi na mafisadi.
Kama ni viongozi tunao tunachohitaji ni kuwaondoa viongozi wenye nasaba za kifisadi.
Kama ni madaktari au waalimu au majaji wapo na tutaendelea kuwapata lakini tunahitaji kusafisha watumishi wote wenye genes za kifisadi.
Hatuna uhaba wa maafisa ugavi au wahasibu wanaoshiriki ufisadi tunahitaji kuzalisha wagavi au wahasibu waadilifu n.k n.k
SIFA KUMI ZA TUNDU LISSU KWA MUKTADHA WA HOJA HII
1-Tundu Lissu ni mkweli kwa kimombo yuko Honest.mara nyingi hujiweka wazi katika misimamo yake na hivyo kuwafanya wake kumuelewa na wao kuamua au kuchukua upande.Kijiko hukiita kijiko na sio beleshi dogo!
2-Maono/Malengo yaliyonyooka ama kwa kimombo niseme anaweza kufocus.
Kama uliwahi kumsikiliza bungeni basi utajua hajaikosa hii tabia kwani hata panapotokea distractions kama vile kutukanwa basi yeye hubaki katika mstari na kuendelea kukifafanua au kukifikia kile anachotaka.
3-Heshima kwa utu.Toka mwanzo wa siasa/harakati Tundu lissu amejikuta akipambania utu wa mwanadamu,rejea harakati za migodini.
4-Uwezo wa kujenga hoja na kushawishi.
Hili ni jambo muhimu kwani ukienda Zanzibar Tundu Lissu ameweza kuwavutia wazanzibar mpaka kupachikwa jina la Messi wa Ukawa.Naweza kusema hakuna kiongozi kutoka bara tena mkiristo anayeweza kuwa na ushawishi kwa upande wa zanzibar isipokuwa TL.iwe ndani au nje ya UKAWA.
Na hii ndio turufu muhimu kwa UKAWA kwa wakati huu.
5-Ujasiri
Tundu lissu hajawahi kuogopa especially kuwaogopa mafisadi.
6-Ujuvi au labda kwa lugha ya malkia niite Arrogance.Arrogance ni tabia isiyopendwa na wengi lakini Tabia hii ndio inayohitajika pindi unapopewa kazi ya kipambana na mafisadi papa na watumishi wajuaji.
pia ni sifa hii inayohitajika pale utakapokutana na mataifa makubwa yanayotaka kunyakua rasilimali za nchi hii.
7-Ni kijana na bado ni mkakamavu.
8-Ni mwanasheria nguli anayejua kucheza na sheria na hiki ndio kiama cha mafisadi kwani watafilisika kwa kukodi mawakili wa kupambana na Rais mwenye dhamira ya kuwanyoosha.
9-Ameishi na kukulia katika umasikini.Amekumbana na kuchukia dhahma za kuchangishwa michango ya kipuuzi huku kodi zikiliwa na mafisadi.
10-Anajifunza na kucope na mazingira kwa haraka.Uwepo wake ndani ya bunge baada ya Dr Slaa kuondoka umekuwa ni chachu ya mabadiliko nchini.
Nimalize kwa kusema kuwa Tundu Antiphas Mughwai Lissu ni aina ya kiongozi anayehitajika kwa sasa.
Tuungane kutokomeza ufisadi!!![/QUOTE
Ingelifaa Kuwa WAZIRI MKUU na si RAISI.Kwa structure ya Mumford wetu,WAZIRI Mkuu Ndiye mtendaji mkuu.Ndo mana ni Mnadhalimu Mkuu bungeni.
....mkuu hakika mtu huyu ni wa kumsimamia na kumpigania kwa nguvu zote ili siku moja atuongoze.....Inasikitisha sana kiwango cha kuptoka kwa maadili ya viongozi katika TZ ya leo....Inasikitisha zaidi pale tunapoona hata wale wanaoaminiwa na jamii (kama viongozi wa dini)wanashiriki katika kulitafuna taifa..hakika taifa hili linahitaji mkombozi atakaeonyesha njia kwa tabaka zote za kijamii...Mimi siku hizi hata viongozi wa dini ninapima kauli zao...maana hawaaminiki wengine....
...Ndio maana nasema tunahitaji mtu kiongozi msafi asiye na doa katika taifa hili ili awe kioo cha jamii nzima....Kwa kuanzia hapo ndipo mabadiliko ya kweli yataanza kwa nchi hii.....Na mtu huyu namwona ni Lissu katika TZ ya leo....maana amejidhihirisha pasi na shaka kwa matendo na kauli zake.....ndio maana wanamwogopa na kumchukia wale walio wachafu....
...Labda kwa reference tu kwa wasomaji humu...someni makala hii chini toka kwa mtu makini(msomi)...ili mjue tunayosema yanasemwa pia na wasomi..
...Raia Mwema - Kujitoa ndani ya virusi vya kimfumo, anahitajika mtu
Naunga mkono hoja lakini tundu sio president material tumuweke kwenye utendaji
..ni kweli hajamtaja mtu..ila anamzungumzia mtu anayetakiwa na taifa hili....sifa ambazo ukianisha anazo mh.Lissu....Dhana ya uchambuzi wake si kumtaja mtu bali kuainisha aina ya mtu anaetakiwa kwa taifa hili kutuvusha kwenye mkwamo huu wa kimaadili na kimfumo...Mkuu nimesoma na kuridhika na uchambuzi wa mwandishi huyu ingawa hakumchukuli TL kwa uzito.
...kuna dhana potofu sana iliojengeka kwa watanzania pale wanapohusisha hekima na umri/uzee wa viongozi wetu...hii mi naona ni dhana potofu sana..na mara nyingine ni upungufu unaotumiwa sana na wale wanaogombea wakiwa wazee kama hoja ya kushinda....Anaweza kabisa kuwa kiongozi wa taifa hili tena akaliongoza kwa ufanisi mkubwa kabisa, Lakini kwa nature ya kiongozi anayetakiwa kwa miaka ya 2015 to 2020 ni kiongozi who can make very hard decision in very high wisdom, kiongozi wa kufanya maamuzi katika hekima ya juu sana
Tundu lisu ni mtendaji na kiongozi mzuri sana na anaweza kabisa kusimama kwa hiyo position na kufanya mabdiliko but nikiangalia nafasi kama ya mwansheria mkuu he can perform zaidi na zaidi
Anaweza kabisa kuwa kiongozi wa taifa hili tena akaliongoza kwa ufanisi mkubwa kabisa, Lakini kwa nature ya kiongozi anayetakiwa kwa miaka ya 2015 to 2020 ni kiongozi who can make very hard decision in very high wisdom, kiongozi wa kufanya maamuzi katika hekima ya juu sana
Tundu lisu ni mtendaji na kiongozi mzuri sana na anaweza kabisa kusimama kwa hiyo position na kufanya mabdiliko but nikiangalia nafasi kama ya mwansheria mkuu he can perform zaidi na zaidi