Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Kama kweli ulisomea sheria na argument yako ndiyo hii basi ulikuwa kilaza mkubwa na hadi leo umebaki kuwa hivyo! Pamoja na kujitutumua sana lakini watu wameendelea kukupuuza hata ndani ya chama chako.Wanabodi,
Kwanza sio kila kitu ni siasa, vitu vingine ni hoja za kikatiba, Sheria, taratibu na kanuni.
Ukileta hoja specific, hakuna ubaya kujifagilia ubobezi wako katika eneo husika.
Mimi Paskali Mayalla ni Mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea, ila pia nilisomea sheria, LL.B, UDSM, ile kutua tuu UDSM, siku ya kwanza kipindi cha Kwanza ni LW 101, unajua mwalimu wangu wa kwanza kabisa UDSM ni nani?... ni Dr. Tulia Akson!.
Prof. Issa Gulamhussein Shivji na Palamagamba Kabudi, walitufundisha LW. 200 ndio yenye Katiba, nilifumua A, utadhani mtihani nilikuwa natunga mimi!. Hivyo kwenye hoja hii ya Katiba ya Chadema, mimi naizungumza as an authority.
Katiba ni kakitabu kadogo tuu, ila kukaelewa ni shughuli. Kabla ya chama chochote cha siasa kusajiliwa ni lazima kiwasilishe katiba yake kwa Msajili wa vyama, ipitiwe na wataalamu wa katiba, wajiridhishe kuwa iko sawa na inaendana na katiba ya nchi.
Hivyo hata Chadema, iliposajiliwa kwa mara ya kwanza ile 1992, iliwasilisha katiba fulani amaizing iliyokuwa nzuri kabisa, yenye kipengele cha ukomo wa uongozi mwisho ni vipindi viwili vya miaka 5 na mwanachama wa Chadema alikuwa huru kuitafuta haki yake mahakamani.
Mwaka 2006, Chadema wakafanya marekebisho ya Katiba na kuyasilisha ofisi ya msajili wa vyama, na ikakubaliwa.
Nilipoipitia katiba hiyo ya Chadema ya 2006, nikakuta kile kipengele cha ukomo wa uongozi, hakipo!, kimenyofolewa kinyemela!. Nilipokiulizia kipengele hicho humu jf, Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Slaa alinishukikia vilivyo na kukanusha kuwa Chadema halikuwahi kuwa na kipengele hicho!.
Hii maana yake ni hata Katibu Mkuu Chadema, alikuwa haijui Katiba ya chama chake!. Kama Katibu Mkuu ambaye ndie custodian wa katiba ya Chadema, haijui katiba hiyo, what do expect kwa the rest of the people?.
Baada ya Dr. Slaa kunishukia, aliyeninusuru ni JJ. Mnyika kukiri kifungu hicho kilikuwepo na sasa hakipo sio kuwa kimenyofolewa!, no!, bali ni hakikujadiliwa kabisa hivyo kikayeyuka tuu into thin air!
Katiba hiyo ya 2006 pia ikapenyeza kifungu ambacho kinakwenda kinyume cha katiba ya JMT kumzuia mwanachama wa Chadema kwenda mahakamani, akienda tuu ndio amejifukuzisha Chadema!.
Tukija kwenye hoja za bandiko hili ambazo mimi nimeziita Chadema ni ubatili, ubatili ubatili mtupu mpaka basi!. CC ya CDM haina mamlaka kumjadili Mwenyekiti wa Bawacha, kwasababu sio mamlaka yake ya nidhamu, CC hiyo ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumjadili na kumfuta uanachama Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee?!.
Mamlaka sahihi ya nidhamu ya Mwenyekiti wa Bawacha ni Baraza Kuu, kwenye kikao cha juzi cha Baraza Kuu la Chadema, kuna mtu yoyote alisikia likijadil mashitaka yoyote ya Halima Mdee?. Ilichofanya Baraza Kuu ni kubariki maamuzi yale batili ya CC ya Chadema. Kitendo cha Baraza Kuu, kurudhia kuvuliwa uanachama wa Halima Mdee, Baraza Kuu lilipata wapi mamlaka hiyo?!.
Katiba ya Chadema ipo na imeweka taratibu na kanuni za mamlaka ya nidhamu, kwanini hazifuatwi?. Sasa vitu vidogo tuu na straight kama hivi vinawashinda hawa jamaa, jee ingetokea watu kama hawa ndio wameshinda uchaguzi na kuikalia Ikulu yetu si ni ingekuwa ni majanga?. Kwa lugha nyingine, inawezekana Chadema ni Chama Majanga ila tuu watu walikuwa hawajui, hivyo mitikisiko kama hii ndio itawaonyesha wengine maeneo yenye matundu na jinsi nyumba yao inavyovuja.
Kama Chadema ndio chama kikuu cha upinzani kwa huku bara, jee tunaupinzani wowote wa kweli ambao ni serious, capable, credible, na reliable, wenye the ability and the capabilities wa kuiondoa CCM madarakani?!.
Paskali
Ni vema ukajisahihisha!