Ni Ubatili Mtupu Mpaka Basi!. CC ya CHADEMA ilipata wapi mamlaka?. Baraza Kuu halina mamlaka hiyo!. Je, inawezekana CHADEMA ni chama majanga ila?

Nashukuru mkuu angalau umejibu Kwa hoja
 
Pascal Mayalla Zitto aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu alifukuzwa kwa katiba hii hii.
It's true, Zitto alitimuliwa hivi hivi kama Mdee. CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya NKM, mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu na mamlaka yenye uwezo wa kumtimua ni Mkutano Mkuu. Zitto alitimuliwa kwa uonevu, karma ya uonevu huo kwa Zitto imeisha tembeza bakora zake, Chadema kama chama kimekula share yake na individual members wa Chadema nao wamekula bakora zao, tatizo ni hakuna a defined and a specific time frame ya malipo ya karma, unaweza kufanya ubaya leo ukalipwa kesho, na unaweza kufanya ubaya leo, ukalipwa miaka 10 baadae, sasa wakati wa malipo, utahesabu ni majanga tuu wala hutakumbuka ulifanyaga nini. Hata naniliu kaondoshwa kwa karma payback.

Ukiisha ijua karma, epuka dhulma na maonevu. Kati ya wabunge hao 19, not all wamehusika, wengine wameingizwa tuu hivyo kuwahukumu kwa mtindo wa tenga la samaki, mmoja akioza wote wameoza sio kuwatendea haki, karma lazima itawalipia!.
P
 
Unaanzaje kujibu huo utopolo? Umeona kuna vifungu vyovyote vya katiba ya Chadema ameambatanisha ili kusapoti hayo madai yake kuwa Mdee alipaswa kuchukuliwa nidhamu na Baraza Kuu?
Sasa kwa kufanya hivyo, ndiyo wewe na wenzako mumjibu kwa kutumia lugha za kuudhi? Jibu hoja zake kwa staha.

Vifungu vya katiba ya Chadema vinavyoonyesha udhaifu wa kimaamuzi vimewekwa kwenye uzi huu. Post namba 109. Jisomee mwenyewe.
 
Mkuu BURUTA , naunga mkono hoja, sio wana CCM wote wanapenda kucheza faulo, kwenye uchaguzi, hivyo hata CCM tunaishauri humu, tofauti ya CCM na Chadema, CCM ni sikivu sana. Hebu angalia bandiko hili, CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! nilitoa ushauri kwa both parties, CCM ikatekeleza ikalamba bingo, Chadema ikapuuza, ikaangukia pia!.

Kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa, angalia nilishauri nini Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa!

Baada ya uchaguzi huo nilisema Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Karma, hainaga cha mswalie Mtume wala haijui cha nani ni nani!.
P
 
Ni kweli Mayalla maana yake ni NJAA?
Ni kweli ila sio njaa ya tumbo inayohitaji mlo, ni njaa ya ukame, baa la njaa, Hunger drought, famines.
NB. Sio kila anayeongea Kisukuma ni Msukuma au kila anayezaliwa Usukumani ni Msukuma!, hivyo mtu kushindwa kutofautisha njaa ya tumbo na baa la njaa ni kawaida sana kwa impostors.
P
 
Lakini kwa namna kubwa hilo jina linaakisi tabia zako mkuu ...
 
Hivi Bro muda wa kuandikaandika mashuzi mareeeeefu humu JF unauyoaga wapi??
 
Jana nilimweleza Mnyika kuwa katiba yao sio halali sababu inanyima haki ya kikatiba ya nchi yaani kwenda mahakamani kudai haki. Wakati wao wanapiga domo kudai vitu havipo kwenye katiba mfano Rais ashitakiwe. Yaani wanafiki wakubwa MaCHADEMA.!
Wee Mzee Mdee, naona umevurugwa!
 
Yaani, hueleweki!
 
Sio vizuri kutoa siri za Mgonjwa.Siri ya ugonjwa ni daktari na mgonjwa tu.so usianike chochote tuendelee kuchangia uzi wake kwa hekima.
 
Achana na mambo ya karma kila mtu ana karma yake.

Zitto hakufika kwenye Baraza Kuu kwa sababu aliipeleka CC mahakamani naliposhindwa akawa amejifuta uanachama automatically kwahiyo hakuonewa alikiuka katiba ya chama.

Mdee na wenzake waliitwa na CC wakagoma wakakata rufaa ambayo Baraza Kuu ambalo ni hatua ya mwisho kwenye chama wakienda mahakamani watakuwa wamevunja katiba. Ni haki yao lkn hata kuomba tena uanachama itakuwa vigumu.

Soma katiba ya Chadema.

 
Brother P kwaelewa Chadomo ni kazi sana , lile ni kundi la vilaza wenye uthubutu wa kupambana, haiweze kama mkuu wa chama kufeli shule kwa kuzungusha zero aje awe mbadala wa CCM kusaidia taifa ,


CHADEMA kifutwe tu

USSR
Mkuu hebu tuwe wakweli wa nafsi zetu, kama JPM alishindwa kuifuta CDM! Utaweza wewe kwa maneno ukijificha nyuma ya keyboard?
 
Paskali nimesema mahala naona CHADEMA wanaelekezwa mahakamani
 
Pascal Mayalla
Juhudi zako zimeanza kujibu nimekuona umepewa kandarasi ya kuitangaza TARURA na kwa kasi hii utapewa ile ya Musiba ya ATCL
 
Paskali mayala aka Njaa huna uhalali wala dignity ya kuzungumzia mambo ya CHADEMA kwa sababu wewe una personal interest.Personal interest yako ni kuwa wewe ni Mwanachama hai wa CCM uliyetia nia ya Kugombea Ubunge -2020.Kwa maana hiyo hauko huru bali unafungamana na upande wa CCM nadhani umenielewa, binafisi natamani na kupenda taifa letu liheshimu Katiba, kanuni na sheria zetu za nchi lkn na zilizo Kwenye taasisi zingine kama vyama vya siasa au michezo kama TFF.
Kwenye issue ya hawa dada zetu hata mjinga anajua au kuelewa kuwa Kuna namna ilifanyika isiyo sahihi Kwa mfano mdogo sana yule dada aliyekuwa gerezani Nusrat nani alimtoa gerezani usiku ili akaape? nani alipeleka jina lake akiwa gerezani na nani? aliandaa nyaraka zake.Ila ukiamua kujitoa ufahamu unaweza ukaamua kubishi haina tatizo japo Ukweli unauona tena peupe kabisa.Ninazani hata wao CHADEMA inawauma kuwatimua wanachama 19.Ila kama wamekengeuka hakuna namna ni kama mguu ulioshambuliwa na Kansa huwa unakatwa lkn pindi unakatwa anayekatwa hapendi.Nazani hata CHADEMA hawapendi. Mfano mdogo sana Halima na Matiko wamepewa Ubunge wa viti maalumu na Chama chako mara kadhaa mbona bila shida huko nyuma.Mwisho hakuna mkubwa kuliko taasisi Lowasa alikatwa na CCM kwa masrahi mapana ya chama.Tusitetee upuuzi lazima Kila Mwanachama aheshimu katiba na taratibu za Chama chake kwani anaingia huko kwa hiari yake.
Mwisho kwa nini maneno mengi kwa CHADEMA lkn Lipumba wa CUF alivyofanya hivi haikuwa shida.
 
Mbona unaongea tu bila kuweka citation ya hivyo vifungu vya katiba ya chadema vilivyokiukuwa? This is an empty minded thread
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…