Ni Ubatili Mtupu Mpaka Basi!. CC ya CHADEMA ilipata wapi mamlaka?. Baraza Kuu halina mamlaka hiyo!. Je, inawezekana CHADEMA ni chama majanga ila?

Ni Ubatili Mtupu Mpaka Basi!. CC ya CHADEMA ilipata wapi mamlaka?. Baraza Kuu halina mamlaka hiyo!. Je, inawezekana CHADEMA ni chama majanga ila?

Hoja zako P ni sahihi lakini zinashutumiwa kwa lilelile nililowahi kukueleza wewe... upofu wa mahaba.... wote wanaoponda hawaangalii mantiki hawautaki ukweli wanabaki na chuki ambayo ni sumu mbaya sana kwenye haki. Katiba ya Chadema imevunjwa na sasa wanabaki na dhahania, matusi na kejeli.
Mnaacha kuangalia haki za kina Ben sanane mnaangalia haki za majizi yaliyofoji saini
 
Washauri hao wasaliti waende mahakamani na wewe ukajiunge jopo la utetezi.

Njaa kweli mbaya sana, epuka aibu ndogo ndogo mkuu zitakazokufedhehesha siku za usoni.

Hamjajifunza kesi ya Mbowe tu? CCM kweli kuna vichwa vigumu sana.
Muache apamp wenzie ujinga wakakutane na kibatala Ndio akadhibitishe Hiyo A yake aliyopewa na makanjanja wenzie.
 
Ahsante sana mtoa Hoja ,Ila ingependeza sana iwapo ungeweka vifungu vya Katiba ya chadema vinavyozuia mwenyekiti wa bawacha kujadiliwa na kikao chochote kile isipokua mkutano mkuu tu.ili tupate nafasi ya kuchangia vizuri Hoja yako.
 
Wanabodi,
Kwanza sio kila kitu ni siasa, vitu vingine ni hoja za kikatiba, Sheria, taratibu na kanuni.

Ukileta hoja specific, hakuna ubaya kujifagilia ubobezi wako katika eneo husika.

Mimi Paskali Mayalla ni Mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea, ila pia nilisomea sheria, LL.B, UDSM, ile kutua tuu UDSM, siku ya kwanza kipindi cha Kwanza ni LW 101, unajua mwalimu wangu wa kwanza kabisa UDSM ni nani?... ni Dr. Tulia Akson!.

Prof. Issa Gulamhussein Shivji na Palamagamba Kabudi, walitufundisha LW. 200 ndio yenye Katiba, nilifumua A, utadhani mtihani nilikuwa natunga mimi!. Hivyo kwenye hoja hii ya Katiba ya Chadema, mimi naizungumza as an authority.

Katiba ni kakitabu kadogo tuu, ila kukaelewa ni shughuli. Kabla ya chama chochote cha siasa kusajiliwa ni lazima kiwasilishe katiba yake kwa Msajili wa vyama, ipitiwe na wataalamu wa katiba, wajiridhishe kuwa iko sawa na inaendana na katiba ya nchi.

Hivyo hata Chadema, iliposajiliwa kwa mara ya kwanza ile 1992, iliwasilisha katiba fulani amaizing iliyokuwa nzuri kabisa, yenye kipengele cha ukomo wa uongozi mwisho ni vipindi viwili vya miaka 5 na mwanachama wa Chadema alikuwa huru kuitafuta haki yake mahakamani.

Mwaka 2006, Chadema wakafanya marekebisho ya Katiba na kuyasilisha ofisi ya msajili wa vyama, na ikakubaliwa.

Nilipoipitia katiba hiyo ya Chadema ya 2006, nikakuta kile kipengele cha ukomo wa uongozi, hakipo!, kimenyofolewa kinyemela!. Nilipokiulizia kipengele hicho humu jf, Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Slaa alinishukikia vilivyo na kukanusha kuwa Chadema halikuwahi kuwa na kipengele hicho!.

Hii maana yake ni hata Katibu Mkuu Chadema, alikuwa haijui Katiba ya chama chake!. Kama Katibu Mkuu ambaye ndie custodian wa katiba ya Chadema, haijui katiba hiyo, what do expect kwa the rest of the people?.

Baada ya Dr. Slaa kunishukia, aliyeninusuru ni JJ. Mnyika kukiri kifungu hicho kilikuwepo na sasa hakipo sio kuwa kimenyofolewa!, no!, bali ni hakikujadiliwa kabisa hivyo kikayeyuka tuu into thin air!

Katiba hiyo ya 2006 pia ikapenyeza kifungu ambacho kinakwenda kinyume cha katiba ya JMT kumzuia mwanachama wa Chadema kwenda mahakamani, akienda tuu ndio amejifukuzisha Chadema!.

Tukija kwenye hoja za bandiko hili ambazo mimi nimeziita Chadema ni ubatili, ubatili ubatili mtupu mpaka basi!. CC ya CDM haina mamlaka kumjadili Mwenyekiti wa Bawacha, kwasababu sio mamlaka yake ya nidhamu, CC hiyo ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumjadili na kumfuta uanachama Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee?!.

Mamlaka sahihi ya nidhamu ya Mwenyekiti wa Bawacha ni Baraza Kuu, na mamlaka yake yenye uwezo wa kumfuta uanachama Halima Mdee, ni Mkutano Mkuu pekee!. Sasa kwenye kikao cha juzi cha Baraza Kuu la Chadema, kuna mtu yoyote alisikia likijadil mashitaka yoyote ya Halima Mdee?. Ilichofanya Baraza Kuu ni kubariki maamuzi yale batili ya CC ya Chadema. Kitendo cha Baraza Kuu, kurudhia kuvuliwa uanachama wa Halima Mdee, Baraza Kuu lilipata wapi mamlaka hiyo?!.

Katiba ya Chadema ipo na imeweka taratibu na kanuni za mamlaka ya nidhamu, kwanini hazifuatwi?. Sasa vitu vidogo tuu na straight kama hivi vinawashinda hawa jamaa, jee ingetokea watu kama hawa ndio wameshinda uchaguzi na kuikalia Ikulu yetu si ni ingekuwa ni majanga?. Kwa lugha nyingine, inawezekana Chadema ni Chama Majanga ila tuu watu walikuwa hawajui, hivyo mitikisiko kama hii ndio itawaonyesha wengine maeneo yenye matundu na jinsi nyumba yao inavyovuja.

Kama Chadema ndio chama kikuu cha upinzani kwa huku bara, jee tunaupinzani wowote wa kweli ambao ni serious, capable, credible, na reliable, wenye the ability and the capabilities wa kuiondoa CCM madarakani?!.

Paskali
Amazing scriptue kaka Mayala.

Ukweli umeuweka na hakika asiyeelewa atapoteza muda kuupinga
 
Anaona madhaifu ya chadema ila haoni wizi wa kura uliofanywa na CCM 2020 au mauwaji ya Wana chadema ! Na kama chadema ni dhaifu kwanini mnaipambanisha na dola? We huoni think tank ya system inachagua viongozi vijana toka chadema na sio wajinga kama wewe au uvccm?
 
Hatuna upinzani credible! Tuna watu ambao mbele ya kamera ni wapinzani lakini mlango wa nyuma wanapokea maelekezo Lumumba na from within kuna mtu mmoja ndio Katiba, ndio hakimu!

Itachukua muda sana kupata chama credible kisicho na makando ya kilumumba! Huku chini kwa machawa wanacharurana wenzao jioni wanagonga mvinyo na kuyajenga! Ndio maana alipokuja mtu asiye na chembe za unafiki kama JPM kuna watu walijikutana kapu moja na hawakushangaana what happened [emoji23]
 
Ifike mahali tuheshimu taratibu na sheria tulizojiwekea!

Yani kabisa Pascal Mayalla kwa usomi huo na majigambo ya kutuonesha umefundishwa na nani unaamini kabisa wapinzani CHADEMA wamefanya KOSA KUBWA la kwanza na sio WALIOFUKUZWA kama wakosaji wa kwanza katika saga hii?

Kunanyakati mtu unafikia kutokusoma andishi la mtu flani kwa sababu ya kuwa na mitizamo ambayo hujaribu kupaka mafuta kinyesi!
Amepewa rushwa na akina Halima awasaidie kupiga debe, nenda na akina Halima umoja party kwani lazima wawe wanachama wa CHADEMA?
 
Ni mtazamo tu!

Vyama vya Siasa vinaongozwa kisiasa na si kidikteta wala vinginevyo.

Siasa ina take and give, gain and lose na inaongozwa kwa masahuriano na sio kuwa rigid ka Sheria!

Vyama vyote vya siasa duniani kote vinafanya siasa za kimashauriano na chama tawala katika mambo agharabu pale yanapoguswa maslahi ya nchi. Hukaa na kuteta pamoja kuona namna gani jambo liendwe ilhali katika win win situation.

Ni upuuzi kuwa na chama cha siasa kisichotaka mashauriano. Hicho kitakuwa si chama cha siasa bali wahuni tu kama M23 au kama kikundi kinachoongozwa na Joseph kony!

Kwamba wewe unaona siasa za kimariadhiano ni upuuzi kwamba ni kuchukua maelekezo ya chama tawala?

Na kwamba JPM hakuwa mnafiq kwenye kauli na matendo yake?...tukiwa tumelewa upenzi na uhusudu juu ya mtu flani, furaha zetu zibaki katika vyumba vya mioyo yetu na si kuropaka kuwaona wengine kama machawa na wasiojua jambo.

Kwa namna yeyote ile kama ulikuwa mfaidika wa utawala uliopita, endelea kufaidi lakini usitumie nafasi na muda kuwatusi wale wanaofaidi na kufurahia utawala wa leo.
 
Harafu mbona siafu wa kijani mmeumia na kufurushwa hao covid? . shida ni nini magamba !!?. Mbona nyinyi maCCM mlimtimua Sofia simba hamkuingiliwa wala kupangiwa na mtu. Mbona mlimtimua Membe watu hawakupiga kelele !?. Lumumba tangu lini mliona Chadema wanatenda ya kuwafurahisha !. Mliwaweka vibaraka ndani ya chadema , Leo wameshitukiwa na kutimuliwa mnatoa povu. Kama mnaona wana potential si muwapokee huko Lumumba !?. Mbowe shikilia hapo hapo usiachilie .
Wamepewa rushwa na akina Halima kuja kuwatetea ndiyo maana ametoa shingo tangu last week na wala hana point, mtu na akili zako ufundishwe chuo na Tulia au Kabudi na wewe ujiite una akili we si sawa na mfu asee
 
Back
Top Bottom