Omona Wanyu
Member
- Feb 29, 2012
- 51
- 6
Vijana tusiwe na ugonjwa wa fikra duni, ni jambo la kipumbavu wewe kama kijana unayejiita msomi na unae tegemewa na jamii yako, kuanza kuvibagua vyuo vingine kwamba si vyuo bali ni taasisi za kuelimishia vilaza, mfano mtu kabisa anasimama na kusema "Tanzania Chuo kikuu pekee ni UDSM", au "Tumaini nacho chuo" "SAUT ndio nini?" au "UDOM ni chuo cha kata" huo kimsingi ni mtindio wa kufikilia unaochagizwa na ujuha wa mawazo na kimsingi elimu yako haijakusaidia, ni jambo la kipuuzi kuvibeza na kuvibagua vyuo kwa reasoning isiyo na mantiki, Tungeonekana wasomi sana na wazalendo kama tungevishindanisha vyuo vyetu katika maswala ya utafiti na uvumbuzi katika tasnia mbalimbali kama Chemical Engineering, Nuclear Physics, Social Science....nk nisiwachoshe na maneno mengi kimsingi, watu makini hupima Ubora wa Mhitimu kwa kuzingatia Uwezo alio nao na si Chuo alichosomea!