Ni uhakika kwamba waliotekwa karibu wote tayari wamekufa

Ni uhakika kwamba waliotekwa karibu wote tayari wamekufa

PhD

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2009
Posts
4,923
Reaction score
4,594
Nimetaarifiwa rasmi kuwa karibu watu wote waliotekwa wamkwishakufa, kutokana na mateso, kuugua kwa sabababu ya majeraha wakati wa kutekwa kwao na pia wengine wawili walikufa kutokana na sonona ya huko walipohifadhiwa.

Haya yote yamefanyika ili baadhi ya watu waendelee kupata haya:
1. Misafara kwenye kazi zao
2. Mali kama fedha na majumba
3. Heshima ya kuabudiwa na binadamu washenzi
4. Kufanya ngono na wanaume au wanawake wawapendao na wengine mapenzi ya jinsia moja
5. Ufahari katika ulimwengu huu wa giza
6. Fursa za kuzunguka ulimwenguni

Mwisho niwakumbushe haya:

Aya za Biblia​

  1. Kutoka 20:13
    “Usiue.”
  2. Mwanzo 9:6
    “Amwagaye damu ya mwanadamu, damu yake itamwagwa na mwanadamu; kwa maana Mungu alimfanya mwanadamu kwa mfano wake.”
  3. Mathayo 5:21-22
    “Yesu alisema: ‘Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue; na kila atauaye atahukumiwa.’”
  4. Warumi 12:19
    “Msijilipizie kisasi wenyewe… kwa maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, asema Bwana.”

Aya za Quran​

  1. Surah Al-Ma’idah 5:32
    “Yeyote atakayemuua mtu bila ya sababu ya haki… basi ni kama amewaua watu wote; na atakayemuokoa mtu mmoja, ni kama amewaokoa watu wote.”
  2. Surah An-Nisa 4:93
    “Na mwenye kumuua Muumini kwa makusudi, basi malipo yake ni Jahannam, atadumu humo; na Mwenyezi Mungu amemkasirikia na kumlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.”
  3. Surah Al-Isra 17:33
    “Wala msiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameiharamisha, isipokuwa kwa haki.”
Aya hizi zinaonyesha kuwa katika dini zote mbili kuu—Ukristo na Uislamu—kuua bila haki ni dhambi kubwa inayofuatwa na hukumu, laana au adhabu kutoka kwa Mungu.

Kwa wapendwa wetu, BEN SAA NANE, AZAVORY GWANDA, MDUDE NYAGALI, HAMPHREY POLEPOLE, SOKA, MASHAHIDI WA OKTOBA 29, 2025 kwa ujumla wenu, MZEE KIBAO na wengineo wengi, damu zenu zinalia kutoka ardhini, Mungu asiyeshindwa atawalipia mateso makubwa mliyopitia.
 
Na ww umekosea.

Sio karibia.
Sema wote waliotekwa na wakakaa zaid ya mwez bila kuonekana jua wameshakufa.

Na wale waojiuliza wanaoteka ni akina nani.
  • bas tutafakar kwann Roma alivyoachiwa tu akahama nchi.
  • Kwanini Mo Dewji alivyoachiwa hakwenda hata polisi kuandika maelezo na hadi leo hatak kugusia suala lake la kutekwa kwenye vyombo vya habar.
 
Tunavyovipigania, vyoote tutakufa tutaviacha, mali, madaraka, watoto, heshima na kila kitu....tume alisema kaburini unaenda na matendo yako tu. Sasa tujitahidi kufanya mema, tupendaen ya nini kuua mtu kisa cheo, cheo ambacho hutaishi nacho milele.

Mambo mengi yanafanyika sababu ya uchache wa imani tu na ukosefu wa fikra
 
Watakeji wanajulikana bayana
 
Exactly Leo unalala mzima kesho unakua rip
 
Watu duniani tunapita ila kwa tamaa wakati wanaishi hapa wanataka karibia kila kitu kiwe miliki yao
Si mbaya kutamani kila kitu, binadamu tumeumbiwa tamaa,
Tunatamani kula vizuri, kulala pazuri, pesa nyingi, wanawake warembo etc..
Je unavipata vipi ni halali? Kwanini umdhuru mtu kisa wewe ulale pazuri? Leo unadhulumu ardhi kesho unakufa unazikwa nayo...

Kikubwa hapa ni watu hawana fikra, hawana hofu, hawakumbuki kifo.
Mtume alisema kifo ni mawaidha tosha, ambae atakikumbuka kifo lakini moyo wake usishtuke hata kidogo, dah, huyo tumuweke fungu gani sijui
 
Si mbaya kutamani kila kitu, binadamu tumeumbiwa tamaa,
Tunatamani kula vizuri, kulala pazuri, pesa nyingi, wanawake warembo etc.
exactly
.
Je unavipata vipi ni halali? Kwanini umdhuru mtu kisa wewe ulale pazuri? Leo unadhulumu ardhi kesho unakufa unazikwa nayo..
Imagine
Kikubwa hapa ni watu hawana fikra, hawana hofu, hawakumbuki kifo.
Watu kama wanyama wa mwituni
Mtume alisema kifo ni mawaidha tosha, ambae atakikumbuka kifo lakini moyo wake usishtuke hata kidogo, dah, huyo tumuweke fungu gani sijui
Inafikirisha
 
Back
Top Bottom