Ni uhakika kwamba waliotekwa karibu wote tayari wamekufa

Ni uhakika kwamba waliotekwa karibu wote tayari wamekufa

Tunavyovipigania, vyoote tutakufa tutaviacha, mali, madaraka, watoto, heshima na kila kitu....tume alisema kaburini unaenda na matendo yako tu. Sasa tujitahidi kufanya mema, tupendaen ya nini kuua mtu kisa cheo, cheo ambacho hutaishi nacho milele.

Mambo mengi yanafanyika sababu ya uchache wa imani tu na ukosefu wa fikra
Pamoja nakuviacha ni muhimu vipatikane kwa udi na uvumba
 
Nimetaarifiwa rasmi kuwa karibu watu wote waliotekwa wamkwishakufa, kutokana na mateso, kuugua kwa sabababu ya majeraha wakati wa kutekwa kwao na pia wengine wawili walikufa kutokana na sonona ya huko walipohifadhiwa.

Haya yote yamefanyika ili baadhi ya watu waendelee kupata haya:
1. Misafara kwenye kazi zao
2. Mali kama fedha na majumba
3. Heshima ya kuabudiwa na binadamu washenzi
4. Kufanya ngono na wanaume au wanawake wawapendao na wengine mapenzi ya jinsia moja
5. Ufahari katika ulimwengu huu wa giza
6. Fursa za kuzunguka ulimwenguni

Mwisho niwakumbushe haya:

Aya za Biblia​

  1. Kutoka 20:13
    “Usiue.”
  2. Mwanzo 9:6
    “Amwagaye damu ya mwanadamu, damu yake itamwagwa na mwanadamu; kwa maana Mungu alimfanya mwanadamu kwa mfano wake.”
  3. Mathayo 5:21-22
    “Yesu alisema: ‘Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue; na kila atauaye atahukumiwa.’”
  4. Warumi 12:19
    “Msijilipizie kisasi wenyewe… kwa maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, asema Bwana.”

Aya za Quran​

  1. Surah Al-Ma’idah 5:32
    “Yeyote atakayemuua mtu bila ya sababu ya haki… basi ni kama amewaua watu wote; na atakayemuokoa mtu mmoja, ni kama amewaokoa watu wote.”
  2. Surah An-Nisa 4:93
    “Na mwenye kumuua Muumini kwa makusudi, basi malipo yake ni Jahannam, atadumu humo; na Mwenyezi Mungu amemkasirikia na kumlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.”
  3. Surah Al-Isra 17:33
    “Wala msiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameiharamisha, isipokuwa kwa haki.”
Aya hizi zinaonyesha kuwa katika dini zote mbili kuu—Ukristo na Uislamu—kuua bila haki ni dhambi kubwa inayofuatwa na hukumu, laana au adhabu kutoka kwa Mungu.

Kwa wapendwa wetu, BEN SAA NANE, AZAVORY GWANDA, MDUDE NYAGALI, HAMPHREY POLEPOLE, SOKA, MASHAHIDI WA OKTOBA 29, 2025 kwa ujumla wenu, MZEE KIBAO na wengineo wengi, damu zenu zinalia kutoka ardhini, Mungu asiyeshindwa atawalipia mateso makubwa mliyopitia.
My friends, ladies and gentlemen,
unafiki kuhusu hizo drama na hiyo michezo sidhani kama vinampeleka mtu peponi, ni kujidanganya tu mbele ya jukwaa na mitandaoni ya kijamii, kwamba fulani ana uchungu au huruma sana kumbe ni unafiki mtupu, anatafuta tension tu jukwaani.

Nadhani ingefaa zaidi huo uhakika wa hiyo porojo kusaidia hizo familia angalau hata kuona mabaki tu ya miili ya ndugu zao uliothibitisha wameuawa yalipo,
lakini kinyume na hapo nadhani unakoleza majonzi na kuzidisha huzuni zaidi kwenye familia husika, na hiyo inawatia mashaka na pengine inawathibitishia wazi kwamba, huenda nawe unasaidia kikamilifu kudhulumu haki na stahiki za wapendwa wao, waliodhulumiwa kwa hizo drama, lakini pia unafubaza na kuwavunja moyo kabisa jitihada za familia dhidi ya juhudi zao za kusaka wapendwa wao.

Sidhani kama unafiki wa aina hiyo ni faraja kwa waliopotelewa na ndugu zao bali maumivu makali zaidi na msongo wa mawazo, juu ya kwanini mtoa hoja huwaambii wala kuwapa uhakika wanafamilia juu ya wapendwa wao walipofichwa, bali una uhakika tu kwamba wameshakufa?

Huenda wanafamilia waliopoteza ndugu zao hivi sasa wanatamani kumuuliza mtoa hoja, kwamba,

kamanda,
Tuonyeshe basi walipofia ndugu zetu na ilikuaje? Na mbona unatupa uhakika wa kufa tu, si utupe na uhakika wa ilikuaje na wamezikwa ama laa?

Unafiki unaumiza sana wajemeni, tupunguze hiyo nonsense hata kama ni kutafuta kiki.🐒
 
My friends, ladies and gentlemen,
unafiki kuhusu hizo drama na hiyo michezo sidhani kama vinampeleka mtu peponi, ni kujidanganya tu mbele ya jukwaa na mitandaoni ya kijamii, kwamba fulani ana uchungu au huruma sana kumbe ni unafiki mtupu, anatafuta tension tu jukwaani.

Nadhani ingefaa zaidi huo uhakika wa hiyo porojo kusaidia hizo familia angalau hata kuona mabaki tu ya miili ya ndugu zao uliothibitisha wameuawa yalipo,
lakini kinyume na hapo nadhani unakoleza majonzi na kuzidisha huzuni zaidi kwenye familia husika, na hiyo inawatia mashaka na pengine inawathibitishia wazi kwamba, huenda nawe unasaidia kikamilifu kudhulumu haki na stahiki za wapendwa wao, waliodhulumiwa kwa hizo drama, lakini pia unafubaza na kuwavunja moyo kabisa jitihada za familia dhidi ya juhudi zao za kusaka wapendwa wao.

Sidhani kama unafiki wa aina hiyo ni faraja kwa waliopotelewa na ndugu zao bali maumivu makali zaidi na msongo wa mawazo, juu ya kwanini huwaambii wapendwa wao walipofichwa bali una uhakika tu kwamba wameshakufa?

Tuonyeshe basi walipofia ndugu zetu na ilikuaje? Mbona unatupa uhakika wa kufa tu Tupe na uhakika wa ilikuaje na wamezikwa ama laa.
Unafiki unaumiza sana wajemeni 🐒
Bado kitambo kifupi, pazia la hekaluni litachanika na kila kitu kitakuwa wazi. Yote mliyodhani mmeyaficha yatawekwa hadharani na hapo ndiyo mtajua vizuri hasira za WaTanzania.
 
Bado kitambo kifupi, pazia la hekaluni litachanika na kila kitu kitakuwa wazi. Yote mliyodhani mmeyaficha yatawekwa hadharani na hapo ndiyo mtajua vizuri hasira za WaTanzania.
sasa tizama porojo kama hizo,
huu si unafiki wa kiwango cha juu kabisa kama mafarisayo tu gentleman?

ili uonekane jukwaani sio? Itakufaa au kufaidi nini sasa kwa mfano?🐒
 
Kuweza kufanya haimaanishi ni haki..
Mzee unauaje mtu ili upate tu madaraka..
Mie nina majumba kibao, mashamba bwelele kwanini nimdhulumu yatima shamba lake la urithi kule KIZIMKAZI?
Hii ni sawa kisa tu dunia ni survival of the fittest?
Ni kweli unayosema ila ni kama dunia inachagua wenye nguvu na wanyonge wanaangamia na kutoweka , kama wasipo jipambania , hiyo ndio survival of the fittest.
 
Kwahiyo ile dhana ya kusema watu wasiojulikana tuifute. Si ndio
WASIOJULIKANA ni jina tu walilopewa Mafwele na genge lake lakini ukweli ni kwamba wanajulikana na anayetewatuma na kuwalinda wawe juu ya sheria za nchi ni Samia.
Kuna watu wasio rasmi(si waajiriwa wa serikali ie; Abdul) lakini wanahusika moja kwa moja katika kuchagua wahanga wa kuwateka na funding and facilitating katika kufanikisha utekaji.
 
Back
Top Bottom