Ndiyo, ni ujinga na ujuha Mkubwa kwa wana CCM wachache wanaoamini kuwa, bila kuviponda na kudhihaki kazi za Hayati JPM na hata kumdhihaki yeye mwenyewe JPM, watu hawatatega masikio yao kusikia yale anafanya Rais Samia kwa sasa! Au kumsikiliza.
Kwani kinachofanywa na wana CCM wahuni, kuponda na kuzodoa kazi zilizofanywa kwa ushirikiano wa JPM na aliyekuwa Makamo wa Rais ambaye sasa ndiye Rais wa TZ, kina maana gani? Kama sio akili fupi kudhani wasipofanya hivyo, maana yake itakuwa vigumu kwa watanzania wengi sana kurudisha masikio yao kwa rais wa sasa!
Je? Akili yao wanaamini kiatu kile cha JPM ni kikubwa mno kwa maana hiyo wanaamua kukipunguza kikatili kwa mafyekeo na mapanga?
Swali langu ni kwamba kwa hao wana CCM wajinga wajinga wenye kuamini hivyo!
Je, JPM alikuwa Rais kupitia chama gani?
Je, Mh Rais aliyepo sasa, anaongoza Serikali kupitia chama gani?
Je, JPM, alikuwa akitekeleza ilani ya chama gani, na Je, Mh Samia, anatekereza Ilani ya chama gani?
Kwa akili zenu fupi, Mnadhani sasa, mkimchafua JPM, macho ya Watanzania yatapigwa upofu yasiuone ujenzi wa SGR na JKHP?
Mnataka wafumbe macho ili wasione zile hospitali za Rufaa Chatto, Mara, vituo vya afya, madege Yale, na mageuzi makubwa katika kila wizara?
Mnafikiri kwamba, Watanzania ni wepesi hivyo kusahau na wajinga kama mlivyo nyinyi chawa msiojua ni kitu kipi cha kujivunia kwa chama chenu ovu?
Chama ambacho ilikuwa ukivaa sare za CCM unazomewa na hata watoto mitaani?
Chama ambacho karibu kila mmoja alikuwa amechafuka kwa uwizi na kujilimbikizia Mali?
Na kwa tarifa yenu, subirini 2025
Watanzania hawajasahau uovu wenu na mnaoendelea kumchafua kiongozi aliyeleta unafuu kwa wanyonge wengi kupenda nchi na kufanya kazi zao kwa amani bila bughudha
Nchi ilifikia mahali, masikini ndio wanaofungwa wao tu magerezani
Masikini walikuwa wakilima, yie mnavuna?
Wakila, nyie ndio mnashiba?
Mkiugua nyie, wao ndio wanakufa?
Wakinunua viwanja, nyie mnajenga na kuwasweka magerezani kwa jeuri ya fedha zenu, Masikini ilikuwa hawezi kupata haki kokote?
Mnadhani ni chepesi vile kwao kumsahau JPM
Tafadhari, muunganisheni Mama kwenye cheni hiyo ya mambo mazuri walioyafanya wakiwa wrote! kamwe msimtenge nayo enyi chawa wa CCM!