Kutengeneza urafiki kwanza huku ukiwa unampenda mwanamke kimapenzi ni ishara ya udhaifu na uoga wa REJECTION.
Tongoza mapema kabla hamjazoeana sana ili hata akikataa kusiwe na yale maumivu ya kumzoea, lakini pia Mwanamke akiwa rafiki yako ni lazima atajua vitu vingi sana kuhusu wewe na maisha yako, who knows? Pengine kwenye characters zako au baadhi ya mambo yako yanaweza kumfanya asikuwazie kama mtu unayeweza kuwa mwanaume wake, tofauti na ambapo atayajua mkiwa kwenye mapenzi tayari (anaweza kukuvumilia ubadilike taratibu).
Ingawa kuna marafiki zetu wa kike wanatakiwa kubaki kama marafiki tu, sio kila mwanamke anayekuwa karibu na wewe basi aliwe.