Hatujachagua upande wa kushabikia dhidi ya upande mwingine. Ni dhana yako labda kwa kuona watu wanahoji walichotangulia kukifanya Hamas dhidi ya Israel.
Ni hivi. Mambo ya uhamiaji yamekuepo kwa mataifa yote. Jamii dhidi ya jamii. Mfano kuna makaburu karibuni Million 5 huko S. Africa ambao walihamia pale karne nyingi zilizopita. Je leo uwafukuze warudi wapi ?!. Ikiwa walikotoka babu zao hata kumbukumbu zao hazipo. Na hiki cha sasa ni kizazi kilichozaliwa Africa kusini. Utawapereka wapi ?!. The same na waarabu walioko Zanzibar na hata bara je kuna nafasi zao huko Oman tena leo hii ?!. Wahindi waliozagaa Tanganyika na visiwani je wanazo nafasi za kuwarudisha India leo hii ?!. Je makabila yetu ya mipakani, iliyoingiliana na watu wa mataifa jirani. Je leo tuwakatae kwa sababu zozote zile ?!. Tutakuwa taifa la namna gani ?
Mwl kwa hekima alisema wote waliokutwa na uhuru hapa, ni waTanganyika (Tanzania). Hiyo iliondoa pressure za uhasama, dhidi ya jamii za wachache.
Kuhusu mambo ya itikadi ukabila, imani za dini tofauti tofauti. Ni kukubali kuishi pamoja kwa kuvumiliana. The same leo Tanzania tunazo itikadi tofauti, imani tofauti, mila tofauti na hata asili tofauti. Lakini tunavumiliana na kila moja anafuata hamsini zake. Hicho kitu ndicho kinachotakiwa ktk eneo lile la wayahudi na Wafilisti. Kukubali kukaa pamoja kwa kuvumilana. Lakini ukimtafuta wa kumhamisha leo unaleta vita visivyoisha. Ndiyo hiyo utaona na watoto wanauliwa. Kwani vita havina macho.