Kuufuta uongo ni kutumia mbinu ya Russia, na Uingereza kwa kuwezesha mashirika yao ya habari kujitanua ulimwenguni. Wengi mnazijua RT na BBC ni vyombo vilivyochini ya serikali ya nchi hizo tajwa. Vyombo hivi vimesaidiwa kupata vibali vya kurusha matangazo kwenye maeneo ambayo nchi hizo zinadhani zinachafuliwa ama masalahi yake yaweza kuhatarishwa. Vyombo hivi vimefanya kazi kubwa sana kutimiza azma ya serikali hizo.
Ni kwa mtaji huu, binafsi nafikiri Serikali ya Tanzania iliwezeshe shirika la utangazaji la taifa TBC kupata leseni za matangazo huko huko kwenye mataifa tunapodhani tunahujumiwa kwa uongo. Shirika liwezeshwe kuboresha viwango vya watangazaji wake na hata kwa kupata watangazaji bora kutoka kwenye mashirika mengine makubwa ili kukidhi vigezo vya kuimarisha mbinu za kufuta uongo.
Hii itasaidia sana kumuwezesha rais wetu mpendwa Mama Samia KUENDELEA kufanya Kazi nyingine za kuboresha uchumi wa Taifa hili kwa ujumla.