Ni uongo gani unaoenezwa duniani kuhusu Tanzania?

Ni uongo gani unaoenezwa duniani kuhusu Tanzania?

Nilimsikia Rais akisema filamu tunayoitengeneza inakwenda kufuta uongo unaoenezwa duniani kuhusu Tanzania.

Niwaombe wadau mnisaidie kujua ni uongo gani hip? Ni nani wanaeneza? Je, filamu pekee inatosha kufuta huo uongo?
Hivi ni nani anayemwamini huyu mama ?
 
Demokrasia
kwahiyo katika makumi ya barozi nchini hapa walioona na kuumizwa na mwenendo wa demokrasia ni hao peke yao!!!mna marafiki wa aina gani nyinyi??

wakaendeleze kilimo cha ng'ombe huko wasitusumbue.
 
Tanzania kuna Amani wakati wananchi hawajawahi kupiga kura.

Hili nalo neno.Tuna madiwani ambao hatujawachagua,tuna Wabunge ambao hatujawachagua.Mbaya zaidi tuna kiongozi Mkuu ambaye ajachaguliwa na wananchi bali mfumo mbovu ulioambatana na wizi mkubwa wa kura kwa usaidizi wa vyombo vya dola.
 
Uongo mwingine ni wanaosema eti mama anauoiga mwingi, huo ni uingo 100%
 
TBC hii hii ambayo hata WaTz hatuangalii.?
Tunataka hata ninyi watanzania wachache ambao hamuiangalii muiangalie baada ya serikali kufanyia kazi mapendekezo yangu na yale mapendekezo ya wadau wengine. Hii inaweza kufanyiwa kazi kama serikali itaifikiria TBC kama shirika la kulifaidisha taifa lote la Tanzania badala ya suala linaloelekea kufanana na kufaidisha wanaserikali wachache.

Najua mapendekezo yangu na ya wengine katika kuiboresha TBC kuwa shirika lenye tija kubwa kwa taifa linaweza kupigwa vita na wale wanaoonekana kama wanaserikali wachache wafaidi TBC. Pia mapendekezo haya yatapigwa vita na incompetent, lazy, and greedy private broadcasting cooperations zilizopo nchini na nje ya nchi.
 
Nilimsikia Rais akisema filamu tunayoitengeneza inakwenda kufuta uongo unaoenezwa duniani kuhusu Tanzania.

Niwaombe wadau mnisaidie kujua ni uongo gani hip? Ni nani wanaeneza? Je, filamu pekee inatosha kufuta huo uongo?
Kama una vigezo vya kutosha omba nafasi ili udahiliwe chuo kikuu ukachukie shahada ya Uzamivu na katika tafiti yako ihusu 'uongo unaoenezwa huko nje kuhusu Tanzania.Kupitia tafiti zako utapata majibu yote na ya ziada.
 
Nilimsikia Rais akisema filamu tunayoitengeneza inakwenda kufuta uongo unaoenezwa duniani kuhusu Tanzania.

Niwaombe wadau mnisaidie kujua ni uongo gani hip? Ni nani wanaeneza? Je, filamu pekee inatosha kufuta huo uongo?
Nadhani anadanganywa tu. Nakumbuka Aljazeera walishaomba wafungue kituo cha kimataifa ukanda huu tukawakatalia. Hatutaki dunia itujue... lakini maajabu tunatengeneza filamu za maisha ya kifahari "royal tour", ili tukaudanganye ulimwengu?

Tanzania itabaki kama ilivyo, hata tutumie nguvu ya aina gani kuilazimisha dunia ituelewe tofauti na tulivyo.

Kinachotakiwa ni kuishi kwa ukweli, haki, uhalisia, na kushirikisha wananchi kwenye mipango na maendeleo. Tusijidanganye.
 
nani mzamini wa hii tuwa ? Mara paap unasikia serikali imetumia bilioni elfu kukamilisha igizo hili.
 
Back
Top Bottom