Ni upi ukweli kuhusu Nguva (Samaki mtu)?

Ni upi ukweli kuhusu Nguva (Samaki mtu)?

Jamani kumbe tulikuwa tunadanganyana sana kuwa samaki aina ya nguva ana umbo kama msichana mrembo sehemu ya kukatia kiunoni kwenda juu na kwenda chini samaki.

Huu ni uongo mtupu wa hadithi, ukweli ni kwamba nguva ni samaki mkubwa mwenye umbo la samaki ila sehemu ya kichwani hasa mdomoni anafanana kila kitu na ng'ombe na kitaalam anaitwa NG'OMBE BAHARI.

Huu ndio ukweli wa nguva, ukitaka ushahidi kamili nenda pale posta makumbusho ya taifa utamuona huyu samaki nguva na utakubaliana nami.

Mkuu Siku Entrance Wanataka Tuchangie Tsh Ngapi Pale?
 
Jamani kiumbe huyu inasemekana yupo kutokana na ushahidi wa footage za mashuhuda.tembeleeni youtube mtaweza kuona baadhi ya video clip za kiumbe huyu.japokuwa bado kuna debate kutokana na kwamba jamii kubwa bado haijawahi kumshudia kwani ni nadra sana kuonekana.
 
Nguva wapo ila kukutana nae ni bahat sana so wazungu walokutana nao ndo wao wamramua kuiga kijitengeneza lakin nguva mwenyewe hadi mokono yake ina kama magamba ya samaki kabisa
 
... Nyie TeamYoutube, Mnaamini kila mnachoona kwenye Youtube?? Mnafahamu kuwa huko kuna wajinga wajinga wengi tu ambao kazi yao ni kutengeneza na kupost vitu visivyokuwa na kichwa wala miguu? Kalageni baho...!
 
Wanabodi,
Kwa Mwenye elimu juu ya viumbe hawa karibu utupe somo

Viumbe hawa wana uhusiano gani maana huyu nguva kwa mjibu wa taarifa anasura nzuri ya msichana tena mpole chini anatisha sana na mazingira yake ni sawa na majini

Nawasilisha.
 
Wale wajuzi wa viumbe maji njoni hapa mtujuzee!!je nguva wapo au ni story tu
 
Habar za nguva ni za kusadikika tuu hazina ukweli
 
Wanabodi,
Kwa Mwenye elimu juu ya viumbe hawa karibu utupe somo

Viumbe hawa wana uhusiano gani maana huyu nguva kwa mjibu wa taarifa anasura nzuri ya msichana tena mpole chini anatisha sana na mazingira yake ni sawa na majini

Nawasilisha.
ni uzushi...google..mermaid uone
 
Kuna huyu samaki wa ajabu ambaye nasikia anapatikana baharini na mara nyingi anafananishwa na jinsia ya kike,inasemekana kuanzia kiunoni kuja juu ni mtu tena 'ke' na kuanzia kiunoni kwenda chini ni samaki,hivi ni kweli yupo samaki wa aina hiyo au ni simulizi tu?
 
Back
Top Bottom