Nakumbuka mwaka 2001, nikiwa Morogoro, nilipata dili la matikiti Dar. Kuna mteja alihitaji matikiti 500, kila moja buku. Sasa mie nikayasaka nikapata kwa mia nne na muuzaji alikuwa na tikiti ka 800. Sasa issue ilikuwa nina Tsh 60,000 mfukoni. Nikaamua kwenda kwa rafiki yangu Nsindi. Huyu jamaa alikuwa na bucha na yeye ni mwenyeji wa Gamasala Tarime.
Sasa jamaa ni mkorofi haswa na wengi walimwogopa ila mie tulielewana japo kwa manati. Nikamuomba aniazime laki nne na nusu na nitamrudishia asubuhi. Jamaa nikamuelezea dili lenyewe na kumsihi sana aniazime. Akakubali ila kwa sharti kesho 12 asubuhi ataifuata ili akanunue ng'ombe machinjioni. Nilitoka hapo nduki na baiskeli kuelekea kwa mkulima wa matikiti.
Tobaaa, nilipofika, mkulima akaniambia kayauza yote kwa 450, nilimaindi ila nikaamua kurudisha pesa ya Mkurya. Heee, ile kujikagua nikakuta mfukoni kuna coin ya shilingi 20 tu! Nilivurugika. Nilizitafuta hizo jela mpaka kwenye Ndala nilizovaa.
Sasa Usiku huo, sikulala kabisa, nikawazaaa namwambiaje jamaa. Nilistuka saa 11 alfajili nagongewa mlango na sauti ya mkurya.
Je, wewe ni tukio gani lilikufanya usilale?