Ni vigezo gani unatumia kutathmini ubora wa kazi iliyofanyika?

Kazi inaitwa bora baada ya kufia vigezo vilivyowekwa awali kwa asilimia πŸ’―

Kama kazi ilikua na vipengele 5
Ukavifanya kwa usahihi

Na kama maks kila kipengele ni 1
na wewe umefanya kwa ubora vipengele vyote vitano
Unakua umepata 5/5
Hapo imefanya vizuri umefanya kazi bora
 
Hakuna kazi isiyokuwa na vipimo mkuu. Kwa mfano, mtu wa customer care akipewa kazi ya kuongea na wateja online akaambiwa kwa siku anapaswa kuhudumia wateja 300 na kila mteja mmoja anapaswa kuongea naye kwa wastani wa dakika 2 lakini yeye akaweza kuhudumia wastani wa wateja 150 kwa siku na muda wake wa kuongea ukawa dakika 4, hasi huyo mtu anafanya kazi chini ya viwango kwa 50%.
 
Ubora wa kazi hupimwa kwa kazi husika kupitia kwenye mlolongo ufuatao:
1: Kuweka lengo la kazi husika/matokeo.

2: Kutanabaisha ubora wa kazi husika itakapokuwa imekamilika, unataka iwe na vigezo vipi?

3: Kutanabaisha hatua mahsusi za utendaji kazi husika na wahusika (SOP).

4: Kutekeleza kazi husika kwa kufuata taratibu mahsusi zilizowekwa hatua kwa hatua.

5: Kupima matokeo/evaluation ya kazi dhidi ya vigezo vya ubora uliotarajiwa/ vilivyowekwa pale juu.

NB: Mzunguko huu huanza upya kwa kuzingatia matokeo yaliyopatikana kwa kuimarisha au kurekebisha baadhi ya hatua ndani ya utekelezaji.

Pia, kwa baadhi ya maeneo ya kazi kuna vitengo mahsusi vya kuweka ubora na kufatilia ubora wa kazi kila wakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…